Utafiti wa Kisiasa Kuhusu Maziwa ya Mama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utafiti wa Kisiasa Kuhusu Maziwa ya Mama

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Dec 23, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Utafiti wa Kisiasa

  Maulamaa, watafiti na madaktari wa ulimwengu mzima wamekongamana kwa kauli moja kwamba maziwa ya mama ndio chakula bora kabisa kwa watoto wachanga. Chakula ambacho huwapa siha (afya njema) na kuwapa kinga dhidi ya maradhi mbalimbali. Maziwa ya mama ni johari kwa maisha yote ya vichanga hivi. Imeonekana kwa jamii ya wanyama wanyonyeshao (mammals), hali kadhalika kwa binadamu kwamba maziwa yao wenyewe ndio chakula bora na chenye kuwafaa watoto wao wachanga. Kwa mfano maziwa ya ng’ombe ni chakula bora kifaacho kwa ndama wake, kwa sababu wao (ndama) wanahitaji kukua haraka kimaumbile ili waweze kuitumia miguu yao minne kwa ajili ya kujitafutia riziki na maisha yao. Ukuaji wao wa kiakili si muhimu sana kwao kama ule wa kimwili. Lakini kwa upande wa binadamu, watoto wachanga hawahitaji kiasi kikubwa hicho cha nguvu za mwili ambacho kinahitajiwa na jamii ya wanyama wanyonyeshao. Kwa sababu wao (watoto wachanga) hawatakiwi kutembea na kujitafutia riziki yao wao wenyewe kama ilivyo kwa watoto wa wanyama. Kinyume chake, watoto wachanga wa binadamu kwanza huhitaji maendeleo ya haraka ya vitivo vyao vya akili na mfumo wa mishipa ya neva. Ili kuwawezesha kusaga chakula vema, kulala, kuhisi, kuelewa na kuzungumza kwa kawaida. Kwa kiasi cha kutosha kabisa, maziwa ya mama hukidhi mahitaji haya ya kichanga kwa njia-maumbile. Hii ndio sababu, watoto wanao nyonyeshwa maziwa ya ng’ombe, kwa kawaida husumbuliwa na matatizo ya kutokupata choo (constipation) au kuhara. Maziwa ya mama yana mafuta (fats) 4% wakati ambapo maziwa ya samaki aina ya “seal” (mammal-fish) yana mafuta 40% zaidi ukiyalinganisha na yale ya mwanadamu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba samaki mchanga huyu “seal” mara tu baada ya kuzaliwa huhitaji utando wa mafuta (layer of fat) karibu ya ngozi yake ili kumuwezesha kuishi ndani ya maji barafu.

  Na kwa upande mwingine, kiasi cha juu kabisa cha protein kinapatikana kwenye maziwa ya sungura, ni mara kumi zaidi ya kile kilichomo ndani ya maziwa ya binadamu. Ni kwa ajili hii, ndio vichanga vya sungura hukua haraka zaidi, uzito wao huwa mara mbili zaidi ya uzito wa siku walipo zaliwa ndani ya kipindi cha siku sita tu tangu kuzaliwa. Wakati ambapo kichanga cha binadamu kwa kawaida huhitaji miezi sita kuwa na uzito maradufu ya ule wa siku ya kuzaliwa. Hizo ndizo sheria za maumbile, ni kitu cha kushangaza kuwa leo hata watoto wachanga wanasumbuliwa na maradhi ya moyo! Lakini watoto wanao nyonyeshwa vema na mama zao, huwa salama dhidi ya maradhi kama hayo.

  Kuacha kuwanyonyesha watoto na maradhi ya moyo:

  Kwa mujibu wa utafiti wa kisasa katika nyanja ya sayansi tiba, imegundulika kwamba maradhi ya shinikizo la juu la damu hukita mizizi yake wakati wa kipindi cha uchanga. Moja ya sababu kuu za msingi zinazo sababisha hali hii ni kiasi kikubwa cha madini aina ya “sodium” kinacho patikana ndani ya maziwa ya ng’ombe. Kwa kipindi cha miaka 25 iliyo pita karibu nusu ya akina mama wa Kiamerika waliwanyonyesha watoto wao maziwa ya ng’ombe (kopo) badala ya yale yao wenyewe. Katika jiji la Uingereza ni asilimia thelathini na sita tu ya akina mama ndio wanao wanyonyesha watoto wao. Ndani ya kipindi cha miaka mitano tu asilimia khamsini na moja ya watoto wachanga wamenyima haki ya kunyonya maziwa ya mama zao. Takwimu hizi zinatosha kabisa kufichua sababu inayo pelekea kuongeza kwa maradhi ya moyo siku hata siku katika nchi hizi na zile zote zinazo jiita nchi zilizo staarabika na kuendelea za Kimagharibi. Kwa kweli asili/maumbile yameyafanya maziwa ya mama kuwa ndio chakula bora kabisa na kifaacho kwa afya ya mwili na akili ya watoto wachanga.

  Mbali na umuhimu wa kimaumbile wa kuwanyonyesha watoto, natija/athari zake za “Psychological” pia zinakita kina na ni zenye manufaa mno kwa vichanga. Mtoto anayenyonya maziwa ya mama yake akiwa amepakatwa mapajani mwake, si tu hupata lishe bora, bali pia hujihisi salama na mwenye amani. Hisia hizi za usalama na amani humfanya mtoto katika mustabali wake kuwa mwanamke au mwanamume mwenye utu wa kawaida ulio lingana sawa. Mtoto kukosa hisia hizi zisizo hitajia gharama katika kuzipata, humuwekea na kumjengea misingi ya masumbuko ya utu na watoto kama hao kwa kawaida huwa wagonjwa wa akili. Ambao huishia kwenye hospitali za magonjwa ya akili au kuwa waharifu wadogo na baadae kuwa majambazi yasiyo na chembe ya huruma.

  Wataalamu : “Psychologists, “Psychiatrists na “Sociologists” ulimwenguni kote wana fikra kwamba ongezeko la kasi katika mienendo ya kitabia na maradhi ya akili. Kimsingi husababishwa na watoto kukosa upendo, kujaliwa na huruma kutoka kwa wazazi wao. Wazazi wa leo, khususan akina mama walio zama katika shughuli za kiuchumi, hawana muda wa kutosha kuwafanya watoto wao kuhisi kuwa wako salama kupitia upendo wao (wazazi), kujaliwa na kuonewa huruma nao. Kwa ajili hii basi, watoto hawa huwa waasi na kusheheni fikra za chuki na visasi kwa wazazi wao hawa wasio na muda wa kuwaonyesha upendo. Kwa upande mwingine, dhamira ya akina mama hao huwasuta kwamba hawawatendei haki watoto wao kwa kuwapuuza kwao. Hisia za kuona kuwa wana hatia, mara nyingi huwafanya kukosa amani ya moyo. Kwa hivyo basi, matapo (makundi) yote mawili; akina mama na watoto kama hao si tu kwamba wanapoteza furaha ya maisha yao wenyewe. Bali pia huongeza idadi ya matatizo – jamii ikiwa ni pamoja na magonjwa ya akili.
  __________________
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mzizi,...Embu waambie mods wakubadilishie heading ya thread yako, maana baada ya kusoma nimeona hilo neno "kisiasa" halihusiki kabisa hapo, badala yake weka "kisasa" ndo utaeleweka....Vinginevyo, utafiti huo ni muhimU na ingefaa kama kila mwanamke angepata nakala ya hii kitu ili ajue umuhimu wa maziwa kwa vichaNGA.
   
 3. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...PJ..Mi nadhani alitaka kumaanisha kisayansi...hata mimi nilitaka heading ilinivutia nione huo utafiti wa kisiasa kuhusu maziwa...mh!!
   
 4. B

  Bumbwini Member

  #4
  Dec 23, 2009
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli yote uliyoyasema ila tukumbuke kua sio kila kitu mpaka waseme wazungu ndio tuamini haya yote yameandikwa hata kwenye vitabu vyetu vya dini kua maziwa ya mama ni lazima mtoto anyonyeshwe kwa miaka 2 hii ni lazima imesisitizwa saana kwa ajili ya afya ya mtoto iae njema na ukuaji wake.
   
Loading...