Ushimen
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 37,194
- 85,291
Makala haya yanatokana na habari ambayo iliandikwa katika gazeti la Ammennusatia la kule Finland katika toleo lake la Julai 1989.
Kikundi kimoja cha wanajiologia (wana elimu ya miamba) wa Kirusi walikuwa katika mradi wa kutoboa tundu katika eneo la Kola, karibu na Murmansk; maili takriban 150 kaskazini mwa Duara la Aktiki, nchini Siberia. Watafiti hao waliweza kutoboa tundu ardhini lenye urefu wa kilometa 14.4 kwenda chini.
Dr Azzacov, ambaye alikuwa ndiye meneja wa mradi alisema kuwa wakati wa kutoboa, ghafla drili ilianza kuzunguka bila utaratibu, hali iliyoonyesha kwamba drili imefika kwenye sehemu iliyo na uwazi.
Taarifa tunazokusanya ni za kushangaa sana, kiasi kwamba kwa kweli tumeingiwa na hofu maana hatujui kile tunachoweza kukikuta huko chini, alisema Dr Azzacov.
Jambo la pili lililotushangaza lilikuwa ni kiwango cha joto tulichokigundua katikati ya dunia. Mahesabu yanaonyesha kuwa joto hilo lilikuwa takribani nyuzi 1,000 za Selsiasi, aliongeza kusema Dr Azzacov. Hii ni zaidi ya kile tulichotegemea. Inaonekana ni kama moto wa jehanamu unawaka kwa nguvu sana humo ndani, katikati ya dunia!
Ugunduzi wa mwisho ndio uliokuwa wa kushitua sana masikioni mwetu kiasi kwamba wanasayansi wana hofu kubwa ya kuendelea na mradi huu. Tulikuwa tukijaribu kusikiliza mjongeo wa dunia kila baada ya muda fulani kwa kutumia vinasasauti vya hali ya juu sana (supersensitive microphones), ambavyo tulikuwa tukivishusha hadi chini kupitia kwenye tundu tulilotoboa. Dr Azaccov anaendelea kueleza kwamba, Kile tulichosikia, wanasayansi hawa ambao wamezoea tu kuamini mambo yanayoleta mantiki akilini, kiliwafanya kutetemeka kwa hofu kubwa mno! Wakati mwingine hicho tulichokisikia kilisikika kwa sauti ya chini lakini kali ambayo mwanzoni tulidhani inatokana na vifaa vyetu. Lakini baada ya kuvirekebisha, tulibaini kwamba zilikuwa ni sauti zilizotoka katikati ya dunia kabisa. Hatukuamini masikio yetu. Tulisikia sauti ya mwanadamu akipiga kelele kwa maumivu. Japokuwa sauti moja ilikuwa inasikika kwa uwazi zaidi, tuliweza kusikia kwa nyuma sauti za maelfu, na huenda mamilioni ya watu wakilia kwa mateso na maumivu.
Baada ya ugunduzi huu wa kutisha, nusu ya wanasayansi waliachana na mradi huo kutokana na hofu. Ni matumaini yangu kuwa hicho kilichoko huko chini kitabia hukohuko, aliongezea Dr Azzacov.
Na kilichowamaliza kabisa nguvu hawa wanasayansi wa Kisovieti, mbali na hizo sauti walizozisikia, ilikuwa ni kutokea usiku uleule kwa gesi inayong’aa kutoka kwenye tundu lile walilokuwa wamelitoboa; na katikati yake alijitokeza kiumbe mwenye mabawa kama ya popo pamoja na maneno yaliyokuwa yameandikwa kwa Kirusi ‘Nimeshinda’.
Baada ya mkasa huo, Dr Azzacove alisema, Mimi kama mkomunisti, siamini juu ya mbingu au Biblia, lakini kama mwanasayansi, hivi sasa naamini juu ya kuwapo kwa kuzimu. Ni kweli tuliogopa sana kutokana na ugunduzi huo. Lakini tunajua fika kile tulichokiona na kukisikia. Tunaamini kabisa kuwa tulitoboa tundu kwenye lango la kuzimu yenyewe!
Je, kuna ukweli wowote kuhusuiana na tukio lililo simuliwa na watafiti hawa?
Wajuzi wa mambo "GT" ebu mkuje mtufumbue walau kwa machache tupate kujifunza.