Utafiti wangu: Ukweli na usichokijua kuhusu mauaji Mkuranga, Kibiti

MdengestanfromCuba

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
572
573
Kwa muda sasa kumekua na ukakasi na sintofahamu miongoni mwa watanzania juu ya haswa mauaju yanayoendelea kila leo huko Pwani maeneo ya Kibiti, Rufiji, Mkuranga, Ikwiriri nk. limekua si jambo geni sana kusikia watu wamepigwa risasi maeneo hayo, ila watu tumekuwa tukisubiri tu na kusikiliza leo nini kimejiri kule (naweza kusema taratibu tunaanza kuzoea hali hii).

Nirejee kwa kilichonifanya kuweka andiko hili, mara baada ya mauaji haya kushika kasi miezi ya hivi karibuni kumekuapo na taarifa nyingi, simulizi nyingi, ili mradi kila mtu anafunguka kile anachotizamia kua ni sababu au chanzo cha yanayoendelea huko, bila kupepesa macho mimi nilishindwa nimwamini nani juu ya hili maana wote wanaosimulia mfano hapa mtaani kwetu hawana uhakika saana ni ile hali ya kusikia tuu, sasa nikaona pia nijaribu kusikia chochote kutoka kwa wenyeji wa huko labda, nikaamua kufanya mazungumzo kidogo na rafiki yangu mmoja mwenyeji na mkazi wa Mkuranga ambaye nipo nae hapa kwenye taasisi yetu ndipo nikagundua mambo kadhaa, moja ni jambo ambalo limaekuja kushika kasi na kupata umaarufu baada ya kuwa na mizizi tayari, pili Wanamkuranga wenyewe wanazo taarifa nyingi juu ya hili, isipokua tu maharamia wale kwa sasa ni kama wameafunga midomo kwa vitisho.

Katika maongezi na rafiki yangu ni kwamba, inasemekana kuna kundi kubwa la vijana wenye misimamo fulani ya imani fulani likiongozwa na viongozi wao vinara (taarifa zinadai vyombo vya usalama wanayo majina yao vinawatafuta na wanafahamika), kundi hili lilianza vuguvugu miaka ya nyuma kidogo (inadaiwa kabla hata ya utawala wa Mkwere) ambapo walichukuliwa makundi kwa makundi na kupelekwa Somalia kupewa mafunzo ya kijeshi (kama sio kivita) kuvipa nguvu vikosi vya maharamia huko pembe ya Afrika (pale Mkuranga wanawafahamu baadhi ya watu walioenda huko) mwanzoni walikua wanapitia Kenya, lakini kwa sasa inasemekana mipaka upande wa Kenya imekua migumu, kwa hiyo wanazungukia upande wa DR Congo. Rafiki yangu akazidi kunielea kwamba kundi hilo la vijana mara baada ya kua wanarejea nchini walikua tayari wamepikwa kiitikadi na sasa walichokua wanaleta ni itikadi zao mpya ndani ya sehemu zao za kuabudia, inadaiwa kila sehemu waliyokua wakiingia waliwapa 'dawa' (kwa waislamu wanajua nini maana ya dawa) na kila msikiti walioingia palitokea mfarakano. Matokeo yake kukatokea kuanzishwa kwa misikiti mingine chini ya usimamizi wao na itikadi zao mpya hizo walizokuja nazo, taarifa zinadai kwamba walianza kuzunguka vijiji na vijiji ukanda wa pwani kusambaza 'dawa' na kujenga misikiti mingine chini ya itikadi zao (inadaiwa walianza kuungwa mkono na watu wenye uwezo) mpaka ilifikia hatua kuna misikiti ilijengwa hauruhusiwi kuingia kama hufahamiki ni nani.

mambo yote haya yalileta hali ya hamaki kwa wanachi kwa kile walichokua wakishuhudia, hali iliyopelekea wao kuanza kutoa taarifa kwa mamlaka juu ya hali ya mashaka kwani inasemekana kuna baadhi ya misikiti watu walionekana wakiwa na silaha za moto, huku kwingineko watu wakipewa mafunzo ya kimapigano, hii ilipelekea kukamatwa kwa viongozi kadhaa wa misikiti hiyo ambao ndio kwa sasa wanadaiwa kuwa manguli kwa yanayoendelea ukanda huo, watu hao wanafahamika sana Mkuranga, lakini hata hivyo waliachiwa kwa masharti kadhaa ikiwemo kuripoti kituoni kil baada ya muda fulani, lakini hata hivyo walitii masharti hayo kwa muda na baadaye wakatoweka kabisa na hapo ndipo mambo yalipoanza kidogo kidogo.

Baada ya kutoweka kwa muda kidogo ndipo yalipoanza kusikika matukio ambapo kuna lile la Stakishari ambapo wenyeji wanaeleza ni kundi hili lilifanya, na lile tukio la kuvamiwa NMB Mkuranga ambapo walipora kiasi cha zaidi ya milioni 200, ni baadhi ya matukio tu lakini yote inaonekana yalikuwa yakifanyika kwa misingi ya hawa watu kujiweka katika mazingira ya kujipanga. Kama mnakumbuka kipindi fulani zile taarifa za magaidi Tanga, sasa inadaiwa ni mlolongo huu huu isipokuwa ni kwamba kwa upande wa Tanga mamlaka ziliwahi kuzima harakati hizi mapema sana, kwa upande wa huku Mkuranga Jiografia ya haya maeneo imekua ni kama msaada mkubwa kwao, inadaiwa pia hata sasa wanakamatwa baadhi yao, huku wengine wakitoa vitisho kua wao wapo nchi nzima (rafiki yangu alijaribu kurejelea tukio lililowahi kutokea Mwanza watu waliochinjana msikitini).

Mwanzoni wananchi walitoa ushirikiano sana kwa vyombo vya dola lakini inadaiwa watu hawa baadhi wabaya ni miongoni mwa wanachi, sasa inshu ilikua ni ukitoa taarifa tu au ukitoa ushirikiano wowote kwa vyombo vya dola, usiku wanakufata. Mpaka ikafikia hatua wakawa na orodha ya viongozi kadhaa wa serikali za mitaa ambao walichukuliwa kama 'wanoko', unaambiwa kwa sasa Mkuranga au huko Kibiti watu wamefikia hatua wanaogopa hata kuongea na wanausalama hata kwa mambo ya kawaida tu, kwani ukionekana tuu, usiku unalo!

Kwa tetesi za waenyeji ni kwamba watu hawa hawafungamani kabisa na BAKWATA, ni kama wanataka kuleta itikadi zao mpya kabisa!! inadaiwa kuna mmoja aliwahi kukamatwa na kudai wao wanataka kuanzisha dola ya kiislamu!!

Rai yangu kwa serikali ni kuimarisha Intelijensia maeneo hayo na hata nchi nzima, kwani inaonekana kinachoendelea Kibiti kinaweza kutokea tena Mtwara, Lindi n.k japo hatuombei lakini ndio ukweli!!

Kwa mwenye taarifa zaidi au lolote nakaribisha michango tafadhali
 
Lakini hawa hawana sifa ya kupora pesa au Mali kama ulivyoeleza,wao wanafanya mauaji tu nakutokomea sanasana kuchukua siraha ikiwa wameua askari.
 
Ni suala LA muda tu ila hao wote watakamatwa tu, hatuwezi kuvumilia uvunjifu Wa amani kiasi kile, pia watu Wa maeneo hayo watoe ushirikiano kwa siri maana hayo maharamia baadhi watakuwa wanayajua , kwa nn uogope kutoa ushirikiano? Ukikaa kimy IPO siku watakuja kwako pia ni bora kushirikiana na serikali ili wakamatwe.
 
Kwa muda sasa kumekua na ukakasi na sintofahamu miongoni mwa watanzania juu ya haswa mauaju yanayoendelea kila leo huko Pwani maeneo ya Kibiti, Rufiji, Mkuranga, Ikwiriri nk. limekua si jambo geni sana kusikia watu wamepigwa risasi maeneo hayo, ila watu tumekuwa tukisubiri tu na kusikiliza leo nini kimejiri kule (naweza kusema taratibu tunaanza kuzoea hali hii).

Nirejee kwa kilichonifanya kuweka andiko hili, mara baada ya mauaji haya kushika kasi miezi ya hivi karibuni kumekuapo na taarifa nyingi, simulizi nyingi, ili mradi kila mtu anafunguka kile anachotizamia kua ni sababu au chanzo cha yanayoendelea huko, bila kupepesa macho mimi nilishindwa nimwamini nani juu ya hili maana wote wanaosimulia mfano hapa mtaani kwetu hawana uhakika saana ni ile hali ya kusikia tuu, sasa nikaona pia nijaribu kusikia chochote kutoka kwa wenyeji wa huko labda, nikaamua kufanya mazungumzo kidogo na rafiki yangu mmoja mwenyeji na mkazi wa Mkuranga ambaye nipo nae hapa kwenye taasisi yetu ndipo nikagundua mambo kadhaa, moja ni jambo ambalo limaekuja kushika kasi na kupata umaarufu baada ya kuwa na mizizi tayari, pili Wanamkuranga wenyewe wanazo taarifa nyingi juu ya hili, isipokua tu maharamia wale kwa sasa ni kama wameafunga midomo kwa vitisho.

Katika maongezi na rafiki yangu ni kwamba, inasemekana kuna kundi kubwa la vijana wenye misimamo fulani ya imani fulani likiongozwa na viongozi wao vinara (taarifa zinadai vyombo vya usalama wanayo majina yao vinawatafuta na wanafahamika), kundi hili lilianza vuguvugu miaka ya nyuma kidogo (inadaiwa kabla hata ya utawala wa Mkwere) ambapo walichukuliwa makundi kwa makundi na kupelekwa Somalia kupewa mafunzo ya kijeshi (kama sio kivita) kuvipa nguvu vikosi vya maharamia huko pembe ya Afrika (pale Mkuranga wanawafahamu baadhi ya watu walioenda huko) mwanzoni walikua wanapitia Kenya, lakini kwa sasa inasemekana mipaka upande wa Kenya imekua migumu, kwa hiyo wanazungukia upande wa DR Congo. Rafiki yangu akazidi kunielea kwamba kundi hilo la vijana mara baada ya kua wanarejea nchini walikua tayari wamepikwa kiitikadi na sasa walichokua wanaleta ni itikadi zao mpya ndani ya sehemu zao za kuabudia, inadaiwa kila sehemu waliyokua wakiingia waliwapa 'dawa' (kwa waislamu wanajua nini maana ya dawa) na kila msikiti walioingia palitokea mfarakano. Matokeo yake kukatokea kuanzishwa kwa misikiti mingine chini ya usimamizi wao na itikadi zao mpya hizo walizokuja nazo, taarifa zinadai kwamba walianza kuzunguka vijiji na vijiji ukanda wa pwani kusambaza 'dawa' na kujenga misikiti mingine chini ya itikadi zao (inadaiwa walianza kuungwa mkono na watu wenye uwezo) mpaka ilifikia hatua kuna misikiti ilijengwa hauruhusiwi kuingia kama hufahamiki ni nani.

mambo yote haya yalileta hali ya hamaki kwa wanachi kwa kile walichokua wakishuhudia, hali iliyopelekea wao kuanza kutoa taarifa kwa mamlaka juu ya hali ya mashaka kwani inasemekana kuna baadhi ya misikiti watu walionekana wakiwa na silaha za moto, huku kwingineko watu wakipewa mafunzo ya kimapigano, hii ilipelekea kukamatwa kwa viongozi kadhaa wa misikiti hiyo ambao ndio kwa sasa wanadaiwa kuwa manguli kwa yanayoendelea ukanda huo, watu hao wanafahamika sana Mkuranga, lakini hata hivyo waliachiwa kwa masharti kadhaa ikiwemo kuripoti kituoni kil baada ya muda fulani, lakini hata hivyo walitii masharti hayo kwa muda na baadaye wakatoweka kabisa na hapo ndipo mambo yalipoanza kidogo kidogo.

Baada ya kutoweka kwa muda kidogo ndipo yalipoanza kusikika matukio ambapo kuna lile la Stakishari ambapo wenyeji wanaeleza ni kundi hili lilifanya, na lile tukio la kuvamiwa NMB Kibiti ambapo walipora kiasi cha zaidi ya milioni 200, ni baadhi ya matukio tu lakini yote inaonekana yalikuwa yakifanyika kwa misingi ya hawa watu kujiweka katika mazingira ya kujipanga. Kama mnakumbuka kipindi fulani zile taarifa za magaidi Tanga, sasa inadaiwa ni mlolongo huu huu isipokuwa ni kwamba kwa upande wa Tanga mamlaka ziliwahi kuzima harakati hizi mapema sana, kwa upande wa huku Mkuranga Jiografia ya haya maeneo imekua ni kama msaada mkubwa kwao, inadaiwa pia hata sasa wanakamatwa baadhi yao, huku wengine wakitoa vitisho kua wao wapo nchi nzima (rafiki yangu alijaribu kurejelea tukio lililowahi kutokea Mwanza watu waliochinjana msikitini).

Mwanzoni wananchi walitoa ushirikiano sana kwa vyombo vya dola lakini inadaiwa watu hawa baadhi wabaya ni miongoni mwa wanachi, sasa inshu ilikua ni ukitoa taarifa tu au ukitoa ushirikiano wowote kwa vyombo vya dola, usiku wanakufata. Mpaka ikafikia hatua wakawa na orodha ya viongozi kadhaa wa serikali za mitaa ambao walichukuliwa kama 'wanoko', unaambiwa kwa sasa Mkuranga au huko Kibiti watu wamefikia hatua wanaogopa hata kuongea na wanausalama hata kwa mambo ya kawaida tu, kwani ukionekana tuu, usiku unalo!

Kwa tetesi za waenyeji ni kwamba watu hawa hawafungamani kabisa na BAKWATA, ni kama wanataka kuleta itikadi zao mpya kabisa!! inadaiwa kuna mmoja aliwahi kukamatwa na kudai wao wanataka kuanzisha dola ya kiislamu!!

Rai yangu kwa serikali ni kuimarisha Intelijensia maeneo hayo na hata nchi nzima, kwani inaonekana kinachoendelea Kibiti kinaweza kutokea tena Mtwara, Lindi n.k japo hatuombei lakini ndio ukweli!!

Kwa mwenye taarifa zaidi au lolote nakaribisha michango tafadhali
Nakupongeza.lkn jiandae kw matusi.ulichokisema ni kweli kbs.
 
Kama kuna ukweli katika habari yako basi hili ni zaidi ya tatizo mkuu.Kama serikali wana macho nadhani unaweza kuwa msaada mkubwa kwao.Pamoja san mkuu
 
Unakaribisha michango! wee ni nani? inaonekana kama kuna vitu vingi unavijua, ila Majaliwa alisema mauaji ya Kibiti hayana uhusianano na Uislamu hivyo usihusishe hayo mambo na dini, kumbuka hata hawa Sunni hawapo Bakwata hata sherehe ya Idd walisherehekea kivyao.
 
Yeah ni kweli, lakini huu ni ukweli nilioupata kutoka kwa wenyeji
 
Back
Top Bottom