beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Utafiti wa kitalaam unaonyesha kwamba wananchi wengi wana matatizo ya kinywa na meno licha ya kuwa wenyewe hawajui.
Hayo yamebainishwa juzi na daktari bingwa wa upasuaji wa shingo, kichwa na meno kutoka Hospitali ya Rufani ya Kanda ya Bugando, Dk. Emmanuel Motega.
Dk. Motega alisema utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa asilimia kubwa ya wananchi wana matatizo ya kinywa na meno na kwamba wanaishi na matatizo hayo.
Sababu kubwa, kwa mujibu wa daktari bingwa huyo, ni kuwapo kwa uelewa mdogo juu ya magonjwa hayo huku akiwaomba wananchi wanapohisi maumivu ya meno, harufu mbaya ya kinywa, kuwahi hospitalini.
Alisema mtu akichelewa kupata matibabu, bakteria huingia sehemu zingine za mwili na kusababisha magonjwa mengine kama moyo, majipu ya kashuka kwenye shingo au kifuani, uvimbe na saratani.
"Kwa sasa huduma ya meno imeboreshwa kwa kiwango cha hali ya juu kwani tunaweza kutibu jino bila kung'oa. Tunaweza kuziba meno, kusafisha fizi ambazo zimepata magonjwa, kufanya upasuaji wa shingo na kichwa," alisema Dk. Motega.