Kuziwa
JF-Expert Member
- May 23, 2011
- 248
- 212
Habari wadau,
Huu ni utafiti wangu binafsi. Wanaume wengi ambao wana wake wawili, mabinti zao nao hawaogopi kuwa katika mahusiano ya aina hiyo.
Hapa namaanisha kuwa, binti anaweza kuingia kwenye mahusiano na mume wa mtu akiwa anajua kabisa kuwa wewe ni mume wa mtu, na akakubaliana na hali hiyo. Ukichunguza kwa umakini utagundua kuwa, baba wa binti huyo ana wake wawili.
Kuna uhusiano mkubwa kati ya tabia za mtoto wa kike na tabia za baba yake; mfano ni huo, pia baba akiwa malaya na tabia hii ikajulikana kwa mtoto wako wa kike, basi wewe kama mzazi usianze kusema watoto siku hizi hawana adabu, madhara hayo umesababisha mwenyewe.
Tutafakari kwa pamoja. Karibuni!