Utafiti wabaini: Wanawake wafupi hatarini kwa vifo vya uzazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utafiti wabaini: Wanawake wafupi hatarini kwa vifo vya uzazi

Discussion in 'JF Doctor' started by Michael Amon, Jul 28, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Jul 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  SIKU zote mwanamke awapo mjamzito huwa na matarajio makubwa ya kukipata kiumbe chake ambacho huwa ni faraja ya pekee maishani mwake.

  Lakini inapotokea mwanamke huyo akashindwa kukipakata kiumbe alichokisubiri kwa hamu kwa muda mrefu wa miezi tisa, huwa ni msiba … majuto na upweke wa aina yake.

  Hiyo ndiyo hali iwakumbayo wanawake wengi wanaopoteza watoto wao wakati wakujifungua .
  Zipo sababu chekwa zisababishazo vifo vya watoto wachanga na moja ya sababu hizo ni maumbile ya wanawake wenyewe.

  Wengine si tu hupoteza vichanga bali hata maisha yao wenyewe huenda yakawekwa rehani katika kipindi hiki.

  Kwa mujibu wa Hadija Kimwaga, Ofisa Muuguzi na Mkunga kutoka Hospitali ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, wanawake wafupi wako katika hatari ya kupata matatizo wakati wa kujifungua ingawaje si kila mwanamke wa aina hiyo kwani wapo wengine ambao hujifungua kwa njia ya kawaida.

  "Baadhi ya wanawake walio na urefu ulio chini ya sentimita 150 huwa na nyonga ndogo. Hivyo, inashauriwa mara watakapokuwa na ujauzito kwenda kwanye vituo vikubwa vya afya ama hospitali kubwa kwani huko wanaweza kupata huduma sahihi", anaeleza.

  Anaongeza kuwa na hii ni miongoni mwa sababu zinazowafanya wataalamu wa afya kuwashauri kufika kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya mtoto na afya zao kwa ujumla katika kipindi hicho.

  Kwa wale wanaopata tatizo mara nyingi njia pekee ya kuwanusuru imekuwa ni upasuaji. Hivyo, ikithibitika kuwa nyonga za mwanamke husika hazitanuki kwa kiwango kinachohitajika basi huduma hiyo hutolewa kwa lengo la kunusuru maisha ya mama na mtoto.Lakini hatari kubwa hutokea pale wanapocheleweshwa anasisitiza.

  Pamoja na kuwa suala la kimo mara nyingi hutegemea na hali ya kijenetiki, wakati mwingine ufupi husababishwa na ukosefu wa lishe bora wakati wa utotoni.

  Dk. Hassan Saad kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids)anasema kimo kifupi mara nyingi husababisha matatizo wakati wa kujifungua kutokana tatizo la kushindwa kutanuka kwa nyonga
  Anasema tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa mara nyingi lishe duni wakati wa utotoni hupelekea kudumaa. Jambo linalochangia hupelekea mtoto husika kuwa mfupi.

  Baadhi ya mambo yanayochangia hali hiyo ni ukosefu wa vitamini D na ukosefu wa mwanga wa jua wa kutosha unaosababisha kupata matege na magonjwa mengine ya mifupa ikiwamo hilo la kutokuongezeka kwa nyonga.

  "Lishe bora ina nafasi kubwa ya kuongeza kimo na pia kuongeza kimo cha mji wa uzazi" alisema.
  Imebainishwa kuwa wanawake walio katika tatizo hili kwa sasa, huwa wameathiriwa wakiwa wadogo.

  Dk Maggie Blott, mshauri wa masuala yanayohusu magonjwa ya wanawake, kutoka Uingereza ameandika kwenye mtandao wake kuwa baadhi ya wanawake walio na kimo kifupi wana nyonga ndogo, ambazo hushindwa kushindwa kutanuka wakati wa kujifungua na hivyo kusababisha madaktari kuchukua uamuzi wa kuwafanyia upasuaji .

  "Mara nyingi ili kuokoa maisha ya mama na mtoto, tumekuwa tukitumia njia ya upasuaji", anaandika daktari huyo.
  " Katika nchi zinazoendelea umasikini na ukosefu wa lishe bora kwa watoto unasababisha watoto hao kukua , wakati mifupa ya wasichana inakuwa haijakomaa. Hali hii ya kudumaa husababisha matatizo wakati wa kujifungua na pia fistula", anasisitiza.

  Tatizo hili limekuwa ni la kawaida kwa nchi masikini na hasa kwa wanawake na wasichana walio na hali ya chini kimaisha.

  Vifo vya wajawazito mara nyingi vinasababishwa na matatizo wakati wa kujifungua na vimekuwa vikiongezeka zaidi katika nchi zinazoendelea hasa kutokana na huduma duni za afya zinazotolewa hususani na wakunga jadi.
  Wakati mwingine mzazi hupoteza damu nyingi sana kabla ya kujifungua, kutokana na mtoto kukandamiza njia ya uzazi na kusababisha majeraha yanayosababisha kuvuja kwa damu. Jambo linalosababisha mwanamke husika kufanyiwa upasuaji.

  Ulaji wa chakula bora tangu kipindi cha mimba na baada ya kuzaliwa, ni njia mojawapo ya kuepuka tatizo hili.
  Kwani ikiwa mama atakula chakula bora wakati wa ujauzito, ni wazi kuwa atajifungua mtoto mwenye afya bora.
  Mtoto huyo pia akipata chakula bora wakati wa makuzi yake, ni wazi kuwa atakuwa katika hali bora kiafya. Hali hiyo huchangia kuondoa udumavu, unaopelekea hatari wakati wa kujifungua.

  Lakini, kwa wanawake kama Magreth Mwenda hawana jinsi ya kurekebisha maumbile yao, isipokuwa ni kuhakikisha wanajifungua sehemu salama yenye madaktari wenye ujuzi wa kutosha.

  Pia, kuwapa chakula bora watoto wao pindi watakapojifungua ili kuwaepusha na tatizo kama hilo.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #3
  Jul 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Kwa [h=2](Utafiti wabaini: Wanawake wafupi hatarini kwa vifo vya uzazi) kwa thread yako uliyoweka sisi wenye wanawake wafupi kuna hatari ya kwa vifo vya uzazi tuwe waangalifu asante kwa ujumbe wako ninakupa hongera kwa hiyo thread yako Mkuu Young_Master[/h]
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Its a long time fact, mwanamke mwenye urefu chini ya cm 150 ana uwezekano mkubwa wa kujifungua kwa operation. Sasa inaongelewa kana kwamba imegundulika sasa. Muwe mnachagua wachumba warefu,lol
   
 6. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #6
  Jul 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Tukichagua warefu wafupi wataolewa na nani?
   
 7. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #7
  Jul 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu MziziMkavu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Tuwe tuna mix mbegu. Kama ww mrefu,uchague mfupi Kama funguo ya starlet.
  sio wewe mfupi Kama opener unachagua mfupi Kama spana namba 8
  :loco:
   
 9. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #9
  Jul 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Sasa si ndio mambo ya kizungu hayo? Wewe umeona wapi mzungu akiona mwanamke mrefu kuliko yeye?
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Kama wewe ni Mrefu ninahisi mkuu King'asti
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  huu ni uweli kabisa kwamba wanawake wafupi wanahatari ya kufariki wakati wa kujifungua. ila sasa inabidi kama wanataka kuepusha vifo basi wawe wanazaa kwa upasuaji lakini wasijaribu kuzaa kwa kawaida.
   
 12. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Sasa Ina maana wanaume wafupi waoe mbilikimo? Ndo mixing nnayoongelea hapa, Kama ww mfupi usijivunge, oa mrefuuu ili wanao wasikulaumu
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Hehehe, mie mrefu Kama nyundo boss wangu.
   
 14. Rapunzel

  Rapunzel JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,089
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mungu ndiye muweza wa yote kwenye suala la kujifungua, na kwa wanawake wafupi wanatakiwa wachkue tahadhari mapema na wapate ushauri wa daktari ili wajue njia gani mnzuri ya kujifungulia, maana kuna warefu wengne na nyonga zao pia huwa hazitanuki, au njia ndogo so ina depends na mwili wa mtu
   
 15. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #15
  Jul 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Sasa kama nikioa mrefu King'asti kwenye maswala ya kukisiana barabarani inakuwaje? Si ndio mambo ya kuanza kutembea na stuli njiani ili kila mara ntakapohitaji kumkiss niwe napanda kwenye stuli.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  U can't get everything u want every time sugar boy! Didn't ur mom teach u that?
  Anakuwa havai 6-inches heels na unajifunza kusimamia vidole gumba
   
 17. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #17
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  wajapan ni wafupi lakini huyasikii haya.

  wapare ni wafupi lakini mambo swaafi.

  All in all nakushukuru kutoa elimu kwa umma.
   
 18. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #18
  Jul 29, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Taabu kweli kweli.
   
 19. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #19
  Jul 29, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hivi tafiti ni kweli? Au ni imagination za kisayansi tu? Nimeona wakina mama wafupi wamejifungua salama, na sometimes warefu hawakufanikiwa.
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  Jul 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ma mbili kimo si ndo watakuwa hatarini kabisa?
   
Loading...