UTAFITI WANGU: Utakachomsimulia mpenzi wako mwanzoni penzi lenu linapokuwa jipya ndio maneno atakayokurushia siku mtakapokwaruzana

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu Jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania, hivi mnajua ya kwamba;

Utakachokuwa unamsimulia sweetheart wako siku za mwanzoni penzi lenu linapokuwa jipya na moto moto ndio maneno hayo hayo atakayokurushia kama silaha siku ya kwanza mtakapogombana?

Nimefanya utafiti huu kwa kuwauliza baadhi ya marafiki na watu wengine randomly kwa muda wa wiki kama mbili hivi.

Ndugu yangu wewe pia yaliwahi kukukuta kwa sweetheart wako?

Mapenzi ni kitu cha ajabu sana kwa siku za mwanzoni. Hormones zinakuwa zipo juu and you find yourself deep in love kwa kiasi kwamba unajikuta upo free sana kusimulia udhaifu wako au wa ndugu zako wa karibu kama vile ulevi wa kaka yako, changamoto za ndoa ya dada yako au ubahili wa baba yako.

Mimi niliwahi kumsimulia sweetheart wangu wa zamani kuhusiana na tabia yangu ya uchoyo wakati nipo form 4 mwaka 2003. Zamani mimi nilikuwaga mchoyo sana wa vitu vyangu.

Hii haimaanishi kuwa hivi sasa sio mchoyo. hapana. Mimi bado nina elements za uchoyo uchoyo kwa mbaaaaali lakini nilipokuwa secondary nilikuwa mchoyo zaidi ya hivi sasa.

Niliwahi kumsimulia huyo dada my love jinsi nilivyoficha mishikaki ya nyama katika kabati langu la nguo ili tu ndugu zangu wasiniombe kwa kuwa siku ile pale home walikuwa wamepita ugali na mboga nisiyoipenda kabisa. Kwa bahati mbaya zaidi na mimi nikaja kusahau kama nilifinya nyama katika kabati la nguo na matokeo yake panya wakaja wakala zile nyama pamoja na nguo zangu nzuri.

Siku moja nikiwa nipo job mwaka juzi wa 2018 alinitumia SMS akiniomba pesa kiasi cha 70,000/= kwa ajili ya masuala kadhaa ya maandalizi ya sikukuu ya X-mas, na mimi kwa wakati ule nilikuwa ndio kwanza nimeanza kazi, mshahara wenyewe kidogo, basi ikabidi niwe mkweli tu nimwambie my love kwamba kwa sasa Soldier yupo vibaya sana financially.

Aisee yule dada si akaanza kuniporomoshea lawama kwamba mimi ni m-bahili na mchoyo na ikitokea nikamuoa basi ninaweza hata kumuua kwa njaa humo ndani kama ambavyo niliwafichia ndugu zangu nyama siku ile plus maneno mengine meeeeeengi si unajua tena hawa akina mama wanavyojua kuongea.

Ushauri wangu wa siku ya leo kwa vijana ni kwamba, unapoingia katika uhusiano kwa siku za mwanzoni jitahidi sana usimwambie sweetheart wako kila udhaifu wako au ule wa ndugu zako hata kama upo "deep in love" kwa kiasi gani na unapoachana na mpenzi wako kamwe usitangaze udhaifu wake uliopata kuujua pindi ukiwa katika uhusiano naye na hiyo itakufanya kuwa mwanamke/mwanaume wa kweli (a real gentleman).

Sio mtu ulikuwa katika uhusiano na mwanamke kisha ukagundua labda ana udhaifu wa ******** basi ikitokea mmeachana na wewe ndio unatumia udhaifu wake ule kama silaha ya kuanza kumtangaza kwa watu. Please don't do that. Man up brother.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Back
Top Bottom