Utafiti Dar: 85% ya Vijana wa Kiume wanaishi kwa kipato cha chini

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,021
1,609
Utafiti wa Repoa uliofanyika Kati ya Machi na Aprili 2021 unasema 85% ya Vijana wa Kiume wenye chini ya Miaka 35 wanaishi kwa kipato cha chini ya Tsh. 300,000, huku wa Kipato cha kati wakiwa 13% na uwezo wa kupata Tsh. 300,000 hadi Tsh. 1,300,000 na 2% pekee ndio wenye kipato cha zaidi ya Tsh. 1,300,000 kwa Mwezi

Ripoti hiyo ilikuwa ikiangazia Ukuaji wa Miji unavyoongezeka, Upatikanaji wa Huduma za Umma kwa Usawa na Michakato ya Ushiriki wa Wananchi katika Maamuzi.

Chanzo: Ripoti ya Repoa
 
13% ndio wapo katika hiyo 300,000 mpaka 1,300,000?
2% ndio wanapata zaidi ya 1,300,000 ?

Nadhani 2% ndio itakuwa kubwa kuliko 13%, hata sijui ninachoongea ILA pita pita maeneo usiku wa Ijumaa na Jumamosi, utajua kati ya 2 na 13 ipi kubwa.
 
Hao wa Ijumaa na Jumamosi siyo mishahara hiyo.
 
13% ndio wapo katika hiyo 300,000 mpaka 1,300,000?
2% ndio wanapata zaidi ya 1,300,000 ?

Nadhani 2% ndio itakuwa kubwa kuliko 13%, hata sijui ninachoongea ILA pita pita maeneo usiku wa Ijumaa na Jumamosi, utajua kati ya 2 na 13 ipi kubwa.
Mm nipo kwenye asilimia 13
 
Utafiti wa Repoa uliofanyika Kati ya Machi na Aprili 2021 unasema 85% ya Vijana wa Kiume wenye chini ya Miaka 35 wanaishi kwa kipato cha chini ya Tsh. 300,000, huku wa Kipato cha kati wakiwa 13% na uwezo wa kupata Tsh. 300,000 hadi Tsh. 1,300,000 na 2% pekee ndio wenye kipato cha zaidi ya Tsh. 1,300,000 kwa Mwezi

Ripoti hiyo ilikuwa ikiangazia Ukuaji wa Miji unavyoongezeka, Upatikanaji wa Huduma za Umma kwa Usawa na Michakato ya Ushiriki wa Wananchi katika Maamuzi.

Chanzo: Ripoti ya Repoa
mseme tu asilimia 85% tunaishi bila kipato....yani sio tu chachini,hicho kipato chenyewe hatuna
 
13% ndio wapo katika hiyo 300,000 mpaka 1,300,000?
2% ndio wanapata zaidi ya 1,300,000 ?

Nadhani 2% ndio itakuwa kubwa kuliko 13%, hata sijui ninachoongea ILA pita pita maeneo usiku wa Ijumaa na Jumamosi, utajua kati ya 2 na 13 ipi kubwa.
Hapana mzee hii takwimu ipo sawa..
Mie naendaga viwanja kama baa kuna watu 100 wanakunywa nakuhakikishia chunguza vizuri utagundua wanaonunua pombe wanaeza wasizidi 30.. wengi chawa wananunuliwa....

Au K VANT moja kubwa watu sita... So nyomi baa lisikudanganye
 
Back
Top Bottom