Utafiti: Joto la laptop linaunguza korodani na hivyo kuharibu rutuba ya mbegu za kium | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utafiti: Joto la laptop linaunguza korodani na hivyo kuharibu rutuba ya mbegu za kium

Discussion in 'JF Doctor' started by Baba Mtu, Nov 29, 2010.

 1. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  UTAFITI: JOTO LA LAPTOP LINAUNGUZA KORODANI NA HIVYO KUHARIBU RUTUBA YA MBEGU ZA KIUME. Posted: 19 Nov 2010 08:19 PM PST
  [​IMG]

  § Je, wewe ni mwanaume? Unayo tabia ya kutumia laptop yako ikiwa mapajani mwako? Pengine itabidi uache tabia hiyo mara moja kwani unaweza ukawa unaangamiza kizazi kijacho.
  § Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la Fertility and Sterility (Elsevier) unaonyesha kwamba joto la laptop ni hatari kwa sababu linaunguza korodani na hatimaye kuharibu na hata kuangamiza kabisa mbegu za kiume. Joto hilo limetajwa kuwa sababu mojawapo inayosababisha kuongezeka kwa utasa katika nchi zilizoendelea.
  § Mbegu za kiume zilizoathiriwa na joto la laptop hazina vichwa, hazina mikia na zingine zina mikia mifupi; na kwa hivyo haziwezi kuogoelea na kulifikia yai la mwanamke ili kuweza kulirutubisha. Kwa ujumla, joto la laptop linaweza kusababisha utasa wa kudumu kwa wanaume.
  [​IMG]
  Ni mwogeleaji mmoja tu hodari ndiye atashinda hapa...
  § Ushauri wa watalaamu: Kama ni lazima uweke laptop yako mapajani, basi panua miguu yako. Hii inasaidia korodani zisiunguzwe na joto la laptop kwa haraka. Njia ya uhakika zaidi ni kutumia dawati au meza kila unapotumia laptop. Utafiti huu unapatikana hapa: http://www.alligator.org/news/local/article_cd027a6c-f06d-11df-8e00-001cc4c03286.html na hapa: http://www.bionews.org.uk/page_82478.asp au hapa:

  CHANZO:
  http://matondo.blogspot.com/2010/11/utafiti-joto-la-laptop-linaunguza.html?utm_source=feedburner&utm_medium=email&utm_campaign=Feed%3A+matondo+%28Dr.+Matondo%29&utm_content=Yahoo!+Mail

   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  I agree with you
  kuna effect kubwa mimi nimeacha kuweka laptop mapajani
   
 3. mchakachuaji192

  mchakachuaji192 JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  thanks mkulu kwa ujumbe huu umeokoa wengi,
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nashukuru kwa habari muhimu sana!!
   
Loading...