Utafiti: Je, ni umri gani sahihi wa mtu kuitwa mzee?

waterproof

JF-Expert Member
Aug 14, 2020
347
500
Kutoka wikipedia, Mzee ni mtu aliyeishi miaka mingi baada ya kuzaliwa.Katika jamii za Kiafrika, sawa na jamii nyingi duniani, neno “mzee” linatumiwa pia kama cheo cha heshima kwa kumtaja mtu mwenye mamlaka fulani. Hapo kuna hoja ya kuwa mtu aliyeendelea katika umri anawazidi vijana kwa hekima na maarifa pia, kwa hiyo anafaa kutawala au kufanya maazimio au angalau kutoa ushauri.

Happymark kutoka Mabibo Dar es salaam, Alieleza kuwa, Mzee ni binadamu yeyote mwanaume au mwanamke mwenye umri zaidi ya miaka 55, mwanadamu huyu anapofika kipindi hiki anapunguza uwezo wake wa kufanya mambo kwa ufanisi kama alipokuwa anafanya alipokuwa na umri wa ujana,ndio maana hata kisheria mtu anapofikia umri huo hushauriwa kustaafu,mzee ana chagamoto nyingi za kimaisha kuanzia namna ya kufikiri na kufanya maamuzi lakini pia hata kujitimizia mahitaji binafsi, Wazee wanahitaji kusaidiwa maana peke yao hawawezi

Isak kutoka Mikocheni, Dar es salaam alielezea, Uzee ni hali ya mtu kuishi miaka mingi na kuanza kupoteza nguvu na uwezo aliokuwa nao katika hali ya kawaida . Uzee huambatana na udhaifu wa kimwili ambapo mwili hushambuliwa na magonjwa ya mara kwa mara kutokana na kinga zake kupoteza uwezo na kuanza kushambuliwa.

Mawa Gorge,kutoka Southen Sudan alisema yafuatayo, Elderly people in South Sudan have both physical and mental characteristics that distinguish them from the young ones. Mentally, their reasoning capacity lowers, Some start talking alone.While physically, their body appearance changes (skin, eyes, etc). Difficulties in walking and working and their strength lowers and Also their regenerative ability gets down. This can be biologically (They can’t give birth anymore)

Edmund, kutoka Kigamboni, Dar es salaam, alieleza.

Najua kuna majibu tofauti zaidi ya haya kwa sababu kila MTU na mtazamo wake,naomba kuwasilisha.
 

waterproof

JF-Expert Member
Aug 14, 2020
347
500
Kiutaratibu huo ndio umri sahihi wa mtu kuitwa mzee na ndio maana hata kustaafu kazi wengi wanastaafu wakiwa kwenye umri huo. Sasa kama mtu hataki huwezi mlazimisha ila kiuhalisia anakuwa tayari mzee
Safi mzee baba umetiririka kinaga ubaga
 

mgen

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
19,659
2,000
Uzee au ujana kweli upo!
Ila nafasi hizo unajiweka mwenyewe!
Kuna watu wana umri mkubwa wanajiweka soap soap huwezi ukaami ana umri mkubwa!
Na kuna wenye umri mdogo anajiacha utafikiri ana umri mkubwa!
 

waterproof

JF-Expert Member
Aug 14, 2020
347
500
Uzee au ujana kweli upo!
Ila nafasi hizo unajiweka mwenyewe!
Kuna watu wana umri mkubwa wanajiweka soap soap huwezi ukaami ana umri mkubwa!
Na kuna wenye umri mdogo anajiacha utafikiri ana umri mkubwa!
Kwanza lazma tutambue ni umri gani sahihi wa kua mzee bila kujali upo katika hali gani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom