Utafiti: Mambo ambayo watu wengi huzungumza dakika chache kabla ya kifo

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,316
50,522
Kulikuwa na mwanfunzi mmoja wa uchungaji ambaye alianza kufanyakazi katika Hospitali ya watu wenye saratani, siku moja akakutana na Profesa wake aliyekuwa akimfundisha na kumuuliza anaonaje kazi yake kwa muda ambao amekuwa hapo hosptalini?

Mwanafunzi yule wa uchungaji aliyekuwa na mika 26 alimwambia Profesa kuwa hutumia muda wake kuzungumza na wagonjwa na mara nyingi huzungumza nao kuhusu familia zao. Alipoulizwa kama huzungumza nao kuhusu dini, Mungu, maana ya miasha, maombi alisema hapa na kuwa wao huzungumza kuhusu familia basi.

Wiki moja baadae Profesa alisimulia mkasa ule darasa ambapo wanafunzi wengine walicheka na kufanya mwanafunzi yule kujiona mnyonge sana na mkosaji.

Miaka 13 baadae bado anawatembelea wagonjwa na kuwahudumia na anaeleza kuwa kama utaulizwa swali kuhusu kazi yake, bila woga wala kupepesa macho atajibu kuwa huzungumza na watu waliopo mahututi kuhusu familia zao.

Kerry Egan anaeleza kuwa muda wake ambao amekuwa akiwa karibu na watu ambao wengi huwa na muda mfupi wa kuishi, wanapenda kuzungumza kuhusu familia zao, watoto wao, baba na mama zao.

Watu hao zaidi hupenda kuzungumzia upendo waliouonyesha kwa ndugu, jamaa na rafiki zao, upendo ambao hawakuuupata au hawakujua namna ya kuwapenda baadhi ya watu. Huzungumza juu ya upendo ni nini hasa, na jinsi unavyotakiwa kumpenda mwenzako.

Aidha, alieleza kuwa wagonjwa wanapokaribia kufariki, wengi hunyoosha mikono kana kwamba wanataka kushika kitu kisichoonekana huku wakiita majina ya baba na mama zao.

Akielezea kwanini angetoa jibu lile lile kama Profesa angemuuliza tena, angejibu ni kwa sababu watu huzungumza kuhusu familia zao wanapokuwa na wachungaji kama vile ambavyo wao huzungumza na Mungu kuhusu maisha yao. Maisha yetu yamefungamana kwenye familia tulikozaliwa, tuliko lelewa na kila kitu chetu kufanyikia huko.

Watu huzungumzia familia zao kwa sababu katika familia ndio sehemu ya kwanza tunajifunza kuhusu kupenda na kupendwa, mambo mengi kwa mara ya kwanza tunajifunza katika familia, hata kuumizwa na anayekupenda kwa mara ya kwanza hutokea katika familia. Ndipo tunajifunza kuwajali wale wasiona uwezo.

Kama Mungu ni upendo, na tunaamini hilo kuwa ni kweli, basi tunajifunza kuhusu Mungu tunapojifunza kupenda. Darasa pekee linalofundisha upendo katika maisha yetu ni familia, alisema Kerry
 
So sad! Inasikitisha sana kuhusu kifo! Wangapi tulikua nao lakini Leo hawapo wametangulia.

Hapa ndio unaona jinsi tamko la Mungu linavyotimia "hakika utakufa" wewe ni mavumbi, na mavumbini utarudi!

Lakini asante Yesu Kwa kuniokoa, ijapo nitakufa kitambo kidogo, lakini nitaishi.
 
Back
Top Bottom