Utafiti watilia shaka deni la Taifa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,565
21,562
mwakagenda-December3-2014.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Muungano wa Madeni na Maendeleo Tanzania (TCDD), Hebron Mwakagenda.

Licha ya kuwapo kwa taarifa kuwa deni la Taifa ni zaidi ya zaidi Sh. trilioni 30, tafiti zinaonyesha kuwapo kwa mashaka kuhusu taarifa hizo, kutokana na kukosekana kwa ofisi ya pamoja ya kusimamia deni na kuwapo kwa maafisa wasiothibitishwa kuiingizia serikali mikopo bila idhini ya Waziri.

Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2012 inaonyesha serikali kushindwa kuingiza mikopo katika deni la Taifa kiasi cha Sh trilioni mbili, na kulifanya deni la Taifa linalotolewa taarifa kutiliwa mashaka.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Muungano wa Madeni na Maendeleo Tanzania (TCDD), Hebron Mwakagenda, wakati akitoa taarifa kuhusu utafiti juu ya deni la Taifa uliofanyika Juni, mwaka huu.

Alisema kuwa taarifa ya CAG inaonyesha upo ukiukwaji wa sheria katika kukopa kwa taasisi za umma na kampuni binafsi inayodhaminiwa kukopa na kuvuka viwango vilivyowekwa kisheria.

"Upo uwezekano wa kuwapo kwa deni kubwa zaidi ya Sh. trilioni 30 kutokana na utoaji wa taarifa za mashaka na baadhi ya madeni yakawa si halali kwa kuwa hakuna uhalali na uidhinishwaji wa kutolewa mikopo," alisema Mwakagenda.

Aliongeza kuwa ipo mikopo ambayo haijatolewa taarifa na Msajili wa Hazina na mikopo hiyo kuhamishiwa kwa Serikali ni Air Tanzania Sh. bilioni 8.8, Mfuko wa Hifadhi wa Watumishi wa Umma (PSPF) bilioni 716, Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Sh. bilioni tatu.

Pia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) Sh. bilioni 75, Pensios Fund bilioni 1,250 na Shirika la Uchumi na Kilimo Tanzania (Sukita), Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), MCU kwa pamoja Sh. bilioni 254.

Aidha, ripoti ya utafiti huo ilipendekeza serikali kutunga sheria ya kuanzisha ofisi ya pamoja ya kusimamia deni, kusomesha wafanyakazi wa kusimamia ofisi hiyo, kuimarisha sheria ya mikopo, dhamana na misaada ya 1974 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2004.

Pia, ilipendekezwa kwamba serikali kutekeleza mapendekezo ya CAG, kufanyia ukaguzi wa deni na miradi pamoja na kuanzishwa kwa mjadala wa kitaifa kuhusu deni la Taifa na kuliweka wazi kwa wananchi.

Viongozi wa Wizara ya fedha jana hawakupatikana kuzungumzia matokeo ya utafiti huo. Waziri Saada Mkuya salum simu yake ilikuwa imezimwa. Naibu wake, Adam Malima, simu yake pia ilikuwa imefungwa wakati Naibu mwingine, Mwigulu Nchemba, simu yake ilikuwa ikiita bila majibu. Alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno hakujibu hadi tunakwenda mitamboni.

Chanzo: Nipashe

 
Mimi binafsi kidogo napata shida kuelewa kuhusu hili deni la taifa.

Naomba wenye kuelewa ufafanuzi.

Je, linatokana na nini hili deni??

Je, mfano hawa waliotajwa katika hii report ndio wanaoidai Serikali??

Je, ni bado SUKITA ipo hai. kwani hili ni Shirika ambalo lipo mikononi mwa CCM.


Msaada kwa wanaofahamu please.MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom