Utafiti: Wanawake wa Afrika wanazidi kuwa wafupi

Ehud

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
2,685
337
Matokeo ya utafiti yaliyotolewa mwezi April mwaka huu yanaonyesha kuwa kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita wanawake barani Afrika wamekuwa wakizidi kuwa wafupi.

Katika utafiti ulioitwa "Heights of Nations" uliofanywa na Profesa SV Subramanian wa Chuo cha Afya ya Jamii cha Harvard, imeonekana kuwa wanawake wanaozaliwa Afrika katika kipindi cha miongo miwili iliyopita ni wafupi wakilinganishwa na mama na bibi zao waliozaliwa baada ya Vita ya Pili ya Dunia.

Mchumi John Komlos amesema kuzidi kupungua kwa urefu wa wanawake wa Afrika kunahatarisha ustawi wa kizaji kijacho.

Komlo ameongeza kuwa urefu wa mtu mzima ni kipimo cha ubora wa maisha, kiwango cha baiolojia ya maisha na muda wa kuishi, hivyo urefu unapodumaa kuongezeka au unapoanza kupungua miongoni mwa vizazi ni ishara kuwa mambo yanakwenda kombo.

Profesa Subramanian na timu yake walichunguza urefu kwa wanawake 364,538 wenye umri wa miaka 24 hadi 49 katika mataifa 54 yenye kipato cha chini na cha kati.

Kati ya nchi hizo 54, nchi 14 zilikuwa na wanawake wanaopungua urefu,nchi 21 hazikuwa na mabadiliko na nchi 19 zilikuwa na wanawake wanaoongezeka urefu.

Nchi zote 14 zilizokuwa na wanawake wanaopungua urefu ni za bara la Afrika.

Utafiti huo umeonyesha miongoni mwa nchi za Afrika ni Kenya Na Senegal tu ndizo zilizoonyesha wanawake kuongezeka urefu.

Kenya umekuwa nchi bora barani ya Afrika na imeshika namba 9 miongoni mwa nchi zote 54, ambapo imeonekana wanawake waliozaliwa Kenya miaka 1980's ni warefu kwa takriba 1.95cm kuliko waliozaliwa miaka ya 1950's.

Urefu kwa wanawake umedumaa katika nchi 15 za Afrika zikiwemo Uganda, Congo Brazzaville, Lesotho, Zimbabwe, Swaziland, Togo, Ethiopia, Zimbabwe, Cameroon, Burkina Faso, Guinea, Tanzania, Ghana, Gabon na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Uganda imeshika nafasi ya 16 kwa kufanya vibaya katika urefu wa wanawake kati ya nchi zote 54 huku Tanzania ikiwa ya 26.

Urefu wa wanawake umekuwa ukipungua katika nchi za Rwanda, Zambia, Comoros, Madagascar, Jamhiri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Msumbiji, Nigeria, Chad, Namibia, Benin, Liberia, Mali, Niger na Malawi huku umekuwa ukiongezeka katika nchi za Nepal, India na Bangladesh.

Rwanda imeonesha urefu kupungua kwa 4.2cm kati ya wanawake waliozaliwa miaka ya 1950's na wale waliozaliwa katika miaka ya 1970-80s.

Source: Mohammed Dewji Blog
 
Utafiti wa huyo msomi nadhani unamapungufu kidogo. Yaani atakuwa amelenga moja kwa moja kama ambavyo mimi naweza nikafanya utafiti katika nchi za ulaya na kuleta repot kuwa. Marekani inaongoza kwa wazungu kuwa na black eyes wakati waingereza wanaongoza kuwa na macho ya blue.
 
Labda inasababishwa na uchafuzi wa mazingira, lakini kwanini Wanawake wa Afrika tu na siyo wa dunia yote au wake kwa waume!?
 
Kwanza ni vigumu saana kucritise research ya watu juu juu bila kusoma content na sampling. Mfano, mtu akija Tanzania, kuna jamii ya watu kama wasukuma ni warefu saana lakini jamii nyingine ni kawaida na wengine ni wafupi km wabena hata wakinga. Kwahiyo tungesoma na kujua alifanyaje kwenye sampling yake hata kwa Tanzania huenda ingetusaidia.
Lakini pia ni lazima tufaham, lishe ni muhim saana katika ukuaji. Unaweza ukaangalia mtoto anayeishi Ulaya wa miaka 14 na yule wa Africa hata wakiwa race moja, utaona wa kule anaonekana mkubwa kwa maana ya Urefu. Kwahiyi pia chakula kina sehemu yake na kwa tafisri nyepesi ni kwamba tumezidi kuwa masikini zaidi kuliko miaka ya nyuma.
 
Haihitaji utafiti kujua hilo. Tembelea shule za jangwani zanaki na kisutu halafu linganisha na miaka ya 80
 
Huu utafiti ulifanywa kwa kufuata mfuatano wa vizazi? (Generations)
Isijekuwa utafiti wa mwanzo ulifaywa kwa wamasai halafu uliofuatia ukaenda kufanywa kwa Wangoni, hapo lazima wataona tofauti...
Kwa uzoefu wangu ni kuwa tunaongezeka urefu, hebu jiangalie urefu wako halafu jilinganishe na wazazi au mababu na mabibi zako kisha uone kama umewazidi, ina maana unaongezeka, kama wamekuzidi basi urefu umepungua.. Kisha tuje na tathmini zetu na sisi tena kwa kuzingatia vizazi vilivyotutangulia...

Kwa mfano mimi nimemzidi Urefu mzazi wangu (baba), naye amemzidi urefu mzazi wake (babu)...
Dada yangu amemzidi urefu mzazi wangu (mama), mama amelingana urefu na mzazi wake (bibi)...

Sijashawishika kukubaliana na huu utafiti...
 
wengi wa watu wa Japan ni wafupi lakini ndio wanaishi mda mrefu. NINA DOUBT NA HUO UTAFITI WAO

Matokeo ya utafiti yaliyotolewa mwezi April mwaka huu yanaonyesha kuwa kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita wanawake barani Afrika wamekuwa wakizidi kuwa wafupi.

Katika utafiti ulioitwa "Heights of Nations" uliofanywa na Profesa SV Subramanian wa Chuo cha Afya ya Jamii cha Harvard, imeonekana kuwa wanawake wanaozaliwa Afrika katika kipindi cha miongo miwili iliyopita ni wafupi wakilinganishwa na mama na bibi zao waliozaliwa baada ya Vita ya Pili ya Dunia.

Mchumi John Komlos amesema kuzidi kupungua kwa urefu wa wanawake wa Afrika kunahatarisha ustawi wa kizaji kijacho.

Komlo ameongeza kuwa urefu wa mtu mzima ni kipimo cha ubora wa maisha, kiwango cha baiolojia ya maisha na muda wa kuishi, hivyo urefu unapodumaa kuongezeka au unapoanza kupungua miongoni mwa vizazi ni ishara kuwa mambo yanakwenda kombo.

Profesa Subramanian na timu yake walichunguza urefu kwa wanawake 364,538 wenye umri wa miaka 24 hadi 49 katika mataifa 54 yenye kipato cha chini na cha kati.

Kati ya nchi hizo 54, nchi 14 zilikuwa na wanawake wanaopungua urefu,nchi 21 hazikuwa na mabadiliko na nchi 19 zilikuwa na wanawake wanaoongezeka urefu.

Nchi zote 14 zilizokuwa na wanawake wanaopungua urefu ni za bara la Afrika.

Utafiti huo umeonyesha miongoni mwa nchi za Afrika ni Kenya Na Senegal tu ndizo zilizoonyesha wanawake kuongezeka urefu.

Kenya umekuwa nchi bora barani ya Afrika na imeshika namba 9 miongoni mwa nchi zote 54, ambapo imeonekana wanawake waliozaliwa Kenya miaka 1980's ni warefu kwa takriba 1.95cm kuliko waliozaliwa miaka ya 1950's.

Urefu kwa wanawake umedumaa katika nchi 15 za Afrika zikiwemo Uganda, Congo Brazzaville, Lesotho, Zimbabwe, Swaziland, Togo, Ethiopia, Zimbabwe, Cameroon, Burkina Faso, Guinea, Tanzania, Ghana, Gabon na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Uganda imeshika nafasi ya 16 kwa kufanya vibaya katika urefu wa wanawake kati ya nchi zote 54 huku Tanzania ikiwa ya 26.

Urefu wa wanawake umekuwa ukipungua katika nchi za Rwanda, Zambia, Comoros, Madagascar, Jamhiri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Msumbiji, Nigeria, Chad, Namibia, Benin, Liberia, Mali, Niger na Malawi huku umekuwa ukiongezeka katika nchi za Nepal, India na Bangladesh.

Rwanda imeonesha urefu kupungua kwa 4.2cm kati ya wanawake waliozaliwa miaka ya 1950's na wale waliozaliwa katika miaka ya 1970-80s.

Source: Mohammed Dewji Blog
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom