Utafiti wa Polisi-Ukatili wa Kiuchumi dhidi ya Wanaume Umeongezeka,hawana Kauli kwa mali/kipato Chao

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,589
14,135
Nawasalimu kwa salamu ya Taifa...Kazi inaendelea..

Kwa mujibu wa utafiti wa Polisi,ukatili wa kiuchumi dhidi ya wanaume umezidi kuongezeka na kuwafanya kuwa watumwa kwenye ndoa..

Sisi wanaume tunashukuru Sana Polisi kwa kulibaini hili,ifike mahala sasa kule kwenye madawati yenu ya kijinsia mtutendee.sawa na muweke na wanaume pale sio askari wa kike tuu ambao huegemea upande wa wanawake pindi kesi za mahusiano ya ndoa zikiletwa.

Hii dhana ya kuwaaminisha wanaume kwamba wao ndio wanatakiwa kutafuta pesa na kwamba pesa ya mwanaume ni ya wote na ya mwanamke ni ya kwake ikomeshwe mara moja maana zinawaathiri wanaume kisaikolojia kiasi kwamba mtu anajiuliza naoa kuwa mtumwa au vipi?

Pili tunaomba sheria ya ndoa inayohusu masuala ya mali iangaliwe upya,haiingii akilini nitafute pesa kwa jasho kubwa afu mwanamke amekaa tuu anakusimanga afu mwisho wa siku anazingua eti na mali mnagawana pasu kwa pasu,hii haiko sawa..

Hawa wanawake wamekuwa wakitelekeza wanaume wakati wa Umri mkubwa na mbaya zaidi wao huwafitini watoto nao wanakutelekeza licha ya jasho na damu uliyotumia kwa ajili yao..

Tunaomba Wizara ya mambo ya ndani Kwa kushirikiana na wizara ya ustawi wa jamii mpeleke sheria Bungeni Ili kubadili vifungu hivyo katili na kandamizi kwa wanaume..

Mali utafute wewe ila usiwe na kauli nayo kwa kisingizio cha kijinga eti ndoa sijui watoto na upuuzi kama huo.👇

Screenshot_20220511-202453.png
 
Yaani mwanamke aninyang’anye pesa?na card ya bank!?inawezekanaje hii au ni mimi sijamuelewa kamanda Suleiman?
 
Wamekuja na Kodi ya mezani kila siku mwanaume anaacha mke anapeleka kwenye mchezo mwishowe mwanaume anakonda na kupungukiwa hisia za mapenzi huku mama akinenepa na kutangaza mme wake kwamba hana nguvu kumbe mawazo ya kodi ya mezani.
 
Harafu na matusi juu,hiyo ya kwenye kikoba sio yako na wakisema ya familia ujue wewe mwanaume sio sehemu ya familia..

Aisee inakera Sana.
 
Wamekuja na Kodi ya mezani kila siku mwanaume anaacha mke anapeleka kwenye mchezo mwishowe mwanaume anakonda na kupungukiwa hisia za mapenzi huku mama akinenepa na kutangaza mme wake kwamba hana nguvu kumbe mawazo ya kodi ya mezani.
This is serious,Wanaume wa Kigoma nao walalamika kunyanyaswa na Wanawake 👇

Screenshot_20220517-092215.png
 
Back
Top Bottom