UTAFITI;Wanawake wengi wanachukia utawala huu kuliko wanaume

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
19,996
49,104
Utafiti uliofanywa na taasisi moja ( sio twaweza) unaonyesha kuwa wanawake walio wengi wanachuki na utawala huu kuliko wanaume,hii inatokana na wanawake wengi kuwa tegemezi kwa wanaume ambao asilimia kubwa ndio watafutaji,baada ya mirija kubanwa maumivu yamekuwa zaidi kwa wanawake ,kwani kuna wale waliokuwa wamejengewa,kupangishiwa nyumba,kufunguliwa miradi,kununuliwa magari pamoja na kusomeshwa aither wao wenyewe au watoto na ndugu sasa huduma hizo zimepungua au kukatika kwa kasi,kila mwanaume anaangalia familia yake kwanza,inavyoonekana namba ya Mzilankende imesomwa zaidi na wanawake,kwani wanaume walisha zoea kula kwa jasho
toa maoni yako kuhusu utafiti huu
 
Wanaume ndio wanaoongoza kuichukia ccm kwani wao ndio watafutaji wakuu

Wanawake huwa wanajisahau sana haswaa kipindi cha kampeni
 
Mpaka kuisoma mwanamke wanaume tumeshaisoma vilivyo kwao yamefika mawimbi tu lkn dhoruba lote he he he... sisemi:D
 
Kwa wapenda mabadiliko ni nafasi murua kabisa kwani mama zetu na dada zetu ndio walikuwa wanakwamisha safari ya mabadiiko kisa kanga za ccm walisha zoea kuletewa kuhongwa so ulipokuwa wakiambiwa maisha magumu hawaelewi
 
Naona hypothesis zako kichwani ndo una generalise kama research findings..
mpaka niseme utafiti wa twaweza ndio utaamini haya utafiti huu ni kwa mujibu wa.......
upload_2017-1-7_12-31-58.jpeg
 
Honestly wanawake wengi ndio wanakuwaga hopeless zaidi kipindi cha uchaguzi.
Wanarubuniwa kirahisi mno.
Let them suffer..
I like it.
 
Mimi sijui juu ya huo utafiti wako;ila nilichokutana nacho naweza kusema kinarandana na andiko lako.

Juzi nimekutana na wanawake sehemu tunapata mambo yetu;kati yao watano wanakiri kuwa kwa miaka 6 mfululizo hawakuwahi kulipa kodi ya pango inayotokana na kipato chao,yaani hela zao za mfukoni.Miaka yote kodi zilikuwa zinagawanywa kwa "madanga".

Danga hili anaomba laki,huku anaomba laki mbili na nusu,haku laki tatu mpaka kodi ya mwaka inakamilika na analipa.Sasa safari hii kwa mara ya kwanza wao ndio wametoa kodi ya pango,na hela imewauma sana;na kwa kweli zile tabia za kupanga "upande mzima" wa nyumba zimewaishia;wanabaki kusema tu "Aaaa mimi chumba na sebule,jiko na choo vinanitosha,dada wa kazi atalala sebureni"

Na kwa kweli walimalizia na kauli ya "Huyu baba hatari,kabana mpaka danga ukilipigia simu halipokei,iwe kwa namba yako au namba mpya"
 
Utafiti uliofanywa na taasisi moja ( sio twaweza) unaonyesha kuwa wanawake walio wengi wanachuki na utawala huu kuliko wanaume,hii inatokana na wanawake wengi kuwa tegemezi kwa wanaume ambao asilimia kubwa ndio watafutaji,baada ya mirija kubanwa maumivu yamekuwa zaidi kwa wanawake ,kwani kuna wale waliokuwa wamejengewa,kupangishiwa nyumba,kufunguliwa miradi,kununuliwa magari pamoja na kusomeshwa aither wao wenyewe au watoto na ndugu sasa huduma hizo zimepungua au kukatika kwa kasi,kila mwanaume anaangalia familia yake kwanza,inavyoonekana namba ya Mzilankende imesomwa zaidi na wanawake,kwani wanaume walisha zoea kula kwa jasho
toa maoni yako kuhusu utafiti huu
Khanga na yale madela ya kijani njano si tulisaidiana kuvaa. Watulize mchecheto 2020 watapozwa na zingine tena kutakuwa na mitandio pia.
 
Hebu fikiri gari inapita ikiwa na ule wimbo wa 'wacha waisome namba eeee, CCM mbele kwa mbeleeee'. Unafikiri nini kitatokea kama mawe yapo jirani?
 
Back
Top Bottom