Utafiti rushwa ya ngono wa TAKUKURU haukufanyika kisayansi

DidYouKnow

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
1,094
1,689
Mimi ni mmojawapo wa watu waliosoma kwa undani taarifa ya Utafiti (si uchunguzi) ya Rushwa ya Ngono katika vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Dodoma iliyotolewa na TAKUKURU.

Ni jambo la kufurahisha kuona taasisi za serikali zinajua umuhimu wa kufanya tafiti ili kufikia malengo yake. Hivyo huu ni mwanzo mzuri. Lakini bado sijaelewa vizuri, kipi kingetoa taarifa nzuri - Utafiti ama Uchunguzi?

Tunajua kwamba walioathirika na rushwa ya ngono, huumia kimya kimya pasipo kutoa taarifa. Ni jambo ambalo humtesa victim maisha yake yote. Bahati mbaya pia, tunapoongelea rushwa hiihii ya ngono, tunasahau asilimia ndogo ya watu ambao husingiziwa kutenda hili tendo na athari zao zinafanana na yule ambaye kaathirika na rushwa ya ngono.

Katika taarifa hii ya utafiti inaonesha TAKUKURU iliingia ubia na Asasi ya Kiraia ya
Women Trust Fund (WFT) ili kufanikisha malengo ya Utafiti. WFT inajipambanua kutetea haki za wanawake na inatoa misaada kwa taasisi au watu yenye uegemeo huohuo. Kwangu, hili ni kosa, maana kuwa na mshirika mwenye uegemeo kama WFT ambaye anatetea haki za wanawake, kunasababisha utafiti wako uwe na bias, kwani WFT atahakikisha kunaoneshwa tatizo ili azidi kupata ufadhili.

Katika Utafiti huu wa rushwa ya ngono Tanzania, uliofanyika katika vyuo vikuu viwili vikubwa nchini Tanzania yaani UDSM na UDOM. Vyuo hivi vinadahilii zaidi ya wanafunzi 20,000 kwa mwaka, hiki ikiwakilisha zaidi ya asimia thelathini na tano ya udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania, kila mwaka.

Watafiti waliamua kutumia mfumo wa case study, ili kuweza kupata majibu ya maswali yao. Walifanya utafiti kwa kutumia sampuli ya walimu na wanafunzi 589 kwa kutumia utaratibu wa mpangilio maalumu. Sina uhakika na uchaguzi wao wa sampuli ya walimu na wanafunzi kama ulikuwa sahihi kuzalisha majibu ya maswali yao, lakini ninaamini kulikuwa na umuhimu pia kuwa na live cases za wanafunzi walioathirika. Wangeweza hata kujitokeza kwa siri.

Nimepata ukakasi kwenye baadhi ya sentensi za hitimisho la utafiti.

1. Kwa ujumla, utafiti umebaini kwamba tatizo la rushwa ya ngono kwenye vyuo vilivyoshiriki lipo na kwamba tatizo hili ni kubwa na si la kupuuzwa. Shuhuda za waathiriwa wa rushwa ya ngono pamoja na shuhuda za uwepo wa watuhumiwa ambao hawajachukuliwa hatua zilitolewa.

Kwanini waseme kwamba tatizo hili ni kubwa katika vyuo hivi viwili - UDSM na UDOM? Ukubwa unaangaliwa kwa simulizi za shuhuda au kuwa na waathirika?

Watafiti walijuaje kama rushwa ya ngono ni kubwa, wakati haijaonesha ni watu wangapi katika sampuli walikiri kwamba wao ni waathirika wa rushwa ya ngono
?

Inawezekana kwa sababu hawa washiriki wako katika chuo kimoja, yamkini kulikuwa na tukio moja (au matukio kadhaa) lilitokea chuoni na sampuli yako yote ikawa inalifahamu, wakati wa mahojiano kila mtu akakiri kuna tatizo, lakini haimaanisha tatizo ni kubwa. Maana wote wana reference moja. Lakini pia sampuli yako, inaweza ikawa ina taarifa ambazo si za kweli, na ikasema kuna tatizo. Hebu fikiria tukio la mwanzo wa mwaka 2020, wale madaktari wa Mbeya walivyoandikwa, (ati zilikuwa ni chuki miongoni mwa madaktari wenyewe), halafu ukachukua sampuli ya watu ambao wamepata habari hizo na zikatrendi hadi Twitter, lazima hitimisho lako itakuwa tatizo kubwa.

Kama kuna watu katika sampuli wakati wa mahojiano walidai kuathirika na rushwa ya ngono, Je, kutoa tuhuma kunamfanya mtu kuwa mwathirika halisi? Mimi sidhani. Hapa ni sawa na daktari ahesabu uwingi wa wagonjwa wa Malaria kwa sababu mgonjwa kaenda hospitali akidai yeye anaumwa Malaria. Daktari mzuri atataka mgonjwa apime kwanza. Ni kitu gani kinafanyika ili kuhoji ukweli wa tuhuma iwe katika utafiti au uchunguzi?

2. Watafiti wanasema lengo la utafiti huu ni kuwezesha upatikanaji wa taarifa za kisayansi zitakazosaidia kukabiliana na vitendo vya rushwa ya ngono katika Taasisi za elimu ya juu nchini.

Sasa mimi najiuliza: Ni taarifa zipi mpya (mpya tu, achana na za kisayansi) TAKUKURU wamezipata kupitia utafiti huu? Taarifa ambazo wasingezipata kwa kufanya uchunguzi wao makini wa kila siku? Mbona naona mambo mengi yako obvious, wala huhitaji kutafiti.

5. Wanaodaiwa kujihusisha na rushwa ya ngono wanavyoendelea kupewa nyadhifa
mbambalimbali za uongozi na vyeo vya kitaaluma. Shuhuda za waathiriwa wa rushwa ya ngono pamoja na shuhuda za uwepo wa watuhumiwa ambao hawajachukuliwa hatua zilitolewa.

Sidhani kama ni sahihi katika nchi yenye utawala wa sheria kumnyima mtu cheo kwa tuhuma ambayo haijathibitishwa. Huku sio kutenda haki. Ingawa tuhuma nyingi ni za kweli, lakini hii isiwe kigezo cha kuwanyima haki watu wachache ambao wanasingiziwa kwa sababu mbalimbali.

6. Kwanini kwenye hitimisho hawajawasema wanafunzi wanatoa rushwa ya ngono? Maana kutoa na kupokea rushwa ni kosa au kwenye ngono tu mkosaji ndio anakuwa mtoaji tu? Naamini mtoaji ni yule anayeshinikiza kupata au kutoa rushwa ya ngono ili apate ujira. Katika andiko lao, inaonesha mistari hiyo hapo chini ambapo mwanafunzi ndio anashinikiza kutoa

“……..kuna mwanafunzi alimuandikia mhadhiri wa somo barua pepe na kumuomba
amsaidie katika somo lake atamlipa chochote lakini sio pesa…….mhadhiri aliamua
kuwashirikisha wanafunzi wengine na baadhi ya wahadhiri idarani…….aliwaasa
wanafunzi wasome kwa bidii na kuzingatia maadili……”

“…….kuna mwanafunzi mmoja alikiri kosa la kumfanyia „Quiz‟ rafiki
yake……mwanafunzi aliyefanyiwa „Quiz‟ alimshawishi mhadhiri kingono baada ya
kubaini kuwa kosa walilofanya ni la kufukuzwa chuo…….mhadhiri huyo
hakushawishika na kuchukua hatua ya kumkabidhi mwanafunzi kwa mkuu wa
idara…….”

Je, TAKUKURU nao wawajibishwe kwa kufanya utafiti ambao haujaleta majibu ya kisayansi? Haya si matumizi mabaya ya fedha?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom