Utafiti unaonesha kuwa watanzania wengi hawajui mambo ya siasa..

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,530
2,000
Mitandao inadanganya sana! Ukiingia humu unaweza kudhani kwamba nchi nzima ipo aware na masuala ya kisiasa nchini..

Wenye access na mitandao ni wachache sana hivyo matokeo ya utafiti haya yanaweka wazi hali halisi ambayo nakubaliana nayo..Just imagine population ya huko shamba.. Wangapi wanatumia hii mitandao?

Ndio maana hii mikutano ya kisiasa ilifaa sana iachwe ili angalau wanasiasa wafike huko wakawafundishe wananchi uraia na masuala nyeti ya kitaifa kupitia siasa.

Wananchi kutojua siasa ni hasara.. Maana yake wapo gizani hawajui nchi inaendeshwaje, haki zao ni zipi na wajibu wa wanaowachagua ni upi..

Tusiliache lenyewe hili kundi. 61% ni kubwa jamani!

7.JPG
 
Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,213
2,000
Na kuna wale wanasiasa wanaofanya sampling ya mitandao kupima kukubalika kwao halafu matokeo ya uchaguzi yakitoka hawaamini macho yao na kudhani 'wamepigwa changa'.

Mitandao hii!
 
DuppyConqueror

JF-Expert Member
Mar 30, 2014
9,451
2,000
Kutokuwa na taarifa ya nini kinaendelea (current [political]affairs) haimaanishi hujui siasa..
 
ZENJIBARIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
595
1,000
na ni nchi gani wanaojua siasa,mataifa yote siasa inaletwa na watawala ili kuwalaghai wananchi wamyonge kupitia mfumo siasa, siasa ni ulaghai ili watu wajione kama na wao ni sehemu ya serikali na wajione kama na wao wana michango kwenye vyombo vya dola lakini uhalisi haupo hivyo ni njia ya kikundi kidogo kutawala wasiojifahamu wengi hio ndio siasa halisi
 
kelvin complex

JF-Expert Member
Jul 27, 2013
573
500
Hakuna viongozi wa kisiasa wa ngazi za chini huko wakafanya kazi ya kusambaza habari na elimu ya uraia? Vyama vinapaswa kujiimarisha kuanzia ngazi za chini, tatizo vyama vyetu vinajisahau kujiimarisha kuanzia ngazi za chini
 
Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,213
2,000
Hakuna viongozi wa kisiasa wa ngazi za chini huko wakafanya kazi ya kusambaza habari na elimu ya uraia? Vyama vinapaswa kujiimarisha kuanzia ngazi za chini, tatizo vyama vyetu vinajisahau kujiimarisha kuanzia ngazi za chini
CCM wanajitahidi eneo hilo.. Tatizo ni psyche ya kweli katika kuhudumia taifa haipo kwa viongozi wengi... Maslahi binafsi tu..
 
Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,213
2,000
na ni nchi gani wanaojua siasa,mataifa yote siasa inaletwa na watawala ili kuwalghai wananchi wanmyonge kupitia mfumo siasa, siasa ni ulaghai watu wajione kama na wao ni sehemu ya serikali na wajione kama na wao wana michango kwenye vyombo vya dola lakini uhalisi haupo hivyo ni njia ya ki8kundi kidogo kutawala wasijifahamu wengi hio ndio siasa halisi
Mmh! Kama kweli hivi...
 
Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,469
2,000
Mbona raisi wa nchi hii sio mwanasiasa, kwa hiyo hakuna haja ya wananchi kujua siasa. Hii ni kwa maneno yao wenyewe
 
Yales

JF-Expert Member
Oct 3, 2015
518
500
Ni kweli usemalo na uambie pia hao Viongozi wanaojipimia ushindi kuputia social media wanakosea sana mataifa endelevu ni sahihi ila sio bongo ambapo watu wengi hawana access na mitandao
 
Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,578
2,000
beth,

Mkuu,

Kama viongozi wenyewe wa kitaifa wa vyama hawajui siasa unadhani wananchi wengine hao watazijulia wapi!?

Wananchi wakisikia fulani kasema hivi wanaelekea huko, upepo ukibadilika tayari wanakuwa huko nao.

Yaani ni, varuvaru kinyamaa ni hakuna utaratibu kwa ujumla.
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
15,741
2,000
wengine bora wakae hivyohivyo tu wakifatilia watajiongezea frustration!
 
treborx

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,634
2,000
Mitandao ingekuwa inasomwa na asilimia kubwa ya watanzania ingeshapigwa marufuku siku nyingi.
 
900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
3,132
2,000
Mitandao inadanganya sana! Ukiingia humu unaweza kudhani kwamba nchi nzima ipo aware na masuala ya kisiasa nchini..

Wenye access na mitandao ni wachache sana hivyo matokeo ya utafiti haya yanaweka wazi hali halisi ambayo nakubaliana nayo..Just imagine population ya huko shamba.. Wangapi wanatumia hii mitandao?

Ndio maana hii mikutano ya kisiasa ilifaa sana iachwe ili angalau wanasiasa wafike huko wakawafundishe wananchi uraia na masuala nyeti ya kitaifa kupitia siasa.

Wananchi kutojua siasa ni hasara.. Maana yake wapo gizani hawajui nchi inaendeshwaje, haki zao ni zipi na wajibu wa wanaowachagua ni upi..

Tusiliache lenyewe hili kundi. 61% ni kubwa jamani!

View attachment 648480
me mwenyewe nipo shamba,watu wako na ma smatphone wanatupia vitu c mchezo
 
Rudeboytz

Member
Jun 23, 2020
81
225
Mitandao inadanganya sana! Ukiingia humu unaweza kudhani kwamba nchi nzima ipo aware na masuala ya kisiasa nchini..

Wenye access na mitandao ni wachache sana hivyo matokeo ya utafiti haya yanaweka wazi hali halisi ambayo nakubaliana nayo..Just imagine population ya huko shamba.. Wangapi wanatumia hii mitandao?

Ndio maana hii mikutano ya kisiasa ilifaa sana iachwe ili angalau wanasiasa wafike huko wakawafundishe wananchi uraia na masuala nyeti ya kitaifa kupitia siasa.

Wananchi kutojua siasa ni hasara.. Maana yake wapo gizani hawajui nchi inaendeshwaje, haki zao ni zipi na wajibu wa wanaowachagua ni upi..

Tusiliache lenyewe hili kundi. 61% ni kubwa jamani!

View attachment 648480
Maisha ya kuwaza kitu kidogo ambacho kipo milele ila mkitaka kuyaondoa ondoeni maisha ya watu kufuata hela nyingi mahali (BUNGENI) kila mtu ajiwakilishe mwenyewe.... Kazi ndogo ipo siku kila kitu ni kukimbiana kwenye kusolve matatizo ili kuondoa hali hiyo ni bunge pekee litatumika next time kwa sababu inawapumbavu wa elimu zote kuanzia Darasa la Saba hadi Profesa... Maisha ya kujifungia na kaelimu kako utaelewa kila kazi baibai...

Bunge la mfano kwa watu hawa ni muhimu kama bunge la kumi na moja lilivyoitisha bunge la watoto kumbukeni mnazaa watoto labda mnataka wasifanye kazi na watu milele:

1. Bunge la mfano la Mitandao ya kijamii

2. Bunge la mfano la wachumi (DPP)

3. Bunge la mfano la Wanajeshi

4. Bunge la mfano la sekta ya Madini

5. Bunge la mfano la mapolisi

6. Bunge la mfano la wastaafu

7. Bunge la mfano la wamachinga

8. Bunge la mfano la mamalishe

9. Bunge la mfano la DINI

10. Bunge la mfano la trafiki

11. BUNGE LA MFANO LA WASANII NA VIDEO QEEN

12. Bunge la mfano la wanasheria

13. Bunge la mfano la WAZEE

NA KATHALIKA

HAPA WALAU KIDOGO MTAJENGA NCHI YA WALUMI KILAHISI
 
wakubeti

JF-Expert Member
Oct 5, 2018
562
1,000
Siokujua mambo yakisiasa tu kwakifupi watanzania wengi wanauwezo mdogo sana kiakili hautoshi kabisa kudeal na vitu vinavotuzunguka haijalishi anakua ameenda shule au hajaenda.
Seriously kabisa wizara ya afya ijitahid kufatlia nin chanzo mpaka tunakua taifa lenye moron's kwenye kila mahali kuanzia uraian Maofisin kwenye mabiashara kwenye siasa mpka kwa viongoz wetu wajuu.

Imagine jecha anachukua form yakuwania urais kwa znz nawanchi wanajionea sawa tu
 
Travic

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
720

Yaani!

Nilikuwa namwambia mtu siku moja kwamba tuna tatizo la kiakili nchi nzima (national psyche). Ukifanywa utafiti, naamini utabaini kwa wastani akili zetu zina mushkeli kama taifa.

Achana na kuwa logical na analytical, angalia mfano kwenye comprehension tu. Watu hawaelewi vitu vyepesi kabisa.

Fuatilia hata thread inapoanzishwa humu na inaweza kuwa imejitosheleza kila kitu lakini bado wengi wanasoma na hawaelewi. Wanachangia vitu havihusiani kabisa na mada husika. Unaweza kucheka!

Ni tatizo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom