Utafiti wa Tanzania Daima juu ya Dk Slaa wapondwa

Status
Not open for further replies.

GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,320
1,195
Jana katika gazeti la Tanzania Daima , ukurasa wa mbele kabisa kulikuwa na kichwa cha habari ' Dk Slaa kinara wa urais 2015'. Habari hii, ilionyesha utafiti ambao ulifanywa na Jamii Forum.
Katika hali kushangaza, utafiti huu umeonyesha waliochangia mawazo yao hawazidi hata watu 1,500 kati ya watanzania takriban zaidi ya million 45. (hii ni sawa na asilimia 0.0033).
Utafiti huu umepondwa kwa sababu zifuatazo
1. Idadi ya uwakilishi wa walio ulizwa ni ndogo mno mno mno sana, kiasi cha kwamba huwezi kujumuisha mawazo ya watu ambao hata asilimia 1 haijafika , ukasema matokeo yako ni sahihi
2. Imekuwa ikitanabahishwa kuwa JF ni mtandao wa CDM, na imedhihiri hivyo. Sasa kwa mintarafu hiyo, huwezi ukafanya utafiti kwenye mtandao wako na wewe mwenyewe unaumiliki na watu wakauamini . Ile dhana ya uwazi inakosekana kwa maana hiyo.
Kwa sababu hizo pamoja na nyingineo ambazo zinatakiwa ili utafiti uwe bora, hazikupatikana kwenye utafiti huu. Kwa hivyo basi, twaweza sema ni utafiti wakukurupuka na wakimagumashi.
 

MpangoA

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
362
0
Poor criticism..Kwani REDET (ya Banna) wanavyofanya utafiti huwa wanahoji watanzania wote? Kwa taarifa tu hata REDET sample yao huwa ni 1,500-2,000.
 

POMPO

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
6,690
1,195
Mbona kichwa cha habari na maudhui ni tofauti?..."wapondwa" na kina nani?

Sishangai maana hata ID yako JF inatofautiana sana na post zako...
kwanza rudi darasani ama Google ujue
What is a research
What is a sampling
 

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,825
0
Tatizo ninanoliona kwa sample ya JF ni kwamba haikatazi watu wenye ID zaidi ya moja kupiga kura zaidi ya mara moja.


*Tanabahi
Watu 1,500 walitakiwa walinganishwe na idadi kamili ya wapiga kura wa Tanzania na sio jumla ya Watanzania wote kwani watoto wa changa, wanaotambaa, wanaosimama dede na wengineo hadi kufikia umri wa miaka 18 maoni yao hayatambuliki kisheria.
 

Joseph

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
3,521
1,225
Inakwaza nii kukubaliana na utafiti ambao umetoka JF?Kama kuna mtandao mwingine ambao unaweza kufanya utafiti ufanye na tupewe kama wafanyavyo watafiti wengine.Sikubaliani na mawazo ya kuwa JF inawakilishwa na CDM,kama ndivyo inashindikana vipi kwa wana CCM kuingia katika mtandao huu na kufanya kile ambacho CDM wanafanya?Maana kujiunga huulizwi unatokea chama gani.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom