UTAFITI WANGU: Kwanini wanafunzi wengi (jinsia zote) wenye maendeleo mabaya shuleni huwa ni watu wa kujituma sana katika shughuli ngumu za nyumbani?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
8,243
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Sio kila siku tunapaswa kuandika, kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya kizungu kama Cold War, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad. Leo ngoja tujadili kidogo masuala ya kimaisha katika jamii zetu hizi tunamoishi.

Ndugu zangu Watanzania eti

Kwanini wanafunzi wengi (jinsia zote) wenye maendeleo mabaya shuleni huwa ni watu wa kujituma sana katika shughuli ngumu za nyumbani?

Sisemi kwamba kufanya kazi za nyumbani ndio kunawafanya wasiweke mkazo zaidi katika masomo, hapana, unakuta baadhi ya nyumba zimeajiri mpaka dada wa kazi lakini mtoto wa kike shule imemshinda ila katika kazi za nyumbano haumwambii kitu unaweza ukasema yeye ndiye ameajiriwa kama dada wa kazi lakini hapana pale ni kwao.

Yaani hakumbushwi majukumu yake. Mtoto wa kike unakutaa saa kumi na moja ameamka mwenyewe na anaanza kupiga deki, anafagia uwanja, anateka maji.

Sasa kwa upande wa pili wa shilingi kwa wale wenzangu na mie ambao ndio intelligent darasani, ambao ndio Tanzania Ones yeye masomo mengi anapata tu A, A, A, A, A, katika kazi za nyumbani wapo zero kabisa. Unakuta weekends kuamka saa 3 asubuhi, hajui kupika, hajui kuosha viombo vikatakata, hajui kudeki.

Je, hii ina uhusiano wowote na issue za Introversion pamoja na Extroversion Psychology?

WATAALAM WA SAIKOLOJIA ZA WATOTO NA WANAFUNZI MNAWEZA MKATOA UFAFANUZI ZAIDI JUU YA HILI.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
6,982
2,000
Ndipo nguvu na uwezo wao ulipo, kwenye kazi za mikono (manual labor). Pia wanaweza kuwa ni watu ambao ni practical zaidi kuliko nadharia. Usiwapuuze hao ndio mafundi vyuma, waashi, wajenzi, na kazi nyingine za suluba ambazo wengi hawaziwezi.
 

Mao ze dong

JF-Expert Member
Aug 28, 2012
666
500
Sikubaliani nawewe maana mimi nilikua kinara mzuri tu darasani na nyumbani narudi napiga kazi kinoma . Malezi tu ila akili ni swala la ki genetics zaidi . Kufanya kazi ni swala la kimalezi zaidi na muundo wa familia .
 

Ndekrepha

JF-Expert Member
Jun 4, 2020
1,495
2,000
Kila mtu anapenda complement, hivyo atatafuta eneo ambalo yuko vizuri zaidi ili aweze kupata hoyo complement.
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
8,243
2,000
Sasa kama umeshajulikana kuwa ni 'Mpumbavu' uwapo Shuleni ( Kitaaluma ) kwanini usijitahidi tu uwe 'Mwerevu' kwa Kuwajibika sana Nyumbani?
Sio kwamba ninakuwa nimeshajijua bali ndio nilivyozaliwa. Kila nikijitahidi ku-balance ninashindwa.

Wanafunzi bright sana shuleni ni wavivu wakubwa wa kazi za nyumbani.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,727
2,000
Utafiti wako hauko sahihi makabila ambayo watu hujituma sasa majumbani ndio huwa na ufaulu mzuri mfano wachaga,watu wa Mara.,Kagera,wasukuma , wanyakyusa na wamasai na wabena
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,727
2,000
Sikubaliani nawewe maana mimi nilikua kinara mzuri tu darasani na nyumbani narudi napiga kazi kinoma . Malezi tu ila akili ni swala la ki genetics zaidi . Kufanya kazi ni swala la kimalezi zaidi na muundo wa familia .
Kuna connection kubwa sana kati ya uchapakazu na akili za darasani pia ndio maana nchi ziliziendelea zina uchapakazi mkubwa na ndio pia wanaongoza kwa uwezo kielimu
 

Cybergates

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
404
1,000
hii kitu ni kweli, ili uishi nyumbani na wazazi wa kupende lazima ume na kimoja kati ya Nidham na kujituman au akili hasa za darasani, ukiamua wewe uwe mtukutu, hujitumi hakikisha darasani unafaulu, kufaulu kutakulinda ukiwa nyumbani, ukiwa na akili kujituma kwako ni option unaweza ukahamka saa 4 unaskia wanalalamika chini chini alafu inaisha, Balaa linakuja pale darasani unafeli alufu alafu unaendekeza utukutu na ukaidi, kama wewe sio mtoto wa kishua ukimaliza la saba unaenda kijijini na ka wewe ni wakishua ukifika la 5 unaenda boding
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom