UTAFITI UNAONYESHA WANAUME WANAOCHEPUKA HUA NA AKILI NDOGO

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
KUNA UTAFITI UNASEMA WANAUME WANAOCHEPUKA HUWA NA AKILI NDOGO JE KUNA UKWELI HAPA AU NI KUWACHANGANYA WANAUME.

SEMA USIKIKE.

Dah!! hii ni kubwa kuliko tareh 22/08/2018 katika kudadisi na kuchokonoa nilibahatika kupata kusoma tafiti fulani kwamba "WANAUME WANAOCHEPUKA HUWA NA AKILI NDOGO". Utafiti huo ndiyo umepelekea kuandika makala hii ambayo inaweza kutupa majibu fulana japo kwa kifupi uwepo wa mwanamke katika jamii kumekuwa kuwachanganya na kuwavuruga sana Wanaume na hii inaonyesha wazi kwamba Wanawake wana nguvu na ushawishi mkubwa mno kwa mwanaume ndiyo ni ngumu sana kusikia mwanamke amejinyonga kisa mwanaume ila wanaume wengi hujinyonga ama kujitoa uhai kisa Mwanamke.

Kumekuwa na tabia ya watu kusingizia wataalamu wamesema. Utakaa kidogo utaambiwa mtaalamu fulani kasema bila kuwa na taarifa ya uhakika, Kusema kwamba wanaume wanachepuka hawana akili siyo utafiti bali ni maneno tu ambayo yanalenga mambo fulani, Kuna utafiti unasema kwamba WANAUME WANAO KUNYWA POMBE WANA MBEGU SAFI, kwa mfano utafiti huu unahimiza wanaume kunywa pombe ili wawe na mbegu safi ina maana ili uwe na mbegu safi unapaswa kunywa pombe tafiti hizi zipo kibiashara zaidi wakati pombe yoyote ile ni hatari kwa Afya

Hizi tafiti huwa nani anafanya mpaka kuja na kauli ngumu kiasi hichi, kauli hiyo ya kusema kwamba WANAUME WANACHEPUKA WANA AKILI NDOGO huko ni kuwachanganya wanaume hata kama kuna ukweli ndani yake na imeonekana kama shambulio la moyo kwa wanaume ambao wanachepuka katika ndoa. Japokuwa pia ni vyema tukakumbushana kwamba wanaume ambao hawachepuki katika ndoa zao ni wachache sana hususani kuanzia miaka 25-45 tena akiwa na hela ndiyo bala tupu japo siyo wote kuna ambao wako safi.

Hivi swala la kuchepuka pia linahitaji kuwa na akili nyingi ama ndogo embu twende sawa japo kidogo nina mifano michache hapo chini kama kuna ukweli wowote ule au ndio tafiti za Twawaweza ambao watakuja na hili kesho watakuja na lile,twende sawa kwanza simaanishi kuchepuka ni jambo jema sana kwa waliokuwa katika ndoa ila na hoji tu Maswali kidogo na ufafanzi juu ya watu wakubwa na mashuhuri duniani waliowahi kuchepuka je na wao wana akili ndogo. Na kwa nini iwe wanaume wanaochepuka wawe na akili ndogo, ni akili zipi hizo wanazozizungumzia hapa.

Vipi kuhusu Jay Z alikiri mwenyewe kwa kinywa chake kwamba amekuwa akichepuka kwa muda sasa vipi na yeye ana akili ndogo maana alichepuka tena siyo mara moja, Mfalme Daudi alichepuka tena akiwa mfalme kwa kuzini na mke wa mtumishi wake kwa hiyo na yeye alikuwa na akili ndogo au tatizo liko wapi hapa kwa nini mambo haya yameonekana kuharibu ndoa nyingi za watu ,suala la kuchepuka imekuwa ni Debate ambayo imekosa majibu hakika,kwa nini wanaume wanachepuka mbali na kuwa na wanawake waaminifu na wenye sifa ndani ya ndoa zao.

Ok inawezekana haitoshi twende tukangalie Bill Clinton alichepuka tena akiwa rais wa Marekani taifa kubwa na yeye ana akili ndogo kama hoja ni kwamba wanao chepuka wana akili ndogo kama tafiti zinavyosema watu wakubwa wamekuwa wanakumbwa na kashfa za uchepukaji je wanaume wanashida gani haswa. Twende Afrika Winnie Mandela alichepuka muda wote ambao Mandela akiwa gerezani na hata alivyotoka bado Winnie aliendelea kuchepuka vip winnie unaweza kusema ana akili kubwa au ni maamuzi tu ya mtu binafsi, ukienda mbali zaidi hata Nicholasi Muduro na Hugo Chaves na yeye alifanya hivyo na hawa ni watu mashuhuri Duniani je hawa wana akili ndogo ama kuna sababu tofauti na hapa.

Twende mbali zaidi mfalme Suleimani alikuwa anachepuka tena pengine kuliko binadamu yoyote yule katika historia ya Dunia je ina maana ana akili ndogo pia na alikuwa mtu mwenye hekima na maarifa kuliko mtu yoyote yule katika hii Dunia na utajiri wake hauna kipimo wala hakuna wa kumlinganisha kulingana na vitabu vinavyosema naye ukisema wanaochepuka wana akili ndogo inakuwa ni mdahalo mkubwa ambayo hatuwezi kumaliza leo kuna ambao wataenda mbali zaidi ya hapa kwamba kwa sababu alikuwa mfalme .

Twende tumwangalie Jacob Zuma alichepuka tena akiwa kama Rais na Mwemyekiti wa chama kikubwa kabisa Afrika ANC. Je na yeye tumuingize kwenye kundi la watu wenye akili ndogo kisa wamechepuka ..? Miaka ya 80s Mugabe alikuwa anachepuka na Grace uku akimuacha mke wake Sarah Francisca ndani vipi hapo utasema Mugabe alikuwa na akili ndogo twende kwa Dangote na yeye ana record zake za kuchepuka vipi na yeye ana akili ndogo, waungwana haya wakini Napoleon Bonaparte aliyetawala Dunia miaka ya 1804-1815 je na yeye alikuwa na akili ndogo,kwa nini wanaume hawatulii wanapoona sketi zikikatizo mbele yao.

Hapa kwetu Tanzania tumeshuhudia Pia Diamond Platnum akiingiaa kwenye zongoto zito baada ya kuchepuka na kuanza kutoka na mwanamitindo Hamisa Mobote mpaka kupelekea kupata mtoto mmoja wa kiume na matokeo yake kusababisha kuachana na mzazi mwenzake Zarina Hassani ambayo alishindwa kuvumiliaa kile alichokiita uchafu wa Diamond,Swali ni je kwa ni wanaume wanachepuka wanakuwa wamekosa nini mpaka wanaacha wake zao na kutoka nje ya ndoa zao je tunaweza kitendo cha Diamond kuchepuka je na yeye alikuwa ana akili ndogo au kuna kinachowafanya wanaume kuchepuka..??

Siyo kila tafiti hutolewa kwa malengo mema katika jamiii zingine zinatolewa tu kwa lengo la kuharibu na kuwagawa watu katika makundi ili mpate cha kujadili na kusahau mambo ya msingi. Katika kizazi cha sasa tafiti zimekuwa nyingi sana ukifungua tu utaambiwa sijui kuna utafiti umefanyika kwamba WANAWAKE WENYE MAKALIO MAKUBWA WANAZAA WATOTO WENYE AKILI SANA. Hizi tafiti zinawafanya kunachanhanyikiwa na kujenga imani fulani ambayo kuwafanya vijana waanze kuhangaika kutafuta makalio makubwa ili wapate watoto wenye akili.

Tafiti hizi mara nyingi zipo kibiashara zaid kwa mfano hivi kuna uhusiano gani kati ya makalio makubwa na akili kwa mtoto , Baada ya kutanguliza hayo hapo juu naomba tuendelea kuchambua hii kauli inayosema kwamba WANAUME WANAOCHEPUKA WANA AKILI NDOGO maana nayo hii ni tafiti imefanyika.Lakini cha msingi hapa lazima kutambua kwamba kuna matangazo na tafiti. Kuna kipindi fulani niliwahi kusikia kwamba WANAUME WAFUPI NDIO WANADUMU KATIKA NDOA ZAO.

Utafiti huu ulidai kwamba wanaume wafupi wanajua kupenda na kunyenyekea zaidi na kuna baadhi ya jamii au watu wanaamini hivyo. Lakini kinachoonekana pia ni kwamba watu wafupi wanadumu kwenye ndoa zao kwa sababu ya uoga ila hili pia halina uhakika sana, tutambue kwamba mengine ni matamko na siyo tafiti, tafiti zingine kwa ajili ya kuelimisha ili watu waufahamu ukweli lakini pia tafiti zingine kwa ajili ya kuongeza maarifa na zingine zinafanyika kwa ajili kutatua matatizo katika jamiii fulani na tafiti zingine zinakuja tu kwa ajili ya kuwachanganya watu wa jamii fulani.

Ukweli usipingika kwamba mwanaume anayechepuka akiwa katika katika ndoa yake hata ukimwita hana akili ama ukamwita mpumbavu au jina lingine lolote lile unakuwa huko sawa maana ni makubali ya mwanadamu kwamba ukishakuwa kwenye ndoa hupaswi kuchepuka bali unapaswa kuwa mwaminifu kwa mke wako. Lakini wanaposema wanaume wanaochepuka wana akili ndogo ni akili ipi hiyo wanayoizungumzia na utafiti huu umewalenga wanaume pekee yao .kiasi kwamba wanawake wao wanachepuka kwa akili tofauti na wanaume.

Tafiti zingine za ajabu sana kuna sababu zinazomfanya mtu achepuke japokuwa wenye sababu za msingi ni wachache kulinanga na muda naomba niseme tu kwamba mwanaume kuchepuka hakuitaji kuwa na akili ndogo ama kubwa, Kuchepuka kwa mwanaume kuna sababu nyingi sana wengine wana sababu za msingi wengine wanasababu za sekondari na wengine wanasababu za Chuo kikuu nitaendelea katika makala inayofuata kuelezea kwa nini mwaume anachepuka
 
Wewe jamaa una copy na Ku paste.!?

Nyuzi zako nimeona zaidi ya saba na zinaongelea mahusiano
 
Back
Top Bottom