Utafiti: Pata muda wa kutosha kulala kujikinga na corona

Sam Gidori

Verified Member
Sep 7, 2020
93
150
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, watafiti wameonesha kuwapo uhusiano baina ya maambukizi ya corona na usingizi.

Utafiti uliofanyika awali ulionesha kuwa asilimia 40 ya watu waliopata maambukizi ya virusi vya corona walikuwa na matatizo ya kupata usingizi. Utafiti mpya unaonesha kuwa watu wenye matatizo ya ukosefu wa usingizi au wanaochoka sana kutokana na kazi wapo si tu katika hatari kubwa ya kupata maambukizi, bali kuthiriwa zaidi na virusi vya corona.

Kila saa moja iliyoongezeka katika muda wa kulala iliongeza uwezekano wa kuepuka maambukizi ya virusi vya corona kwa asilimia 12, kwa mujibu wa utafiti huo uliochapishwa katika jarida la mtandaoni la BMJ Nutrition Prevention & Health. Utafiti huo ulifanyika katika nchi za 6 za Ulaya na Marekani kuanzia Julai hadi Septemba mwaka 2020 na ulihusisha watu 2,884 ambapo 568 kati yao walikutwa na maambukizi.

Washiriki wa utafiti huu walipata wastani wa saa 6 hadi 7 za kulala. 1 kati ya 4 ya wale walioambukizwa COVID-19 waliripoti changamoto ya usingizi ukilinganisha na 1 kati ya 5 ya wale ambao hawajaambukizwa.

Waliokuwa na changamoto za usingizi walikuwa na hatari ya kupata maambukizi kwa asilimia 88 tofauti na hatari ya asilimia 3 tu kwa wale waliokuwa wakipata usingizi wa kutosha, na kwa wale wanaochoka sana baada ya kutoka kazini walikuwa wakiathiriwa na maambukizi ya corona mara tatu zaidi na walitumia muda mrefu kupona baada ya kuambukizwa.

Watafiti hao hawakuweza kutoa sababu za moja kwa moja kuhusu ukosefu wa usingizi (insomnia) na maambukizi ya virusi vya corona, lakini dhanio ni kuwa kukosa usingizi hushusha uwezo wa kinga ya mwili kupambana na magonjwa.

Hivyo, kwa lugha rahisi, ili kujiweka katika mazingira salama ya mwili wako kupambana na maambukizi ya virusi vya corona, unapaswa kupata muda wa kutosha kulala.

Chanzo: HuffPost
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
7,759
2,000
Ikiwa huo utafiti umetazama nchi za kiafrika kama hapa Tanzania basi wengi watakufa/wangekufa, waafrika wako tight na shughuli za kuutafuta 🍞 wa kila siku na kula yao inatokana na kazi ya siku husika.

Kutokana na hilo muda wa kulala ni mchache sana, unakuta mtu anauza bidhaa barabarani, anapanga saa 1asbh na kufunga saa 4:30usk akifunga na kufika home mpaka kukitafuta kitanda sasa...
 

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
11,797
2,000
Hapa naona ndio mwanzo wa kupotea ule uzi wetu pendwa wa JF USIKU WA MANANE.
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,221
2,000
Hawa makuli masokoni, wasukuma mikokoteni Bongo na wabeba zege basi wangepukutika.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom