Utafiti wangu juu ya mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,296
33,079
UTAFITI:

JINSI YA KUMTAMBUA NI MWANAMKE YUPI WA MTANDAONI KAKUPENDA KWELI NA YUPI TAPELI:

(a) MWANAMKE WA MTANDAONI TAPELI

Ukitaka kujua huyu ni mwanamke tapeli mtandaoni na jinsi ya kutambua hupendwi bali unaliwa tu, ukiona hizi dalili, chomoa mapema:

i) Siku ya kwanza tu ya kuanza kuwasiliana nae, atachat nawe text nne ama tano, ya sita atakwambia sms zinakaribia kukata hivyo utume vocha anunue kifurushi muendelee kuchat, usipofanya hivyo hutaona text yake tena(ila kiukweli sms bado anazo)

ii) Siku hiyohiyo unapoanza kuwasiliana naye, jioni yake utashangaa unaambiwa anajisikia njaa, hivyo utume 5000 Tigo Pesa akatoe anunue chakula ale (ila kiukweli hata hana njaa)

iii) Siku ya pili ama nne baada ya kuwasiliana nawe, utashangaa mwenzio kaanza kuumwa jino, kichwa ama homa ghafla, hivyo atataka umtumie hela akang'oe jino ama akanunue dawa, usipofanya hivyo utablockiwa kwa kisingizio kuwa ni mwanaume ambae humjali(ila kiukweli hata haumwi)

iv) Hata kama wiki iliopita ilikuwa ni Birthday yake, akiwa anadate nawe, utashangaa anakwambia keshokutwa itakuwa birthday yake, lengo umtumie hela ya zawadi ya Birthday, usipofanya hivyo wewe hujali, utakula block ya maana

v) Kama yuko mbali nawe, ataanza kujidekeza na akikazania kuwa anataka asafiri aje hadi mkoa uliko ili akuone aenjoy nawe, lengo utume hela ambayo yeye anaita 'hela ya nauri', ukilogwa ukafanya hivyo bro umekwenda na maji, hutaona mtu akisafiri, na akiona unamsumbua kumpigia sana utashangaa WhatsApp block, Facebook block na Messenger block.

(b) MWANAMKE WA MTANDAONI AMBAE KWELI KAKUPENDA:

i) Utafiti uonesha kuwa, mwanamke akiwa amemzimikia na kumpenda kiukweliukweli mwanamme fulani mtandaoni, huwa hamuombi hela hatakama ana shida kiasi gani hasa anapokuwa hajamzoea. Hatakama akimzoea, bado atakuwa kimya akiamini mpenziwe anajua mahitaji yake, atajiongeza na kumsaidia penye shida.

ii) Mwanamke aliekupenda, yu radhi kumuomba hela ya vocha mwanaume mwingine ambae hata hampendi; wao huita "buzi la kuchuna" kisha akatumia hiyo vocha kuwasiliana na mwanaume wake anayempenda.

iii) Akiwa yuko vizuri kiuchumi, mwanamke ana moyo wa kipekee sana, anaweza kuwa anakusapraiz hata kwa zawadi mbalimbali, si kwamba anakuhonga, bali anajaribu kuexpress hisia zake kwako hata kwa kidogo alichonacho.

iv) Ukitoa wazo la kusafiri aje mkutane, hataharakisha kukwambia umtumie nauri, wengi wao hupambana akapata ya kuja kisha ya kurudia ndo aweza kuomba msaada umsaidie, lengo ni kwamba akujengee imani zaidi na kukutoa hofu usije ukadhani labda utatumia hela asije. Hivyo mwanamke atakuwa radhi atumie hata nauri yake mwenyewe na akaja hadi ulipo.

Kiukweli kiasili si kwamba wanawake wanapenda pesa, bali wanawake wana mapenzi ya dhati, ni waaminifu na wema. Labda ukutane tu na yule ambae hajakupenda ndo utachunwa hadi basi, ila ukikutana na mwanamke wa mtandaoni ambae kakupenda kiukweliukweli, utaenjoy, kwani asili yao ni uaminifu.
 
Sasa mkuu kama wewe najua kabisa unamihela ..why nisikupige vizinga?

But pole mkuu
Kuna njia za kumpiga mzinga mtu unaye tarajia kuwa na uhusiano nae kimapenzi sio mtu anakutongoza na hapo hapo unampiga mizinga? Si utamrusha huyo buzi lako kumchuna?
 
Sasa huyo unaetongoza si ndie mwisho wa siku mkikubaliana mnakua kwenye mahusiano ..toa tu pesa ustawishe uhusiano mkuu.
kuan njia za kumpiga mzinga mtu unaye tarajia kuwa na uhusiano w akimapenzi sio mtu anakutongoza na hapo hapo unapiga mizinga? si utamrusha huyo buzi lako kumchuna?
 
Back
Top Bottom