Utafiti Synovate: Dk Slaa ang’ara urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utafiti Synovate: Dk Slaa ang’ara urais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Analytical, Aug 4, 2011.

 1. A

  Analytical Senior Member

  #1
  Aug 4, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Dk Slaa ang'ara urais
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 03 August 2011 23:11 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/14202-dk-slaa-angara-urais.html

  NI IWAPO UCHAGUZI MKUU UNGEFANYIKA SASA ANGESHINDA.
  Leon Bahati
  MATOKEO ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Synovate yanaonyesha kwamba iwapo Rais Jakaya Kikwete angeamua kujiweka kando na ukaitishwa Uchaguzi Mkuu sasa, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi wa nafasi hiyo.Ripoti ya Synovate iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana ambayo inawapa wapinzani fursa ya ushindi kwa mara ya kwanza, wagombea kutoka vyama vya upinzani wana uwezo wa kupata asilimia 67 iwapo uchaguzi ungefanyika sasa.
  Dk Slaa anaongoza kwa kupata asilimia 42, akifuatiwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (asilimia 14), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (asilimia 12) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe asilimia tisa.
  Synovate inaeleza kwenye ripoti hiyo kwamba matokeo ya utafiti huo yanatokana na watu mbalimbali wenye umri zaidi ya kuanzia miaka 18 walioulizwa maswali ya ana kwa ana vijijini na mijini.
  Katika kupata maoni juu ya mtu ambaye wangependa awe rais waliuliza: "Mbali na Rais Jakaya Kiwete, ni mtu gani ungeweza kumchagua kuwa Rais iwapo atakuwa miongoni mwa wagombea?"
  Kwa mujibu wa matokeo hayo, iwapo uchaguzi ungefanyika sasa, Pinda angeambulia nafasi ya tatu licha ya kwamba CCM ndicho chama kinachoongoza kwa kuaminika mbele ya umma ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.Katika utafiti wake huo uliofanywa kati ya Mei 2 hadi 29, mwaka huu, jumla ya watu 1,994 walihojiwa.

  CCM wamtaka Dk Slaa
  Utafiti huo unaonyesha kuwa wanachama wengi wa CCM walionyesha kuvutiwa na Dk Slaa ikilinganishwa na viongozi wengine ndani ya chama hicho tawala.Hii inatokana na takwimu kuonyesha kuwa kati ya waliohojiwa katika utafiti huo, wengi wanatokana na CCM, lakini wakamchagua Dk Slaa.
  Takwimu za ripoti hiyo zinaonyesha kuwa kati ya waliohojiwa, walipoulizwa kuhusu vyama vyao asilimia 51 walisema ni CCM, asilimia 35 wakasema Chadema, 10, CUF na TLP asilimia moja.
  Mbali na Dk Slaa, Profesa Lipumba, Pinda na Zitto wanasiasa wengine wanne wanaofuatia ambao asilimia walizopata zimo kwenye mabano ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (4), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (2).
  Kadhalika, vigogo tisa waliofungana kwa kupata asilimia moja ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya.
  Katika utafiti huo, Synovate iliegemea nyanja tatu za utafiti ambazo ni siasa, uchumi na masuala ya kijamii na utamaduni.
  Mgombea urais CCM 2015
  Ndani ya CCM, anayepewa nafasi ya kwanza kuwa mgombea urais kwa mwaka 2015 ni Pinda aliyepata asilimia 35 akifuatiwa na Dk Magufuli asilimia 14.
  Wanaofuatia kwa mvuto pamoja na asilimia walizopata kwenye mabano ni Membe (8), Sitta (3), Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (3), Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa (3) na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi (2).
  Vigogo tisa ndani ya CCM walifungana kwa kupata asilimia moja nao ni Makinda, Dk Mwakyembe, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Magembe na Waziri Mkuu wa zamani, Dk Salim Ahmed Salim.
  Wengine ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.
  Uvuaji gamba CCM
  Utafiti huo wa Synovate unaonyesha kuwa Watanzania wengi wanatofautiana juu ya uelewa wa mpango wa CCM wa kujivua gamba.
  Katika mpango huo ripoti hiyo inasema asilimia 41 walisema ni mpango wa kuwataka watu kujiuzulu kwenye uongozi wakati asilimia 29 walisema ni mpango wa kutaka kukisafisha chama.
  Inaonyesha kuwa asilimia 15 ya waliohojiwa walielezea kujivua gamba kuwa ni mabadiliko ya uongozi kwa kuondoa viongozi wabovu na asilimia tano wakasema ni mpango wa kuondoa viongozi wote watuhumiwa wa ufisadi.
  Asilimia mbili walisema ni mpango wa kukifanya chama hicho cha siasa kiwe na mfumo wa wazi na unaoeleweka wakati asilimia moja walisema ni suala la kujizuzulu, kutafuta viongozi wachapakazi na wenye tija. Kuna wanaouchukulia kuwa ni mkakati wa kisanii wa kuwadanganya wananchi.
  Kwa ujumla, taarifa hiyo ilisema ni asilimia 45 tu ambao wana taarifa kuwa kuna Sekretarieti ya CCM ilijiuzulu na Mwenyekiti wake, Rais Kikwete amekwishateua wengine kushika nafasi hizo.

  Kero kubwa nchini
  Asilimia 56 walisema tatizo kubwa linalowakumba ni kupanda kwa bei ya vyakula, gharama za maisha na umaskini na asilimia 46 walisema njaa na tatizo kwenye kilimo.
  Tatizo la ufisadi nchini lilichukua nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 36, ukosefu wa ajira (31), tatizo la nyumba, barabara na umeme (27), elimu (23), afya (21), maji (16), uharibifu wa mazingira (12), taasisi za siasa (10), haki za binadamu, uhalifu (6) ubeberu na usafirishaji wa dawa za kulevya (3).

  Katiba Mpya
  Miongoni mwa mambo ambayo yanatajwa kuwa ni vikwazo kwa Tanzania kupata Katiba Mpya ni rushwa (26), kukosekana kwa umoja (19), maslahi ya kisiasa (18), ufahamu mdogo (11) na kukosekana kwa msukumo wa kisiasa (9).
  Hata hivyo, asilimia 78 walisema wanataka yawepo mabadiliko ya katiba nchini wakati asilimia 21 hawaoni umuhimu wake.
  Lakini asilimia 42 walisema wana uhakika kwamba mpango wa Katiba Mpya utafanikiwa.
  Lakini pia makosa ya Katiba iliyopo yalielezwa kuwa ni kupitwa na wakati, kuandikwa kwa Kiingereza zaidi kuliko Kiswahili, kukosekana kwa utawala bora, kutokuwepo kwa sheria za haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #2
  Aug 4, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,240
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Wanafiki tu hawa!!
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  huyu ndiye rais aliyechaguliwa na wananchi 2010
   
 4. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Why today?
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Acha kuota kabla ya kulala, hapa anshindanishwa na watoto wenzake, Zitto na Lipumba, halafu si unajua synovate ni wachakachuaji inawezekana Zitto anaongoza.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  K@#%nina zao. Hawa si ndio waliochakachua maoni kabla ya uchaguzi kumpendelea Kikwete?
   
 7. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #7
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280

  Ile ripoti ya uchaguzi ...walilazimishwa ..na suala lile lilileta ugomvi hata ndani ya Synovate ...maana wana sifa ya kutoa mawazo huru ..nadhani JK alimrubuni resident manager wa Synovate akaaandaa ripoti mbili moja ya kweli akatuma Nairobi[HQ] Na placebo ya kumpendelea JK.....

  Hii ripoti ya sasa tusubiri response ya ccm,maana it is not in there favour.....itabidi wakimbilie REDET[wanyonge wao] waombe counter report..
   
 8. D

  Dundei kinabo Member

  #8
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema tupo juu ile mbaya.
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  whatever ilimradi ssm isiongoze mimi poa tu , tena zitto namkubali sana tu ,huyu kamanda lazima aongoze hii nchi
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  but chadema hawajui kuwa kuna wana ccm wako tayari kuwapigia kura
  wao wanafikiri wana ccm wote ni mafisadi....
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Haya mambo ya Synovate, ni mambo ya kupika. Haiwezekani Zitto aka maarufu kuliko Lissu au Mbowe. Ni mkakati unaolenga kuleta mgawanyiko CDM kwa kutaka kumpa kichwa huyu wakala wa usalama wa taifa. Au haiwezekani mtu kama Pinda ambaye hawezi hata kufanya maamuzi badala yake anaishia kulilia akawa juu kuliko Lowassa au Membe mwanamme wa shoka ambaye anawaendesha puta kina Chenge katika wizi wa rada.

  Waache unafiki, hatutaki kusikia vitu vilivyopikwa na mashushushu.
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Duh!!!!!!! Sasa kwa nini huyo JK wamemweka kando????????????????????
   
 13. Companero

  Companero Platinum Member

  #13
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Labda wanaogopa kesi ya uhaini!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 14. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Damn!!!!!!! haha ahaha ahahah!!! anywayz mambo ya kibongo hayo, nakumbuka G. Bush alikuwa kwenye polls mpaka Dec. 2007 na sometimes mpaka leo hii huwa ana-appear!!!!
   
 15. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,276
  Trophy Points: 280
  Hii ripoti ni ya kichochezi atasema Wassiraa au Lukuvi, na kuomba mwongozo
   
 16. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Wanafiki wakubwa hawa wanatengeneza mazingira yakujaza matumbo yao na mautafiti yao ya ovyo ovyo yakupika.
  Tumewashtukia na huu utafiti wao ambao lengo nikutaka Magamba wajikoki waingilie kati nakuwahonga ili waje nautafiti mwingine in favour of Magamba.Njaa zitawaua nyie Synovate watanzania wa sasa sio wa mwaka 47 na kamwe hatutawaamini hata mkiingia kwa gia ya Cdm credibility yenu ishapotea fukuza management yote iliyo husika kuchakachua utafiti 2010 mje kivingine ila kama ndo walewale wa Uchaguzi 2010 imekula kwenu.
   
 17. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  The Boss sidhani kama huu ni mtazamo wa CDM, kwani kwenye list of shame hawakuoroshena watu Mill 5 wanaokisiwa kuwa wana kadi za CCM
   
 18. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Njaa ndo zinawasumbua Synovate kama ungefanyika ila njo kwenye uhalisia wangekuambia ccm wangeshinda.
   
 19. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Naomba mods muiweke hii post ikifika January 2015 muilete hapa!hao hao Synovate ndio watakuwa wa kwanza kukana hii ripoti yao!wazush tu hawa!ukiwauliza walimuhoji nani utasikia wajumbe wa nyumba kumi kumi.
   
 20. m

  mzee wa mawe Senior Member

  #20
  Aug 4, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 151
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa synovate ni wanafiki tu, hawa ni waganga njaa nadhani na chadema nao wameishawatembelea
   
Loading...