Utafiti usio rasmi: Tofauti ya Vijana wa kiume wa Kinondoni, Ilala na Temeke

smarte_r

JF-Expert Member
Nov 8, 2013
4,538
11,868
Dar ndio jiji kinara la kibiashara hapa Tanzania. jiji hili lenye mchanganyiko wa watu toka makabila yote Tanzania, lina wilaya tano, nazo ni Kinondoni, Ilala, Temeke, Ubungo na Kigamboni.

Katika uzi huu nitazungumzia wilaya tatu, ambazo ni Kinondoni, Ilala na Temeke.

kila Wilaya ina sifa zake, mathalani Kinondoni inasifika kwa kuwa na majumba mengi ya starehe, Ilala inasifika kwa kuwa na majengo mengi marefu, Temeke inasifika kwa kuwa na uwanja mkubwa wa michezo na Bandari kubwa nchini.

Lengo si kuzungumzia sifa za wilaya hizo bali ni kuangazia lifestyle za Vijana wa kiume wanaoishi ndani ya wa Wilaya hizo.

inasemekana lifestyle ya vijana wa maeneo haya matatu hutumika kama reflection kwa vijana wengi wa "mikoani".

Tuanze na Vijana wa Kinondoni:
moja ya sifa kubwa ya vijana wa kinondoni ni utanashati. linapofika suala la kupendeza na kuvaa kitanashati, vijana wa Kinondoni nawapa pongezi.

kupendeza kwao kunatokana na uwepo wa maduka mengi ya nguo na saloon za kisasa mitaa mbalimbali ya Kinondoni.

vijana wa Kinondoni wapo well informed na masuala yanayotrend mjini, hii inatokana na wengi wao kuwa karibu na celebrities. yaani ukitaka "ubuyu" wowote unaohusu mastaa, muulize kijana wa kinondoni, atakupa story nzima na ushahidi wa picha/video atakutumia.

wanapenda tabia za u-marioo.
ni jambo la kawaida kukutana na kijana wa kinondoni ana survive mjini kwa kupitia nguvu ya mwanamke. kuanzia kodi ya nyumba, gari analo drive, mavazi aliyovaa nk. vyote vimetokana na bidii ya mwanamke wake.

wanapenda sana starehe. usijaribu kushindana na kijana wa kinondoni katika kula bata. kinondoni inaongoza kwa kuwa na majumba mengi ya starehe ambayo yanakusanya vijana wa level mbalimbali za kimaisha. ni jambo la kawaida kwa kijana wa kinondoni kuunguza milioni au zaidi kwenye bata la usiku mmoja.

wana connection kubwa na watoto wa kishua. akikwambia ana urafiki na mtoto wa kigogo fulani serikalini au mtoto wa tajiri fulani usishangae wala usibishe. kumbuka Oyster bay, Masaki, Mikocheni na Mbezi Beach upepo unapovuma, zipo wilaya ya Kinondoni. haya ni maeneo ambayo wanaishi powerful and influencial figures wa jiji la Dar.

Tabia ya uchawa na kujipendekeza ni kawaida kwa vijana wa kinondoni. baadhi yao wanalipa kodi kwa uchawa, wanaendesha magari kwa uchawa na hata starehe zao zinatokana na uchawa. uchawa huu wanaufanya kupitia rafiki zao ambao ni watoto wa vigogo, matajiri au vijana wenzao ambao tayari wameshatoboa kimaisha.


Vijana wa Ilala:
wengi hupenda kujitambulisha kama wao ndio watoto wa Mjini, wazawa wa Jiji, maBoni-Tauni.

moja ya sifa kubwa ya vijana wa Ilala ni kuongea sana(tantarira) na ujanja-ujanja wa hapa na pale. hawa ndio vijana pekee wanaoishi mjini kwa kuuza maneno na maisha yao yanawaendea vizuri.

usiambatane na kijana wa ilala ambaye kutwa nzima anashinda maskani kupiga story. ikifika jioni hakosi pesa ya kula na ya bia mbili tatu za kulalia.

wengi wao wanategemea majumba ya urithi waliyoachiwa na wazee wao ambayo kwa sasa yamejengwa upya na kuwa maduka makubwa au ghorofa za kupanga.

kazi yao kubwa ni udalali, hakuna biashara ambayo itamfikia kijana wa ilala halafu asiweke cha juu, never on earth.

linapofika suala la
uchawa basi vijana wa ilala wana phd ya uchawa. hapa hata wale wa kinondoni hawatii mguu. uchawa wao wanaufanya kwa matajiri wa kiarabu ambao wengi wao wanaishi ndani ya ilala.

wapo vizuri sana katika connection na watu wa kada mbalimbali wanaofanya kazi serikalini. kama una kesi ya kudhurumiwa na kijana wa ilala, ni yeye tu aamue ushinde kesi hiyo. akiamua kutumia connection zake vizuri, nakuhakikishia humshindi hata kwa dawa. fahamu tu kwamba mahakama ya kisutu na makao makao makuu ya polisi(maarufu kama polisi central) ipo Ilala.

Vijana wa Temeke:
vijana manunda, vijana wenye roho ya paka katika utafutaji. kazi gani utampa kijana wa Temeke atashindwa kuifanya?. Hakuna.

enzi zile za utawala wa Jk, baadhi yao walitumika katika upunda. wapo waliopoteza maisha, wapo walioishia gerezani, pia wapo waliotoboa kwa upunda huohuo.

unaambiwa asilimia kubwa ya vijana wanaofanya matukio ya uporaji katika mitaa ya johannesburg na durban kule south africa ni watoto wa mbwa walitoka Temeke.

ni vijana wanaobadilika kutokana na mazingira. sio wazuri sana wa kupendeza na kupenda kula bata kama wenzao wa kinondoni, hii inatokana na wengi wao kukosa connection na baadhi yao kutokea ktk familia yenye vipato vya chini.

pia sio wajanja sana wa mjini kama wenzao wa ilala, ila wakipata fursa wanaitumia vizuri na kwa wakati.

Je, wewe upo katika kundi la vijana wa wilaya gani?. kinondoni, ilala au temeke?.
 
Nimeishi na kukulia Kinondoni tokea mwaka 1992,vijana wengi wa Kinondoni wapo hivyo ndiyo maana nilisanuka mapema nikahamia wilaya Temeke nashukuru MUNGU mara baada ya kuishi Temeke nimepata ufahamu Mkubwa Kwenye maisha.

Kinondoni ni sehemu moja ya kijinga Sana nakumbuka mitaa yetu tumekulia Kinondoni manyanya ni hatari Kwa malezi ya vijana
 
Back
Top Bottom