Utaifa, Uchama na Upinzani katika Siasa za Tanzania

sun wu

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
2,020
1,419
Taifa Kwanza…, Chama Baadae.., Ni kauli nzito na ya kuunga mkono ambayo nimesikia wabunge wakiisema mmojawapo akiwa Zitto.., (ninakubaliana nayo kwa asilimia 100)

Tusimamie serikali, ikikosea tuisahihishe, (ikifanikiwa tuipongeze).., Je kauli hii inafaa kutoka kwa mbunge wa upinzani (je chama tawala kinahitaji cheer leaders wa kuwapongeza) au kazi ya upinzani ni kupinga na kufichua maovu ya serikali tu (yaani kupinga).

Je umefika wakati wa Wabunge wote kufanya kazi kwa pamoja bila kujali vyama vyao ?,(Hence wapinzani kufanya kazi ya usaidizi wa Chama Tawala).

Je mbunge asiye na chama huweza kufanya kazi yake vyema kuliko mwenye Baggage ya Chama ?

Je tukipata wagombea binafsi bungeni ambao hawana vyama itachochea maendeleo ?,

Je (kama Katiba ikibadilika na kuruhusu) kuna uwezekano kwa Tanzania ya sasa mgombea binafsi bila back up ya Chama (gharama ya uchaguzi na support) kuweza kuchaguliwa na wananchi ?
 
Back
Top Bottom