joseph1989
JF-Expert Member
- May 4, 2014
- 15,106
- 31,676
Kwa hiyo kukaa nae ina maana yeye na watoto wake tayari raia wa Tanzania?Ukioa mwanamke anabaki Kenya?
Pili mimi nimemjibu mtoa mada kutokana hizi statement.
"Jamii ya wakurya wanaokaa hapa wameanzisha utamaduni wa kuoa wanawake kutoka nchini Kenya ambao tayari wana watoto zaidi ya watatu na kuendelea
Yaani wanaume wa vijiji vya mpakani wanaenda Kenya wanachukua wanawake waliokwisha zaa huko Kenya na watoto wao na kuwahamishia upande wa Tanzania na hao watoto huhesabiwa kama watoto wa Mwita Chacha wa Tanzania na hupewa majina ya ukoo kwa upande wa Tanzania, watoto hawa wengine huwa wana umri mkubwa"
So mimi nimejibu kutokana na mfumo huu wa NIDA unavyofanya kazi,wenye unatengeneza connection ya vizazi na watu wote wa ukoo upande wa baba na wa mama.
Pili NIDA watataka kujua watoto wamezaliwa wapi,kwa maana ya mkoa wilaya na wao watafanya verification.Sasa hapo utadanganya wapi.