Utafiti wa RAI: CCM kushinda Arumeru kwa asilimia 61% | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utafiti wa RAI: CCM kushinda Arumeru kwa asilimia 61%

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Mar 8, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  WanaJF
  Gazeti la RAI linalomilikiwa na kampuni ya Habari Cooperation limeubuka na kile kinachodai ni kura ya maoni ya nani atachaguliwa kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki
  Katika kile wanachodai ni utafiti wao katika kata 17 ni kwamba mgombea wa CCM Siyoi Sumari anatarajiwa kupata ushindi mkubwa wa asilimia 61% huku mgombea wa CDM Joshua Nassari akitarajiwa kuambulia asilimia 38.5%. RAI wanadai Siyoi Sumari anaungwa mkono na makundi yote ya wananchi jimboni humo na pia ndiye anaonekana kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi

  My take:Nadhani ufike wakati vyombo vya habari viache propaganda chafu kwa ajili ya kukatisha wananchi tamaa.Bado hatujasahau gazeti hilihili lilitoa tathmini kama hii wakati wa uchaguzi mdogo jimbo la Igunga ambapo walidai katika utafiti wao mgombea wa CCM angepata ushindi wa asilimia 70%.Lakini nadhani wote tunayajua matokeo ya Igunga yalivyokuwa.Pia tafiti za kipropaganda kama hizi zimekuwa zikitumiwa na maafisa wa tume ya uchaguzi wasio waaminifu kuchakachua matokeo.
   
 2. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  huyu atakuwa bashe tu
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hizi CCM-Lowassa bana na tafiti za KI-FISADI!!! Anyway what was your sample map and size on what you now call 'Research' if at all you know them.
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  jina la sioi limetangazwa wiki iliyo pita na vipi huo utafiti umefanyika lini? na walitumia muda gani kukusanya hizo takwimu zao?

  Hawa jamaa igunga walikuwa against mgombea wa CCM ila huku kwa sababu mgombea amependekezwa na mmoja wa mabosi wao wameona ni bora waanze propaganda mapema,
   
 5. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hutakiwi kushangaa kwa sababu CEO wa Habari corp anajulikana ni Husen Bashe (Al-Shabaab). Huyu bwana alikuwa bega kwa bega na SIOI wakati wa kura za marudio Arumeru kuhakikisha kuwa sioi anapitishwa. Unategemea baada ya kazi kubwa aliyoifanya kule leo hii gazeti lake lije liseme ukweli kuwa Nasary atashinda?? haiwezekani lazima amridhishe mshkaji wake pamoja na wakubwa zake akina EL na RA. Lakini ukweli utaiumbua Rai na Bashe tar 2 mwezi ujao wakati matokeo yatakapotangazwa kinyume cha ubashiri wao
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mbona wametangaza kuwa mgombea wa ccm kwenye uraisi 2015 atashinda kwa 95% sababu ccm inakubalika zaidi nchini, na imefanya makuu kwenye sekta za afya, umeme, maji na miundombinu ya usafilishaji!
   
 7. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndiye!
  Yeye si mkurugenzi?
   
 8. M

  Molemo JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu huoni pia kwamba ni maandalizi ya kuchakachua kura?
   
 9. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  CCM na CHADEMA ni sawa na Yanga na PAN. hata siku moja PAN hamcheki Yanga kufungwa na SIMBA! wewe angalia tuu suala la katiba jinsi CDMA walivyoisaliti nchi na umma wa kitanzania. na mpaka leo hakieleweki kitendawili cha katiba. hivyo wao wataamu tuu nani achukue huku aruumeru mashariki.
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo uwezo wako wa kufikiri ulipoishia.
   
 11. p

  panadol JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM itashinda kwa kuwa wananchi wa Tanzania wanakubaliana na sera zake na mfumo wake wa kiutawala vyama vingine havieleweki watu wanaamini ni vyama kwa ajili ya viongozi kujinufahisha wao wenyewe tumeona kwa NCCR-MAGEUZI,CUF na bado tutaona kwa wengine haiwezekani chama kikawa na viongozi hao hao toka kimeanzishwa kana kwamba hamna watu wengine wenye uwezo wa kuongoza ukichunguza na kufuatlia vizuri utajua kwamba hivi ni vyama vya watu fulani wao,marafiki zao na koo zao vimeanzishwa kwa masilahi ya watu binafsi na wala si kwa masilahi ya taifa sasa hivi watanzania wameshtuka wanaona bora waichague CCM kuliko upinzani,jimbo la Arumeru Mashariki CCM itashinda kwa kuwa wananchi wana imani nayo sana!
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hapana, hii ni kzi ya Esther Bulaya a.k.a Ritz.

  Kula TANO Mkuu, ukiona Wameru wameshindwa kukupa raha kama vile tunavyofahamu on the ground kule Arusha basi uamuzi uliobora zaidi ni mtu KUJIPA RAHA MWENYEWE tu ka hivi ulivyofanya kwa kupitia ile ID yako yaa kutokea.

  Kudos Ritz!!!
   
 13. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Hao jamaa mafisadi tu
   
 14. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  propaganda zao za kijinga zinafanya lisiuzike ka kofia ya polisi
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Jamani Rai ni gazeti huru lina haki kufanya tafiti zake na kuandika wanachokiamini kama wanavyofanya Tanzania Daima.

  Nakumbuka hata kwenye uchaguzi wa Igunga RAI walifanya tafiti zao wakasema CCM itashinda na kweli wakashinda.

  Muanzisha huu uzi unatakiwa uwe mvumilivu sio upende kuona Chadema inasifiwa na kila mtu.

  Humu JF kumekuwepo na tafiti za Chadema kushinda Kigamboni, Chadema kushinda Arumeru, Wameru wanamtaka Nassari kuwa mbunge wao.

  Sababu za kuifanya CCM kuanguka Arumeru, kwenye tafiti zote hizo ulikuwa mstari wa mbele kuchangia na kukubaliana na tafiti hizo.

  Leo Gazeti la Rai wanatoa utafiti wao unalia lia.
   
 16. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45

  Kutokana na katiba ya nchi yetu, kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake.
  Mimi kwa sasa nipo Arumeru, naomba mtu mweye majina ya hizo kata atuwekee hapa na atueleze huo utafiti ulifanyika lini, na ni vigezo/maswali gani yalitumika.
  Nipo tayari kufanya follow up ya jambo hili kwani siamini kabisa yanayosemwa.
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,798
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu kama hicho. ccm na fisi sawasawa, kila anapokatiza lazima azomewe.
   
 18. M

  Molemo JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Vipi mkuu wangu tujiandae tena na propaganda ya Udini kama ilivyokuwa Igunga na Uzini?
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Pokea kwa mikono miwili Utafiti wa Rai, mkuu.
   
 20. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  duh.. unaposema watanzania wanakubaliana na sera na mifumo yake unamaanisha wananchi gani..? walimu ambao hawajalipwa mishahara na mafao yao..? madaktari ambao wako katika mgomo wa kupigania maslahi yao..? wakulima ambao japo wanatumia nguvu zao kulima na kutoa mavuno wanakutana na vizingiti kibao na mwisho kuambulia kiduchu kwenye mazao yao..? wanafunzi ambao wanatumia muda wao mwingi kufuatilia mikopo badala ya kuwa darasani na kupata elimu..? wananchi maskini wanaoporwa ardhi yao kwa kicingizio cha kupewa wawekezaji..? au labda wananchi wasio na hatia wanavyouawa na polisi na hakuna anaewajibika..? wananchi ambao mfumuko wa bei umewaathiri..? wafanya biashara ambao uzalishaji umeshuka kwa kukosa umeme wa uhakika..? Hebu nisaidie mkuu inawezekana tunazungumzia nchi mbili tofauti hapa..
   
Loading...