Utafiti: Mabadiliko ya vimelea vyenye usugu dhidi ya dawa ndiyo chanzo cha ugonjwa wa Malaria kuendelea kuenea Afrika

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Watafiti leo Alhamisi wametoa ripoti kuhusu ushahidi wa kwanza wa kidaktari kwamba mabadiliko ya vimelea vyenye usugu dhidi ya dawa ndiyo chanzo cha ugonjwa wa Malaria kuendelea kuenea barani Afrika.

Wataalamu wa dawa wamekuwa na wasiwasi kwa muda mrefu kuhusu kuibuka kwa tatozo la usugu dhidi ya dawa za kutibu Malaria barani Afrika, hali ambayo ilisababisha asilimia 90 ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo duniani kote kwa mwaka 2019

Utafiti uliochapishwa na jarida la kitabibu la Lancet unathibitisha wasiwasi huo. Katika majaribio ya kimatibabu, utafiti ulionesha kuwa Malaria ilionekana kudumu zaidi kwa watoto waliokuwa wakipokea matibabu ya kawaida kama walikuwa wameathiriwa na vimelea vipya vya Malaria.

Ufanisi wa mchanganyiko wa dawa za Artemisinin ulikuwa mkubwa, lakini watafiti wanasema kuna haja kubwa ya ufuatiliaji zaidi nchini Rwanda ulikofanyika utafiti pamoja na mataifa jirani.

Dawa hii hufanya kazi kuondoa vimelea vya Malaria katika mwili wa mgonjwa ndani ya siku tatu na hutumiwa pamoja na dawa nyingine mshirika inayoondoa kabisa vimelea vilivyosalia.

Katika majaribio, zaidi ya watoto 200 wa umri wa miezi sita hadi miaka mitano walioathiriwa na Malaria walipata matibabu ya siku tatu yaliyozoeleka na walikuwa chini ya uangalizi wa siku 28. Asilimia 15 kati ya hao waliendelea kuugua Malaria.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, kuna takribani visa milioni 229 vya Malaria duniani kote. Ugonjwa huo uliwaua zaidi ya watu 400,000 mwaka 2019 huku theluthi mbili ya hao wakiwa ni watoto.


DW
 
Back
Top Bottom