Utafiti Repoa kuhusu mtazamo wa wananchi juu ya mwenendo wa uchumi na umaskini waibua maswali

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
pic+repoa.jpg



Repoa ilizindua utafiti huo wa Afrobarometer unaoitwa “Mtazamo wa wananchi kuhusu uchumi na hali ya umaskini”, ikiwa ni awamu ya saba tangu ilipoanza kushiriki mwaka 2001 kwa kuwa sehemu ya nchi 36 za Afrika zinazofanya utafiti huo kwa lengo la kuangalia mtazamo wa wananchi katika masuala ya utawala, demokrasia, hali ya uchumi na umaskini.

Dar es Salaam. Wachumi kutoka vyuo vikuu na wadau wa taasisi za utafiti wameibua maswali katika matokeo ya utafiti wa Taasisi ya Repoa, yaliyoonyesha mtazamo wa Watanzania wengi kuridhishwa na mwelekeo wa Serikali katika kushughulikia masuala ya uchumi, ilhali wakati huohuo wanalia ukata.

Repoa ilizindua utafiti huo wa Afrobarometer unaoitwa “Mtazamo wa wananchi kuhusu uchumi na hali ya umaskini”, ikiwa ni awamu ya saba tangu ilipoanza kushiriki mwaka 2001 kwa kuwa sehemu ya nchi 36 za Afrika zinazofanya utafiti huo kwa lengo la kuangalia mtazamo wa wananchi katika masuala ya utawala, demokrasia, hali ya uchumi na umaskini.

Matokeo ya utafiti huo uliofanyika kati ya Aprili na Juni mwaka jana, yanaonyesha wananchi sita kati ya 10, waliohojiwa wanaamini nchi inakwenda katika njia sahihi, huku asilimia 42 wakisema hawapati huduma za maji safi na asilimia 76 wanalia hali ya ukata.

Mhadhiri mstaafu kutoka Shule ya Biashara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Richard Mushi alisema ni muhimu kuzingatia idadi ya sampuli iliyotumika na aina ya maswali yaliyoulizwa.

Dk Mushi alisema maswali yaliyoulizwa yalikuwa yanamfunga mwananchi asieleze sababu za kuonyesha mtazamo fulani, pengine angetakiwa kutoa majibu yangebadilika zaidi.

“Kuna umuhimu wa kuuliza swali la kwa nini, pengine ukimuuliza kwa undani anaweza kubadilisha direction (mwelekeo),” alisema.

Alipoulizwa uhusiano wa takwimu hizo na hoja ya ‘vyuma kukaza’ katika jamii, Dk Mushi alisema kundi lililokuwa likitegemea mkono wa Serikali kwenye biashara lazima litakuwa na mtazamo hasi katika utafiti huo.

Naye mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Saut), Profesa Mwesiga Baregu alikosoa matokeo hayo akisema utafiti umejikita zaidi kwenye mtazamo siyo uhalisia.

Baadaye mkurugenzi mkuu wa Repoa, Dk Donald Mmari alilieza gazeti hili kuwa inawezekana kujitokeza kwa mitazamo hiyo katika jamii kwa kuwa sampuli iliyotumika haikutakiwa kutoa sababu.

“Mtazamo huo unaweza kuwapo kwa sababu, pengine unaweza kuridhika na namna hali ya uchumi inavyokwenda, kwa mfano walipoulizwa unaonaje hali ya uchumi kwa siku zijazo wengi walikuwa na mtazamo chanya, kwa hiyo unaweza kuwa kwenye hali mbaya binafsi lakini ukawa na matumaini ya kushughulikiwa,” alisema Dk Mmari.

Chanzo: Mwananchi
 
Sisi CHADEMA na mwenyekiti wetu Mbowe, na wananchi tumesha ridhia Magufuli aongezewe mda
 
Isingeibua maswali ingekuwa kinyume chake. Siku ingine waje wafanye huu utafiti kwa sample ya JF!
 
Back
Top Bottom