Utafiti Wangu: Watoto wengi hupenda zaidi ndugu upande wa mama kuliko upande wa baba

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania kulingana na utafiti wangu;

Kwanini katika familia nyingi watoto wengi hupenda zaidi ndugu wa upande wa mama kuliko wale wa upande wa baba zao?

Ni mara chache sana utaona mtoto wa baba mdogo na mkubwa wanasaidiana.

Mimi licha ya umri wangu huu mdogo lakini nimekuwa nikishirikishwa sana katika kutatua changamoto za kifamilia kwa jamaa na marafiki.

Kwa mfano unaweza kukuta mtu anakaa Dar lakini amepata safari ya kwenda kwenye interview ya kazi huko mkoani Iringa ambapo kuna ndugu wa pande zote mbili.

Kuna ndugu upande wa mama (mama mdogo) pamoja na ndugu upande wa baba (baba mdogo). Ila amini usiamini, asilimia 95% ya watoto watakuwa na furaha zaidi kwenda Iringa na kukaa nyumbani kwa mama mdogo kuliko kwa baba mdogo.

Watoto wa baba mdogo na baba mkubwa wengi wanakuwaga na beefs za hapa na pale tofauti kabisa na watoto wa mama mdogo na mama mkubwa.

Unaweza ukakuta watoto wa baba mdogo/mkubwa wanawweza kukaa hata miaka 2 bila hata kutumiama SMS ya kujuliana hali lakini watoto wa mama yake mkubwa ama mama mdogo wanawasiliana kila baada ya mwezi mmoja.

Nilijaribu kwenda mbali zaidi kutaka kujua chanzo ni nini kutokana na mahojiana na watu wengi wazima walionizidi umri.

Wengi walionipa majibu wanasema kwamba chanzo kikubwa ni kuwa akina mama wanapoolewa katika koo za watu wengine wao ndio wanakuwa chanzo cha kuleta kelele ndani ya koo walizoolewamo (bado sina uhakika na tetesi hii)

Kuna baadhi ya wataalam niliohojiana nao walipata kuniambia kwamba tafiti za kisaikoloji inaonesha kwamba mtoto ni rahisi sana kuamini maneno ya mama kuliko ya baba. Yaaani mama akikwambia kuwa yule mke wa baba yako mdogo amenitukana na kuanzia leo msiende kwao, na kweli watoto watatembelea mkoa huo lakini hawataenda nyumbani kwa baba yao mdogo/mkubwa tofauti kabisa akiambiwa na baba yake.

USHAURI KWA WABABA WENZANGU: Msikubali wanawake mliowaoa wavunje undugu wenu kwa maana nyie mmetoka mbali zaidi tangia mpo wadogo huko kwenu kuliko hao wake zenu mliokutana nao ukubwani.

Wanawake wengi hupenda zaidi kuwavuta watoto upande wa ndugu zao tu. Yaaani unakuta likizo mtoto anapelekwa kutembelea kwa mama zake au bibi mzaa mama tu baaaas, na hapa ndio mwanaume anapaswa kuwa kichwa ngumu na kusimama kama baba wa familia.

Kuna baadhi ya wababa huwa wanawachukua watoto wa nguvu na kuwapeleka upande wa ndugu zao pia ili wazoeleke na huko. Baadhi ya mwanaume legelege unakuta hata watoto wakizaliwa hata kama wapo 4 basi majina yote yanatokea ndugu upande wa mkewe.

NINAOMBA KUKOSOLEWA KATIKA UTAFITI HUU KAMA SIPO SAHIHI


1620204197797.png

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Mimi niko karibu sana ndugu zangu upande wa baba na si mama. Ila hata kwa baba watoto wa mashangazi ndio tuko nao karibu mno. Tunaweza ongea kwa simu hata masaa 2. Ila kimbembe kiko kwa watoto wa bamkubwa na mdogo hao huwa tunaonana siku ya matukio tu.
 
Hao wa upande wa mama ndiyo ndugu wa ukweli.sababu wa baba mdogo wanaweza wakawa sio watoto wake.

Ndiyo maana mtoto wa dada yako ni ndugu yako halisi ila mtoto wa kaka yako anaweza asiwe ni wa kwake.wanawake wanabeba siri nyingi sana.

hata wewe hao watoto wako wanaweza wasiwe wote ni wako.

Ila point yako inabakia kuwa validi tusaidieane tuu hata kama siyo ndugu
 
Hao wa upande wa mama ndiyo ndugu wa ukweli.sababu wa baba mdogo wanaweza wakawa sio watoto wake.
Mkuu, achana na suala la biology na DNA hiyo ni siri ya mama kwa maana hata nurses huwa wanabadili watoto siku hizi kwa kupewa pesa.

Wewe huyo unayemuita baba unajuaje kama ndio baba yako halisi wa DNA? Mbona bado unampenda?

Hapa hatujadili suala la DNA mkuu...
 
Ndiyo maana mtoto wa dada yako ni ndugu yako halisi ila mtoto wa kaka yako anaweza asiwe ni wa kwake.wanawake wanabeba siri nyingi sana.
Mtoto akizaliwa katika ndoa huyo ni mtoto wako mkuu. Vile vile hata huyo dada yako anaweza pia akabadilishiwa mtoto hospitalini kwa maana huyo mchezo ni mwingi sana kwa nurses hawa wa siku hizi...
 
Watoto watakuwa karibu na ndugu aliye karibu na familia (hasa mama)...inatokea wengi wanakuwa karibu na ndugu wa mama kwa sababu ndio hao wanawekwa karibu na mama. Nikiri tu wazi kwamba hata mimi nakuwa comfortable zaidi nikienda kwa dada kuliko nikienda kwa kaka
 
Back
Top Bottom