Utafiti: Polisi endelea kuongoza kwa rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utafiti: Polisi endelea kuongoza kwa rushwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 19, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  Utafiti: Polisi endelea kuongoza kwa rushwa
  Tuesday, 18 January 2011 21:47

  [​IMG]Mkuu wa jeshi la Polisi Tanzania,IGP Said Mwema

  Hussein Issa na Tausi Kasamalo
  RIPOTI ya utafiti uliofanywa na Tasisi ya Wanaharakati wa Maendeleeo barani Afrika (ForDIA) inaonyesha kuwa Idara za Polisi, Afya na Mahakama bado ni vinara wa rushwa nchini.
  Kwa mujibu Fordia, polisi inaongoza kwa kupokea rushwa, huku sekta za Afya, Mahakama, Elimu, Tanesco na idara za leseni na ushuru zikitajwa pia kuwa na kiwango kikubwa cha rushwa.

  Akitangaza matokeo ya utafiti wa ForDIA jana ambao uliofanyika mwaka jana nchi nzima, Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Bubelwa Kaiza alisema “polisi ndio vinara wa rushwa kwa sasa”.

  Alisema utafiti huo unaonyesha kuwa polisi wanaongozwa kwa asilimia 81.9 kwa kupokea na kutoa rushwa. “Polisi imeendelea kushika nafasi ya kwanza baada ya kuongoza idara nyingine kwa kuwa na asilimia 85.3 mwaka jana kutoka nafasi ya pili ya asilimia 75.8 waliyokuwa wakiishikilia mwaka 2009,’’alisema Bubelwa alisema wakati polisi ikiongoza idara ya Mahakama inafuatia ikiwa na asilimia 79.85 ya rushwa huku sekta ya afya ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na asilimia 62.9.

  Alisema idara za ushuru na leseni zinafuatia kwa kuwa na asilimia 52.6 na Tanesco inafuatia likiwa na asilimia 49.4.

  Kwa mujibu wa Fordia utafiti huo ulifanyika katika mikoa 11 ya Tanzania ambayo ni Dar es salaam, Tanga, Kagera, Manyara, Rukwa, Tabora, Kilimanjaro, Mwanza, Mara, Pwani na Mtwara. Utafiti huo pia umejumuisha serikali za mitaa 47 katika wilaya tofauti nchini na kulishirikisha watu mbalimbali wapatao 1,122 ambao waliulizwa maswali, lengo likiwa kujua kinara wa rushwa nchini.

  Kati ya watu hao 1,122 waliohojiwa wanaume walikuwa 646 na wanawake 476. Hata hivyo watu walioweza kutoa majibu walikuwa 367, ambapo wanaume walikuwa 248 na wanawake 119, huku Bubelwa akieleza kuwa watu waliohojiwa ni wanaoishi mijini na vijijini.

  Alisema sula la umri lilizingatiwa katika kuwahoji watu ambapo, waliohojiwa wote walizidi miaka 18, hivyo utafiti huo kuhusisha vijana, wazee na watu wenye umri wa kawaida.

  Alifafanua kuwa walipata majibu na maoni mbali mbali kutoka kwa wananchi kuhusu suala la polisi ambapo walielezwa kuwa watu hukamatwa kwa uonevu na hulazimika kutoa 'kitu kidogo' (rushwa), ili waachiwe hata kama hawakuwa na makosa, ambapo pia watu wenye makosa wanapofikishwa polisi huachiwa baada ya muda mfupi kutokana na kutoa kitu kidogo.

  Kuhusu mahakama alieleza kuwa malalamiko ambayo Fordia iliyapata katika utafiti huo ni kesi kuchukua muda mrefu bila ya kusikilizwa, huku nyingine zikimalizika katika muda mfupi na nyingine kufutwa kabisa katika mazingira yenye utatanishi.

  Akizungumzia sekta ya elimu katika utafiti huo Buberwa alisema watu waliohojiwa walisema licha ya serikali kuondoa ada kwa wanafunzi wa shule za msingi, bado wazazi wanatozwa fedha nyingi, huku wanafunzi wanaoingia darasa la kwanza wakiandikishwa kwa malipo.

  Kuhusu Tanesco, alisema kwa wakazi wengi hasa wanaoishi vijijini hawana umeme ambapo walidai kwamba wakienda Tanesco kutaka kuwekewa umeme wanalazimika kutoa pesa, jambo ambalo limewarudisha nyuma kimaendeleo.

  Alisema tatizo hilo lilielezwa pia na wananchi wanaoishi mjini waliosema kuwa mtu hawezi kuwekewa umeme mpaka afahamike Tanesco au utoe kitu kidogo na kueleza pia kuwepo kwa shida ya upatikanaji umeme.

  Alisema lengo la utafiti huo ambao ulifanyika kwa nchi nzima ilikuwa ni kuanzisha majadiliano ili kuonyesha uelewa kwa wananchi na kuipa changamoto serikali juu ya mapambano ya rushwa.

  Alisema katika utafiti huo Fordia imebaini kuwa watu wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu rushwa, wala hawajui madhara yake.

  “ Katika vijiji tulivyotembelea watu hawafahamu maana ya rushwa na wengine hawaifahamu kabisa, kwani wao kutoa kitu kidogo ili wapatiwe huduma fulani kwao ni jambo la kawaida,”alisema Bubelwa. Alisema wamebaini kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) haipo vijijini, ndio sababu rushwa imekuwa ikiongezeka kwa kasi.

  Alisema watu wengi walioko vijijini wanahitaji kujua ni kwa nini Takukuru inafanya kazi mjini tu na wala sio vijijini ambako nako kuna watu wanaihusika na vitendo vya rushwa.


   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  Hawa polisi tunawajua huku mtaani hasara wanayotusababishia kwa kudai kitu kidogo..............................na hakuna wakuwafanya kitu...................
   
 3. CPU

  CPU JF Gold Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hii ndio moja ya section ambayo Hosea hawezi kabisa hata kuchungulia kwa nusu jicho.
  Nimemkumbuka Jerry Muro baada ya kusoma hii habari.
  Ila nategemea Polisi watajibu mapigo kwa kudai ni ripoti ya kipuuzi, isiyozingatia haya na yale. Watadai hawajashirikishwa pia
   
 4. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mbona PCCB ya Kenya inawakamata polisi bila shida?
  Kinachoshangaza report kama hii inawahusu TAKUKURU na utendaji wao moja kwa moja, lakini hawajitokezi kuzungumzia watakavyopambana namna ya kupunguza hilo tatizo. Kwa maoni yangu walitakiwa kwanza waishukuru taasis iliyofanya huo utafiti kwani imewarahisishia utendaji wao wa kazi
   
 5. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,957
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Kwani Ikulu na CCM vilikuwa kwenye hadidu za rejea za utafiti?
   
 6. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  suala la rushwa polisi si la kupuuza hata kidogo....IDARA YA UHAMIAJI nayo ilikuwa inanuka rushwa....lakini wamejirekebisha na niliwahi kuwapa pongezi....mbinu ileile iliyotumika KUPUNGUZA NA KUONDOA RUSHWA UHAMIAJI INGEWEZA KUTUMIKA PIA POLISI NA KULETA MAFANIKIO MAKUBWA.....
  nikiwa muathirika mkubwa wa RUSHWA jeshi la polisi hasa kitengo cha usalama barabarani (TRAFFICK) katika shughuli zangu za kila siku imenilazima kuacha/kupumzika hasa kipindi hiki cha watoto kwenda shule kwani utakamuliwa mpaka senti ya mwisho
   
Loading...