Utafiti: Joto huchangia watu kufeli mitihani

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,251
Utafiti uliofanywa ni watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Harvard na vyuo vingine vikuu vya Marekani kuna uhusiano wa "kuaminika" kati ya viwango vya juu vya joto na mafanikio ya shuleni.

Vipimo vya uchanganuzi wa alama miongoni mwa wanafunzi wa shule za sekondari milioni 10 vilivyochukuliwa katika kipindi cha miaka 13 ya joto vinaonyesha kuwa majira ya joto yana athari hasi kwa matokeo ya shule.

Utafiti huo unasema labda njia ya kukabiliana na athari hiyo inaweza kuwa ni kutumia viyoyozi zaidi.

Wanafunzi wanaofanya mitihani wakati wa majira ya joto wamekuwa wakilalamika kuwa wanasumbuliwa na joto.

Lakini utafiti huu kutoka kwa wasomi wa Chuo Kikuu cha Harvard, Chuo kikuu cha California Los Angeles (UCLA) na kile cha kitaifa cha Georgia wanadai kuwa wamepata ushahidi wa wazi unaoonyesha kwamba wakati kunapokuwa na joto matokeo ya mitihani ya shule hushuka

Wimbi la joto
Utafiti uliochapishwa na taasisi ya uchunguzi wa kiuchumi nchini Marekani, ulibaini kuwa wanafunzi walikuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na alama za chini wakati wa miaka ya joto na matokeo mazuri wakati wa miaka yenye vipindi vya baridi.

Matokeo haya yalikuwa sawia katika maeneo yenye tabia nchi tofauti - iwe ni kwa majimbo yenye baridi zaidi ya kaskazini mwa Marekani au majimbo yenye vipimo vya juu vya joto ya kusini mwa Marekani, joto lilionekana kuathiri matokeo ya mitihani shuleni.

Utafiti huo kuhusu Joto na Masomo, unasema kwamba hali ya hewa ya joto huwafanya wanafunzi washindwe kujifunza na kuwa makini wanapofanya kazi wanazopewa shule wazifanyie nyumbani.,

Utafiti huo umebaini pia kuwepo kwa athari za hali ya hewa ya joto katika uchumi wa familia zenye kipato cha chini na wanafunzi wanaotoka katika jamii za walio wachache.

Kulikuwa na madai kwamba familia tajiri zaidi na shule katika maeneo ya watu wenye kipato cha chini waliweza kuingilia kati pale walipoona watoto wanalala darasani na kutafuta muda mbadala wa kuwapatia masomo ya ziada baada ya shule.

Chanzo: BBC Swahili
 
Dah, ni kweli kabisa hata mm naunga mkono mkuu. Hata mm nime experience hicho kitu hii sababu niko dar lkn si kwamba nlikua na matokeo mabaya HAPANA, bali ningekuwa mikoa ya baridi nahisi ningepata zaidi ya nilichopata.

Kwakweli hali ya ubaridi ina infuence mtu kuwa active kuliko kipindi cha joto. Ukichukulia hata watu wanaposoma usiku then kukawa na joto huwa linawakera na kuwapunguzia concentration but kukiwa na hali ya baridi mwanafunzi anakuwa concentrate na kile akifanyacho na pia haichoshi mwili.

But cha kumalizia ni kwamba hata baridi pia likiwa kali linaathiri pia.
TOO MUCH IS HARMFUL.
Nawasilisha.
 
Wazungu muda mwingine wana tafiti za kitoto.

Waafrika tunazipapatikia/shobokea kishenzi.
 
Wazungu muda mwingine wana tafiti za kitoto.

Waafrika tunazipapatikia/shobokea kishenzi.
Kwani Uongo!?.
Sehemu zote za Joto kubwa kama Africa na Australia hakuna maendeleo!. Uarabuni napo mambo ni yale yale with Exception za Foreign people kwenye maeneo hayo!.
Turudi tu kwenye Maisha ya kila siku, kukiwa na kazi halafu kuna joto na kukiwa na Kazi halafu kuna Baridi wapi unafanya sana kazi bila bughudha wala hasira!?.
Kwenye Baridi maendeleo yote yanapatikana hata viwanda vya watoto vipo vingi maeneo ya baridi!.
 
Si binadamu tu hata mashine huwa na efficiency kubwa maeneo ya baridi compare na maeneo ya joto
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom