Utafiti: Paracetamol yaathiri uwezo wa kuzalisha

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
Paracetamol yaathiri uwezo wa kuzalisha.jpg
Utafiti umebaini kuwa matumizi ya Paracetamol kwa siku 7 unapunguza uzalishaji wa homoni za kiume na uwezo wa watoto mvulana kuzalisha baadaye.

Wanawake wajawazito wanapaswa kutahadhari zaidi wanapotumia dawa zozote zilizo na chembechembe za Paracetamol.
Utafiti wa Wanasayansi nchini Uingereza umebaini kuwa unywaji wa dawa zenye kiungo cha Paracetamol kwa kipindi cha siku saba unapunguza uwezo wa uzalishaji wa homoni za kiume ''testosterone''.

Homoni hiyo ''testosterone'' ndio inayowezesha kuumbwa kwa sehemu ya uzazi wa kiume. Sasa madaktari wanashauriwa wasipeane dawa zenye ''Paracetamol'' kwa wanawake waja wazito kiholela. Na iwapo itawalazimu kupeana dawa hizo basi wanashauriwa kupeana dawa hizo kwa kipindi kifupi ilikupunguza madhara kwa watoto waliotumboni.

Halmashauri inayosimamia matumizi ya madawa nchini Uingereza sasa inasema licha ya kuwa inahujumu kiumbe kilichoko tumboni, Paracetamol ni moja kati ya madawa yenye madhara machache zaidi kwa mama mja mzito na mwanawe.

Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa onyo kutolewa dhidi ya wanawake wajawazito kupewa dawa zilizo na kiuongo cha Paracetamol.
Awali utafiti wa wanawake waja wazito 2,000, nchini Denmark ulibaini kuwa,wanawake waliomeza dawa za Paracetamol walijifungua watoto waliolemaa katika sehemu ya mfuko wa uzazi- korodani. Ulemavu huo hatimaye ulijitokeza na kuwa upungufu wa uwezo wao kuzalisha katika maisha yao ya utu uzima.

141119131932__paracetamol_tablets_640x360_getty_nocredit.jpg
Paracetamol yaathiri uwezo wa kuzalisha:Utafiti
Aidha inasemekana kuwa wanawake wanaotumia dawa hiyo ya kupunguza maumivu kwa kipindi kirefu wakati wa ujauzito, wanaweza kuathiri mimba zao na hasa kwa watoto mvulana.

Wanasayansi hao wa Chuo kikuu cha Edinburgh, walitumia panya katika utafiti huo. Shirika linalosimamia maswala ya afya Nchini Uingereza, linasema kuwa wanawake waja wazito wanafaa kumeza tembe hiyo ya paracetamol ikiwa tu wameshauriwa na daktari na pia kwa kipindi kifupi mno.

Dakta Dr Rod Mitchell, aliyeongza utafiti huo anasema kuwa tahadhari kubwa inapaswa kuwekwa inapowadia swala la matumizi ya Paracetamol miongoni mwa wanawake waja wazito.

''utafiti huu unatilia pondo ushauri tuliokuwa nao tayari kuwa chembechembe za dawa hiyo zinaathiri ukuawaji wa sehemu za kiume za watoto wavulana''.

Utafiti huo ulifaulu baada ya madaktari kuwapasua panya na kuwapandikiza mimba na kisha wakawapa dawa hiyo kwa siku saba.
Walipoipima iwapo ilikuwa na chembechembe za homoni hiyo ya kiume waligundua kuwa haikuwa nayo.

Hata hivyo walipoipima baada ya siku moja hawakuona tofauti ya viwango ya homoni hiyo muhimu kwa wanaume.

Watafiti hao hata hivyo wanasema ni vigumu kufikia sasa kubaini iwapo athari hiyo ni sawa sawa...jpg
Watafiti hao hata hivyo wanasema ni vigumu kufikia sasa kubaini iwapo athari hiyo ni sawa sawa miongoni mwa wanadamu.
Watafiti hao hata hivyo wanasema ni vigumu kufikia sasa kubaini iwapo athari hiyo ni sawa sawa miongoni mwa wanadamu.
Hilo linatokana na sheria kali zinazozuia utafiti wa aina hiyo.

Licha ya utafiti huu msemaji wa chuo cha afya ya watoto nchini Uingereza Dr Martin Ward-Platt, anaonya kuwa wanadamu hawapaswi kukatazwa kabisa kumeza dawa zilizo na Paracetamol kwa sababu zinasaidia sana kutibu mafua ya mara kwa mara na wakati mwengi kipimo kimoja au viwili vya Paracetamol vinatosha kutibu homa.

Daktari Sadaf Ghaem-Maghami, kwa upande wake ameonya kuwa utafiti huo haupaswi kukubalika pasi na maswali muhimu kuulizwa kuhusu ukweli wake.

''Licha ya kuwa matokeo ya utafiti huu ni mzuri na unavutia ,tunapaswa kufanya utafiti zaidi kwa sababu utafiti huu ulifanyiwa wanyama, Je mwili wa binadamu utaitikia vipimo vya dawa hii kwa njia sawa na hiyo ? alihoji dakta Sadaf.

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la kisayansi na utabibu '' Translational Medicine''.

Source: BBC
 
Side Effects of Long Term Paracetamol or Panadol Use



PANADOL.jpg



Paracetamol side effects

Use with caution in

* Decreased kidney function.

* Decreased liver function.


Paracetamol side effects


Get emergency medical help if you have any of these signs of an allergic reaction to paracetamol: hives; difficulty breathing; swelling of your face, lips, tongue, or throat. Stop using this medication and call your doctor at once if you have a serious side effect such as:

  • low fever with nausea, stomach pain, and loss of appetite;
  • dark urine, clay-colored stools; or
  • jaundice (yellowing of the skin or eyes).
This is not a complete list of paracetamol side effects and others may occur. Call your doctor for medical advice about side effects. You may report side effects to FDA at 1-800-FDA-1088.

Paracetamol Side Effects
  • Managing Side Effects
Note: This document contains side effect information about acetaminophen. Some of the dosage forms listed on this page may not apply to the brand name Paracetamol.


For the Consumer
Applies to acetaminophen: capsule, capsule liquid filled, elixir, liquid, powder, solution, suppository, suspension, syrup, tablet, tablet chewable, tablet disintegrating, tablet extended release

Other dosage forms:

  • intravenous solution
Side effects requiring immediate medical attention
Along with its needed effects, acetaminophen (the active ingredient contained in Paracetamol) may cause some unwanted effects. Although not all of these side effects may occur, if they do occur they may need medical attention.

Check with your doctor immediately if any of the following side effects occur while taking acetaminophen:

Rare

  • Bloody or black, tarry stools
  • bloody or cloudy urine
  • fever with or without chills (not present before treatment and not caused by the condition being treated)
  • pain in the lower back and/or side (severe and/or sharp)
  • pinpoint red spots on the skin
  • skin rash, hives, or itching
  • sore throat (not present before treatment and not caused by the condition being treated)
  • sores, ulcers, or white spots on the lips or in the mouth
  • sudden decrease in the amount of urine
  • unusual bleeding or bruising
  • unusual tiredness or weakness
  • yellow eyes or skin
Get emergency help immediately if any of the following symptoms of overdose occur while taking acetaminophen:

Symptoms of overdose


  • Diarrhea
  • increased sweating
  • loss of appetite
  • nausea or vomiting
  • stomach cramps or pain
  • swelling, pain, or tenderness in the upper abdomen or stomach area

Paracetamol Side Effects: Common, Severe, Long Term - Drugs.com


Ukitumia Vidonge hivyo yaani Paracetamol au Panadol kwa muda mrefu basi ukae ukijuwa unaharibu Figo lako na Ini lako kupunguwa kufanya kazi vizuri Tujihadhari kutumia kwa wingi hivyo vidonge.

Cc. MziziMkavu 2013
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom