Utafiti: Inaripotiwa kuwa vifo zaidi ya 7,000 hutokana na miandiko mibaya ya Madaktari

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,730
10,033
Kulingana na tafiti ya the Institute of Medicine (IOM)- 2006, majeruhi 1.5 million kila mwaka hutokana na wafamasia, waudumu wa afya kushindwa kusoma maandiko ya madaktari. Vifo zaidi ya 7000 hutokana na mgonjwa kupatiwa dawa isiyo sahihi tofauti na maelezo ya madaktari.

14.jpg

Muda mwingine hata madaktari wenyewe hushindwa kusoma nini wameandika kwenye maandiko yao wenyewe, hata hivyo sababu kubwa ya kuwa na miamdiko hiyo ni kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaotakiwa kuonwa kwa muda mchache, notes na prescription zinazotakiwa kuandikwa kwa muda mfupi.
 
Binafsi huwa wananikera sana, kwa nini wasiandike tu maneno yanayosomeka vizuri? Hiyo Sababu hata sikubaliani nayo, hakuna Cha wagonjwa wengi Wala nini ni upumbavu tu hasa hawa wa kwetu Afrika.
 
Mkuu, inasemekana watu wenye muandiko mbya wana akili sana. Wanafikiri zaidi ya kuandika.

Madokta wengi huchagukiwa kutokana na kuwa na akili nyingi.

Hata wanasaysnsi wengi hawana mwandiko mzuri wala mpangilio wa kuandika ubaoni.

Watu wa art wengi wana mwandiko mzuri, ila kichwani sio smart sana kama wanasayansi(fact).
 
Kulingana na tafiti ya the Institute of Medicine (IOM)- 2006, majeruhi 1.5 million kila mwaka hutokana na wafamasia ,waudumu wa afya kushindwa kusoma maandiko ya madaktari. Vifo zaidi ya 7000 hutokana na mgonjwa kupatiwa dawa isiyo sahihi tofauti na maelezo ya madaktari.View attachment 1790219
Muda mwingine hata madaktari wenyewe hushindwa kusoma nini wameandika kwenye maandiko yao wenyewe, hata hivyo sababu kubwa ya kuwa na miamdiko hiyo ni kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaotakiwa kuonwa kwa muda mchache, notes na prescription zinazotakiwa kuandikwa kwa muda mfupi.
Siku hizi ni computerized
 
Dokta unakuta amecharanga charanga havisomeki umafika kwa pharmacist unampa anasoma anajifanya kaelewa anakupa dawa kameze kutwa mara 6.

Huna jinsi, unakubali tu unasepa.
 
Kuna mmoja alikuwa anagombania mwanamke na dakitari mwenzake aliyekuwa na pharmacy binafsi, siku moja akamwabia mwanamke yule jamaa (Mwenzake mwenye pharmacy) hata kusoma hajui, kama huamini kesho mpelekee cheti hiki akupe dawa uone kama ataweza kusoma, akachorachora hicho cheti yule mwanamke akapeleka, yule mwenye pharmacy akasoma akampa dawa yule mwanamke, akarudi kwa yule dakitari kumwonyesha dawa alizopewa, akamwambia"unaona kuna dawa nyingine hapo hajaziona nilikuambia hajui kusoma mimi nikiandika ni watu wachache sana hapa mjini wanaoweza kusoma"
 
Natakiwa ku attend wagonjwa 30 kwenye foleni alaf nirembe mwandiko kweli?

Na kwenye emergency napo nirembe mwandiko?

Kuna kama code zinatumika ambazo zinaeleweka na health care providers wote ni vitu vichache sana huitaji clarification kama mtu hajaelewa.
 
Naomba yeyote aandike tena hayo maandishi, mimi nimeona ni uchafu. Lakini kwanini ufanyie kazi kitu ambacho ujakielewa? that is also foolishness
 
FB_IMG_16445611424920652.jpg

Naomba niseme, daktari kuandika muandiko wa mchararango sio kipimo cha IQ kubwa wala akili nyingi ni upuuzi tu uliokutwa na kuendelezwa.

Watu wanapewa dawa zisizo zenyewe kwa kushindwa kusoma hii miandiko, nimeshuhudia sana wauzaji wa maduka ya madawa wanatoa dawa zisizo kwasababu ya kushindwa kusoma hii miandiko.

Mimi nipo pia kwenye sekta ya afya nashuhudia wauzaji wengi wa maduka ya dawa wanakimbiliaga kwenye magrouP ya WhatsApp kuomba msaada wa kusomewa dawa iliyoandikwa na daktari.

Hakuna sehemu yoyote kwenye mtaala wa madaktari wamefundishwa waandike hvyo majina ya dawa, huu ni usumbufu na kufanya watu wanaenda maduka ya dawa wanapewa dawa tofauti.

Wengine huwa tunawapa dawa tunazojua sisi, nikishindwa kusoma miandiko naangalia diagnosis ni ugonjwa gani nampa dawa ninazojua mimi.

Kwanini kwenye ripoti zenu na muwapo shule hamuandiki huo ujinga?

Naomba serikali ipige marufuku hili swala kwani wagonjwa wengi waendapo maduka ya dawa hupewa kitu tofauti na kilichoandikwa

Wizara ya Afya Tanzania
 
Kulingana na tafiti ya the Institute of Medicine (IOM)- 2006, majeruhi 1.5 million kila mwaka hutokana na wafamasia ,waudumu wa afya kushindwa kusoma maandiko ya madaktari. Vifo zaidi ya 7000 hutokana na mgonjwa kupatiwa dawa isiyo sahihi tofauti na maelezo ya madaktari.View attachment 1790219
Muda mwingine hata madaktari wenyewe hushindwa kusoma nini wameandika kwenye maandiko yao wenyewe, hata hivyo sababu kubwa ya kuwa na miamdiko hiyo ni kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaotakiwa kuonwa kwa muda mchache, notes na prescription zinazotakiwa kuandikwa kwa muda mfupi.

Ni kweli hizi mentality zipo, hasa kwenye mazingira ya utoaji huduma pale mtoa huduma hujiona yeye ni kila kitu na mhudumiwa hufika na kuji-subject/kuwa chini ya maamuzi ya mtoa huduma kwa asilimia 100.

Lakini nadhani hatujui ni kwa kiasi gani hili lina athiri ubora na matokeo ya huduma tunazotoa.
Hata taratibu kwa ujumla hazielekezi hivyo.

Ukielewa uzito wa tatizo hili, huwezi kufanya hivyo. Na ni muhimu kufahamu kuwa:

1: Ni vyema mgonjwa kuelewa kila aina ya dawa aliyoandikiwa na jinsi atakavyoitumia na kwa muda gani.

2: Mabadiliko anayoweza kuyapata wakati anatumia dawa.

3: Nini afanye anapotumia dawa na hali haiendelei vyema, maana kuna watu wakipata dawa wao huona ni mpaka dawa ziishe huku hali inaenda ndivyo sivyo.

4: Tumia au usitumie hiki wakati unatumia tiba hii.

5: ......

Hii itasaidi matumizi sahihi ya dawa na matokeo chanya zaidi. Tunaweza kusema ni sehemu ya wafamasia, lakini tunawajibika kwa hili.

Ila wagonjwa nanyi muache hiyo mentality/syndrome, kwani utasikia "dokta kwa mwandiko huu hukutakiwa kuwa daktari, labda mwalimu, mhasibu", "sijawahi kuona dokta anaandika hivi"
 
View attachment 2115633

Naomba niseme, daktari kuandika muandiko wa mchararango sio kipimo cha IQ kubwa wala akili nyingi ni upuuzi tu uliokutwa na kuendelezwa.

Watu wanapewa dawa zisizo zenyewe kwa kushindwa kusoma hii miandiko, nimeshuhudia sana wauzaji wa maduka ya madawa wanatoa dawa zisizo kwasababu ya kushindwa kusoma hii miandiko.

Mimi nipo pia kwenye sekta ya afya nashuhudia wauzaji wengi wa maduka ya dawa wanakimbiliaga kwenye magrouP ya WhatsApp kuomba msaada wa kusomewa dawa iliyoandikwa na daktari.

Hakuna sehemu yoyote kwenye mtaala wa madaktari wamefundishwa waandike hvyo majina ya dawa, huu ni usumbufu na kufanya watu wanaenda maduka ya dawa wanapewa dawa tofauti.

Wengine huwa tunawapa dawa tunazojua sisi, nikishindwa kusoma miandiko naangalia diagnosis ni ugonjwa gani nampa dawa ninazojua mimi.

Kwanini kwenye ripoti zenu na muwapo shule hamuandiki huo ujinga?

Naomba serikali ipige marufuku hili swala kwani wagonjwa wengi waendapo maduka ya dawa hupewa kitu tofauti na kilichoandikwa
Duh !
 
Wale jamaa watakuja waseme, ^Ndiyo maana tunahitaji Car-teabar Mpya!^

#Not all doctors, pls. Heshimuni sana sekta ya afya!!!
 
Back
Top Bottom