Utafiti: Unywaji Kahawa watibu Ini lililoathirika kwa unywaji pombe kupindukia

Ambiente Guru

JF-Expert Member
May 21, 2012
2,597
1,072
Watafiti wa Uingereza wamegegundua kuwa unywaji kahawa mfano vikombe 2 vya ziada kila siku utasaidia kuponya magonjwa ya Ini yaletwayo na unywaji pombe wa kupindukia.

Kwa sasa inasemekana hakuna dawa kamili za kuponya magonjwa ya ini.

Chanzo: Reuters; Drinking more coffee may undo liver damage from booze | Reuters
 
Na watafiti wengine wanasema kahawa hiyo hiyo ukizidisha inaleta high blood pressure...
 
Utafiti hautafitiwi kwa kufanya utafiti

sasa mkuu iweje tafiti za kitu kimoja ziwe na majibu tofauti? Ndio maana nikasema inabidi tuzifanyie utafiti hizi tafiti zenyewe kuona kwamba zinavigezo na sifa za kuitwa tafiti....shukrani.
 
Kweli mdau mpaka sasa kuna ushahidi kuwa matokeo mengi yaawali ya utafita uamepigwa chini. Mfano Cholestrol and vidonda vya tumbo

Mkubwa mimi sina neno na wewe kabisa, tatizo langu ni hizo tafiti, tafiti nyingine wanashauri usinywe kahawa kwa wingi (Kupita kiasi), wengine ndio hawa wanasema unywe kwa wingi kutibu maradhi....au unatakiwa kunywa nyingi kama una maradhi ili iwe ni kama dawa na sio kiburudisho?
 
Hizi tafiti za kumalizia shule wakizi upload tukizisoma lzma tuchanganyikiwe. Sababu kila mtu anaibuka na topic yake anapikapika mwisho anapata masters yake life goes on
 
Mkubwa mimi sina neno na wewe kabisa, tatizo langu ni hizo tafiti, tafiti nyingine wanashauri usinywe kahawa kwa wingi (Kupita kiasi), wengine ndio hawa wanasema unywe kwa wingi kutibu maradhi....au unatakiwa kunywa nyingi kama una maradhi ili iwe ni kama dawa na sio kiburudisho?

Wauza kahawa ndio wanagharamia tafiti hizi. Kwa wenzetu Kahawa na Pombe huuzwa bar. Pengine wanataka walevi waendelee kwenda bar hata baada ya kuathirika na unywaji wa kupindukua ili wakatibiwe hapo hapo na waendelee kuwa wateja wao.
 
Back
Top Bottom