Utafiti: Vijana wengi wahitimu wa vyuo wasio na kazi au kufanya kazi za kawaida hudanganya wana Elimu ya Kidato cha 4, 6 au Stashahada

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
Nimefanya utafiti nimegundua kundi kubwa la graduates wasio na ajira au wanaofanya kazi zinazoweza kufanywa na mtu mwenye Elimu ya chini wanajishusha elim zao

kundi hili hudanganya wana elim ya form 4, form 6 na wakienda sana basi ni Diploma.

Sizungumzii ile kujishusha ili upate kazi inayohitaji cheti cha chini, hapa nazungumzia mtu hataki kabisa na anachukia watu wajue ana Degree au Masters

Hii yote nahisi ni kukosa confidence
 
Unafikiri wanapenda?
Hili kundi wengi wana stress sana hii ni kutokana na kuangalia safari ulipoanzia na ulipoishia safari yako

mambo huwa magumu zaidi pale unapojitahid kutofautiana na wengine pale unapokutana na maisha halisi kila unachokutana nacho ni kigeni hapo unaanza kuficha hata uhalisia wako "stress"
Mimi naficha umri na elimu
 
Sasa kwenye hiyo shughuli wanataka watu wa form four na six,wewe na digirii yako unataka kazi, automatically ukisema una jiwe,umekosa kazi this why,wanajishusha
 
Lazima wajikatae kwa sababu hata jamii bado haijawakubali.

Lakini itakapofikia kizazi hiki kilichokosa ajira, kuwa ndio wazazi nadhani hawatoshangaa kwa mwenye digirii kufanya shughuli ndogo ndogo.

So watakao kuwa na digirii wakati huo wala hawatojikataa, kwa sababu itakuwa ni jambo la kawaida na jamii inaelewa hivyo.
 
tatizo jamii bado haijawakubali wenye degree kufanya kazi ndogo ndogo ...na ikitokea wakakujua itakuwa ndio habari ya kitaa.
 
Maisha kupambana mkuu ili mradi mkono uende kinywani.....Mimi nilikuwa napiga kazi na darasa la nne B kibao(Kazi za Viwandani) huku mimi nikiwa na "NYUZI MOJA" hiyo kazi niliunganishwa na rafiki yangu ,sasa rafiki yangu ndio akawa anasema usione jamaa anapiga hiyo kazi ana "NYUZI" huyo basi jamaa wakawa wanaogopa kinoma.

Baada ya kumaliza 6 nikawa napiga zege ,nafyatua tofali ili mradi kujisukuma kimaisha,,,,kwasasa NYUZI nimeiweka kabatini na vyeti nimechoma moto naendesha maisha kwa kuchoma mkaa na kuuza kitaaa!!

Vijana waache usharobaro ,wapige kazi wapate fedha MADEMU/Wanawake wanapenda mtu mwenye hela hata kama anaipata kwa njia za ajabu.
 
Ngoja tuongezeke. Maana kuanzia miaka ya 2012 wapo ambao hawajapata ajira. Sasa tykishakuwa wengiii......tukawa tumeoa tumezaa watoto na mtu anauza matunda ferry pale ndo tutakapokutana tunaongea kizungu confidently na watu wataanza kuhisi kumbe huyu jamaa ana shule.
 
ukiwa kitaa unapambana na shughuli za kitaa za kawaida kabisa sumu ni kujitambulisha una kadegree sijui yaani hiyo kazi ukimaliza hupewii nyingine wanakuogopaa..wajinga watakufanya wa maonesho sasa yoote ya nn..

mm ukinikuta kitaa ni form two b nimemaliza..

ila kitaa pasikieni tu hivyo hivyo kazi za kutumia nguvu ni balaaa kama unaroho ndogo unaweza kulia kwa asila ni ngumu iseee.
 
Back
Top Bottom