Utafutaji wa Mafuta & Gesi na Vurugu chini ya mwamvuli wa DINI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utafutaji wa Mafuta & Gesi na Vurugu chini ya mwamvuli wa DINI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Uncle Jei Jei, Oct 25, 2012.

 1. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,200
  Likes Received: 942
  Trophy Points: 280
  Ni vema tukayatazama haya kwa jicho la tatu. Mungu aepushie mbali hapa kwetu Tanzania, lakini chokochoko zinazozidi kushamiri siku hadi siku (leo katibu wa Bakwata kajeruhiwa kwa bomu, vijana watatu wametekwa na kukatwa masikio Arusha na wanaosadikiwa kuwa WAISLAM, n.k) ni busara zaidi vyombo vya ulinzi na usalama vikapanua mipaka ya upelelezi wa nini chanzo chake nje ya mipaka ya Tanzania kwani nchi nyingi zilizogundulika kuwa na shehena ya mafuta zimeishia kwenye machafuko makubwa chini ya kivuli cha kutetea dini! Yaliyosemwa kuhusu kina FARID na uraia wa YEMEN si vyema yakapuuzwa isije kuwa rasilimali zetu ndo zinazogombaniwa na mahayawani wa nje kimyakimya wakisubiri tuvurugane sisi kwa sisi (tu wana wa Baba mmoja; ADAM) harafu waingie na vikosi vyao kwa visingizio vya kuleta amani huku wakisomba wanachokitaka! Watanzania, HASA WAISLAM NI VEMA TUKAYATAZAMA HAYA KWA JICHO LA TATU KULINDA UTULIVU TULIOKUWA NAO.
   
 2. Mogambi

  Mogambi Member

  #2
  Oct 25, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Ugomvi wa nzige ni furaha ya kunguru. Watanzania ni ndugu, tunafaham hili kwan wengi wetu pamoja na kuwa na dini tofauti ni ndugu wa damu. Je tuuane kwa utofauti huo? baba amuue mwanae kwa tofauti hiyo? Kama kweli tuna imani, tujiulize dini zetu zinatufundisha nini juu ya wenzetu, kama hazitufundishi kupendana,basi tujihoji kwa nini tuziishi hizo dini.
   
 3. L

  Luggy JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 2,113
  Likes Received: 629
  Trophy Points: 280
  kama hili ni kwa ajili ya Waisilamu ....katangazie msikitini
   
 4. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,200
  Likes Received: 942
  Trophy Points: 280
  hii inatuhusu sote mkuu, neno "HASA"nimelitumia kama kutahadharisha tu upande huo kwani wenzetu (sio wote!) imeonekana kumuamini kila anayeibuka na kudai anatetea Dini ya Islam bila hata kohoji uhalali wa anachokidai! Natumai ulisikia tamko la Wanazuoni wa Kiislam.
   
Loading...