Utafiti: Yawezekana maambukizi ya corona ni mengi kuliko inavyoripotiwa duniani kote

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279


BERLIN, UJERUMANI

WATAFITI katika Chuo Kikuu cha Göttingen nchini Ujerumani wametahadharisha kuwa huenda visa vya maambukizi ya virusi vya Corona duniani vimepindukia mamilioni kwa mamilioni.

Watafiti wanasema kufikia sasa ni asilimia 6% tu ya mambukizi hayo ambayo yamegundugulika.

Kulingana na utafiti huo, Christian Bommer na Sebastian Vollmer wa chuo kikuu cha Göttingen Ujerumani, wamechunguza data za gazeti la kila mwezi la Lancet ambalo hutoa taarifa kuhusu magonjwa ya kuambukizwa.

Kulingana na watafiti hao, data hizo zilionyesha kuwa huenda mataifa yamegundua tu asilimia 6% ya maambukizi hayo.

Wanasema idadi jumla ya virusi vya Corona huenda imependukia mamilioni kote duniani.

Wanasema kufikia sasa huenda virusi vya Corona vimeishawaambukizi mamilioni ya watu duniani.

“Matokeo haya yanamaanisha kuwa serikali zote na watungaji sheria wanapaswa kuwa makini sana wakati wakitoa idadi ya visa vya maambukizi ili waweze kurahisishwa katika kupanga mikakati ya kushughulikia visa hivyo. “Alisema Vollmer, profesa wa idara ya Maendeleao na Uchumi katika chuo hicho.

Utafiti huo unakadiria kuwa kufikia Machi 31, 2020, Ujerumani ilikuwa na visa vipatavyo 460,000 vya mambukizi ya virusi vya Corona.

Aidha unabainisha kuwa siku hiyo hiyo Marekani ilikuwa na zaidi ya milioni 10 ya maambukizi hayo, huku nchini Hispania wakikadiria kuwa tayari kulikuwa na watu milioni 5 wenye virusi hivyo.

Huko Italia, nchi ambayo sasa ni kiini cha virusi hivyo, watafiti wanasema ilikuwa na visa vipatavyo milioni 3 kufikia Machi 31 huku Uingereza ikiwa na maambukizi milioni 2.

Kwa mujibu wa data za chuo kikuu cha John Hopkins, iliripoti kutokea kwa visa 900,000 vya maambukizi kote duniani siku hiyo.

Watafiti Christian Bommer na Sebastian Vollmer wameeleza kuwa wakati data za chuo kikuu cha Johns Hopkins zikieleza kutokea kwa maambukizi chini ya milioni moja mnamo Machi 31, wanakadiria kuwa tayari kulikuwa na mamilioni ya maambukizi.

Kulingana na watafiti hao, uhaba wa vifaa vya kupima virusi vya Corona pamoja na kuchelewa kupima kumesababisha kutokea kwa vifo kadhaa katika mataifa ya Italia na Uhispania, tofauti na Ujerumani ambako visa viligunduliwa mapema.

Ujerumani imegundua takribani asilimia15% ya visa vyote ikilinganishwa na asilimia 3.5% na 1.7% ya visa ambavyo vimegundliwa Italia na Uhispania, utafiti huo umebaini.

Aidha unaeleza kuwa idadi ya visa vilivyogunduliwa nchini Marekani na Uingereza ilikuwa chini zaidi kwa asilimia 1.6% Marekani na huko Uingereza ikiwa tu kwa 1.2%

Utafiti huo umeeleza kuwa ni suala la muda tu, kubainika hali mbaya nyingine.

Utafiti huo umetoa wito kuyataka mataifa kuongeza juhudi za kupima na kugundua maambukizi mapya mapema na kuchukua mikakati ikiwemo kuwatenga waathirika.

“Ikiwa mataifa yatashindwa kufanyia hivyo, huenda virusi hivyo vikabaki bila kugunduliwa na kuweza kusababisha mripuko mwingine, ni suala la muda tu.” Watafiti hao wametahadharisha.
 
Hizo takwimu zako usijeukatoa za Tanzania maana kea mujibu wa Sheria hapa nyumbani takwimu zinaratibiwa na NBS ukijifanya mjuaji yanakupata ya yule Binti wa UDZM kule Mwadui Shinyanga, sasa hivi JF hatuchangii mtu hela kwa uzembe kama huo kumtoa Serro
 
Hizo takwimu zako usijeukatoa za Tanzania maana kea mujibu wa Sheria hapa nyumbani takwimu zinaratibiwa na NBS ukijifanya mjuaji yanakupata ya yule Binti wa UDZM kule Mwadui Shinyanga, sasa hivi JF hatuchangii mtu hela kwa uzembe kama huo kumtoa Serro
Acha uongo wewe Hiyo sheria imeshafanyiwa amendment Bungeni , watanzania akili hamna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo pasaka. Tumlilie Mungu tu ibilisi na corona hawana nafasi
 
Tumeamua kufa na tai shingoni kwani tukisema ukweli tutahitaji msaada. Bwana yule hapendi mashart anayopewa na wababe wa dunia.
Hivi kwanini afrika madhara au vifo vya corona idadi ni ndogo sana kuliko kwa wenzetu huko?
 
Kwa waliowahi kufanya research wanalijua hili. Kuna kitu inaitwa sample size. Huwezi ukakusanya data kutoka kwa population yote. Unachagua sample size ndogo tu plus kuna kupika data. Hivyo hilo linaweza kua kweli

Sent From Galaxy S9
 
Kwanini takwimu za ugonjwa wa corona zitolewe na chuo kikuu cha johnhopkins cha marekani na dunia nzima inaonekana kuridhia hali hii.
Hiki chuo kina mfumo gani wa kukusanya taarifa unaoaminiwa zaidi hata kuliko shirika LA afya duniani who wenye ofisi karibu kila nchi duniani.
Ni makubaliano yapi yakifanyika na lini ili kukiteua hiki chuo na kuacha vjngine vyote hata kile cha kwetu pendwa?
 
Nitandao ya kijamii inafanya corona kukua kubwa eh basi tuseme hivyo


It is never to late to begin. Start now
 
Back
Top Bottom