Hizb Tahrir Tanzania
JF-Expert Member
- Feb 18, 2020
- 258
- 235
UTAFITI WABAINI UPOTOFU MADAI YA UGAIDI TANZANIA. NI ULE WA MTAFITI PETER BOFIN
Na Bakari Mwakangwale
Utafiti umeonyesha kuwa chokochoko zote katika suala la ugaidi, hazina na hazionyeshi uhalisia kuwa Waislamu ndani ya Tanzania wanahusika.
Hayo yamesemwa na Bw. Peter Bofin (Mu-Irish) ambaye ni mtafiti wa masuala ya ugaidi katika nchi za Tanzania, Kenya na Msumbiji ambaye pia amefanikiwa kufika kwenye maeneo yote yaliyodaiwa kutokea ugaidi katika nchi hizo.
Bw. Bofin ameyabainisha hayo Julai 2, 2020 akiongea na Mtafiti nguli wa Historia ya Tanganyika (Tanzania) Mzee Mohammed Said, alipomtembelea nyumbani kwake Magomeni Jijini Dar es Saalam.
Mzee Said amesema, alifanya mazungumzo mengi na Bw. Bofin, lakini maongezi yao zaidi yalitawaliwa na historia ya Waislamu na masuala ya ugaidi nchini Tanzania.
Mzee Said, alisema Bw. Bofin, amemfahamisha kwamba ameishi Tanzania kwa miaka 15 na kwamba utafiti wake umeonesha kuwa chokochoko zote alizokutana nazo katika suala la ugaidi, hazina chanzo kutoka kwa Waislamu ndani ya Tanzania.
Mzee Said, alisema katika maongezi yao alimueleza Mtafiti huyo kuwa Wazee wa Kiislamu walipigania haki yao ya kuwa huru kutoka kwa Mkoloni chini ya TANU na hawakunyanyua silaha, bali waliwaunganisha wananchi wote bila ya kujali dini na kabila zao kuondoa dhulma ili haki na usawa vipatikane kwa wote.
Hapo ndipo utaona kuwa hawakumbagua Mwl. Julius Nyerere kwa Ukristo wake na walimchagua kuwa kiongozi wao, wakati Nyerere akija na kuanza siasa Dar es Salaam katika mji wa Waislamu.”
“Nikamweleza huo ndiyo msimamo wa Waislamu wengi wa Tanzania na ikiwa haki itaonekana inatendeka kwa wote, itakuwa vigumu kwa mbegu ya ugaidi kumea katika ardhi ya Tanzania. Amesema Mzee Said, akinukuu maongezi yake na Bw. Bofin.
Aidha, Mzee Said, alisema katika maongezi yao kwa pamoja walirejea Historia ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), ambapo alimfahamisha kuwa katika kudumisha amani ni muhimu kwa Serikali kusikiliza nini Waislamu walio nje ya BAKWATA, wanasema.
Mazungumzo yetu yote tulifanya kwa Kiswahili, kwani Bw. Bofin, anakifahamu vizuri, tuombe dua kuwa taarifa yake popote inapokwenda iakisi fikra nilizomweleza na isaidie katika kutafuta haki kwa nia ya kudumisha amani katika nchi yetu. Amesema Mzee Said.
Awali Mzee Said, alisema Bw. Bofin, amemueleza kuwa amesoma kila alichoandika kuhusu Waislamu Tanzania, amesoma utafiti aliofanya katika madai ya ugaidi na mauaji yaliyo tokea Jijini Tanga katika miji ya Kilindi na Handeni 2013, pia amesoma paper aliyowasilisha Chuo Kikuu cha Ibadan, Nigeria 2006 kuhusu ugaidi.
Mzee Said, alisema Bw. Bofin, amemueleza kuwa kajulishwa kwake na Prof. James Brennan wa Chuo Kikuu Cha Illinois, Urbana Champaign Marekani, ambae yeye (Mzee Said) ni rafiki yake kwa miaka mingi, ambaye pia (Prof. Brennan) ni mtaalamu wa Historia ya Tanzania, aliyeandika vitabu na paper kadhaa kuhusu Tanzania.
(Gazeti la Anuur)
Maoni:
Ikiwa hiyo ndio hali ya dhulma kwa Waislamu tuendeleeni kupaza sauti kutetea mahabusu kadiri inavyowezekana..
Hashtags
#KomeshaUkandamizajiWaKisheriaNaUtekaji (Swahili)
#StopOppressiveLawsAndAbduction (English)
hizb or.tz