UTAFITI: Watu wenye uwezo wa kuona na kutafakari kwa haraka zaidi duniani hutokea Afrika.

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
download-1-4.jpg

Unaweza usiamini lakini kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na BBC, umetaja watu wenye uwezo wa kuona na kutafakari mambo kwa haraka zaidi duniani na Kabila la Himba kutokea Namibia limetajwa kama jamii yenye watu wenye uwezo mkubwa zaidi wa kuona na kukielewa kitu kwa haraka zaidi.

himbaboymom2-1.jpg


Utafiti huo ulionesha watu wa jamii ya kabila la Himba wana uwezo mkubwa wa kufocus na kuona vitu vidogo ambavyo ni vigumu kuonwa na watu wengine. Kutotumia teknolojia ya aina yoyote kwa watu hao kumetajwa kama sababu kubwa inayochangia watu wa jamii ya Himba kuwa na uwezo mkubwa wa kuona jambo kwa haraka.

p04vzj33.jpg


Kwa mujibu wa utafiti huo watu wa jamii ya Himba wana uwezo mkubwa wa kuona jambo na kulituma kwa haraka katika ubongo kuliko watu wengine wa kawaida, Ripoti hii ilionesha jinsi gani teknolojia kama simu, Tv na hata computer zinavyoathiri watu wengi na kuchangia kua na uzito na kutafakari mambo kwa haraka.
 
SASA MBONA WANAISHI MAISHA DUNI NAMNA HIYO?HIYO AKILI YAO KUBWA INAWASAIDIA NINI?
HATA WEMBE HAWAWEZI KUTENGENEZA
mjomba ayo ndo maisha yanayotakiwa ktk huu ulimwengu maana hata manabii hawakushindwa kuomba wakapewa usasa sababu walijua itakua ni changamoto kwa dunia yao .ila kwetu ndo ile mchimba kisima huingia mwenyewe.sayansi na technologia ni kaburi la maharibiko
 
mjomba ayo ndo maisha yanayotakiwa ktk huu ulimwengu maana hata manabii hawakushindwa kuomba wakapewa usasa sababu walijua itakua ni changamoto kwa dunia yao .ila kwetu ndo ile mchimba kisima huingia mwenyewe.sayansi na technologia ni kaburi la maharibiko
What a philosophical response!
 
SASA MBONA WANAISHI MAISHA DUNI NAMNA HIYO?HIYO AKILI YAO KUBWA INAWASAIDIA NINI?
HATA WEMBE HAWAWEZI KUTENGENEZA
duuuu wewe nae ni mtu wa ajabu aseeee,,, sasa vitu kama kiwembe,calculator na vingne vitakua na matumiz gani tena kwa hawa wanamibia sababu ishasemekana wana uwezo mkubwa wa kufikiria hivyo basi pia watakua wanayatawala mazingira yao bila hata vitu hivyo unavosemea kama kompyuta,simu,calculator na vingine,jaribu kufikirisha akili yako kidogo kuhusiana na mtu aliyekuja na idea ya kutengeneza microsoft,,je unafikiri huyu hana mbinu mbadala ya ku-operate hiyo microsoft bila hata kuiweka kwenye compyuta akati yeye ndio ana idea nzima,hao wanamibia kama ni very bright in such a way that they can solve some complex mathematical problems bila hata electronic device yoyote sasa watahitaji scientific calculator ya nini,, pia imagine mtu alikuja na idea ya four figure.
 
Back
Top Bottom