UTAFITI: Asilimia 92 ya wananchi wanaunga mkono vipindi vya Bunge kurushwa moja kwa moja

  • Thread starter Sauti za Wananchi
  • Start date

Sauti za Wananchi

Sauti za Wananchi

Member
Joined
Sep 2, 2014
Messages
95
Likes
103
Points
40
Sauti za Wananchi

Sauti za Wananchi

Member
Joined Sep 2, 2014
95 103 40
Kwa mujibu wa utafiti wa Afrobarometer, asilimia 65 ya wananchi wangependa vyombo vya habari vitoe taarifa za maovu yanayofanywa na serikali ikiwemo vitendo vya rushwa. Hata hivyo, asilimia 31 wanasema utoaji wa taarifa hizo utaiathiri nchi.

Ni wananchi 8 kati ya 10 (75%) wanaosema kuwa vyombo vya habari vinafanya kazi nzuri ya kufichua maovu na rushwa, huku wananchi 2 kati ya 10 (18%) wakisema havifanyi kazi nzuri.

Kwa upande wa uhuru wa kutangaza habari, asilimia 53 wanasema vyombo vya habari viwe huru kutangaza habari yoyote huku asilimia 44 wakisema serikali iwe na mamlaka ya kufungia magazeti.

Vilevile, asilimia 65 wanasema vyombo vya habari havijawahi au kama vimeshawahi, ni mara chache sana vimekuwa vikitumia vibaya uhuru wake kwa kutangaza vitu ambavyo si vya kweli.

Wananchi wanaunga mkono kwa kiasi kikubwa uhuru wa maoni na kupata taarifa. Karibu wananchi wote (95%) wanasema wananchi wawe huru kuikosoa serikali pale ambapo wanaona imekosea.

Wananchi pia wanaunga mkono demokrasia. Takwimu za Sauti za Wananchi za hivi karibuni zinaonyesha asilimia 69 ya wananchi walichagua demokrasia kuliko aina nyingine ya serikali. Uungaji mkono huu wa demokrasia pia unadhihirika kupitia takwimu za Afrobarometer (2014) zinazoonesha asilimia 79 ya wananchi wakisema kuwa serikari inayoongoza kidemokrasia ndiyo aina ya serikali wanayoipenda zaidi na asilimia 81 wakisema ni vema wachague viongozi wao kupitia chaguzi huru za kidemokrasia.

Upatikanaji wa taarifa vilevile ni muhimu kwa wananchi. Asilimia 77 wanasema wananchi wa kawaida wawe na uwezo wa kupata taarifa zinazoshikiliwa na mamlaka za umma, huku asilimia 23 wakisema ni wale tu wanaofanya kazi kwenye mamlaka za umma ndiyo waruhusiwe kupata taarifa hizo.

Asilimia 80 wanasema upatikanaji wa taarifa hizo kwa wananchi utasaidia kupunguza vitendo vya rushwa huku asilimia 20 wakisema watumishi wa umma watatafuta njia nyingine za kuficha maovu yao.

Suala la kuunga mkono haki yao ya kupata taarifa za serikali, karibu wananchi wote (92%) wanasema ni muhimu kwa vipindi vya bunge kurushwa moja kwa moja kupitia luninga na redio. Asilimia 79 wanapinga maamuzi ya serikali ya kusitisha matangazo hayo na asilimia 88 wanasema bunge lirushwe moja kwa moja bila kujali gharama. Asilimia 12 wanasema wanadhani suala la kubana matumizi ni sababu nzuri ya kutokurusha vipindi ya bunge moja kwa moja.

Takwimu hizi zimekusanywa na Twaweza baada ya kutiwa saini kwa sheria mpya kandamizi ya Huduma za Vyombo vya Habari. Takwimu hizi ni za matokeo ya hivi karibuni ya utafiti wa Afrobarometer na Sauti za Wananchi.

twaweza-1-png.442017

twaweza2-png.442018

twaweza3-png.442019

twaweza5-png.442020
 
Barbarosa

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Messages
18,700
Likes
18,491
Points
280
Barbarosa

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2015
18,700 18,491 280

Hahah kwenye nchi ambayo 14% tu ya wakazi wake wana Umeme, na zaidi ya 68% wanaishi chini ya Dola 1 kwa siku, halafu zaidi ya 90% ya hao Wananchi wanataka waangalie TV live??????!!!!!!
Kweli sisi Waafrika kulikuwa na kila sababu ya kupigwa viboko ni wajinga kama Giza!
 
Castr

Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Messages
13,541
Likes
23,378
Points
280
Age
26
Castr

Castr

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2014
13,541 23,378 280
Hahah kwenye nchi ambayo 14% tu ya wakazi wake wana Umeme, na zaidi ya 68% wanaishi chini ya Dola 1 kwa siku, halafu zaidi ya 90% ya hao Wananchi wanataka waangalie TV live??????!!!!!!
Kweli sisi Waafrika kulikuwa na kila sababu ya kupigwa viboko ni wajinga kama Giza!
Bob ukiona hivyo jua hiyo ni asilimia ya hiyo 14% unayoisema wewe.

Na kutokana na utaratibu wa Tz mtu mwenye tv anaweza akaaccommodate wasio nayo wakaangalia kwake.

Hata hivyo ingawa watu hawana umeme wana redio zinazotumia betri na simu zenye redio wanaweza kulisikiliza live.
 
byeyombo

byeyombo

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2015
Messages
1,001
Likes
1,329
Points
280
byeyombo

byeyombo

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2015
1,001 1,329 280
Hivi 8 Kati ya 10 ni 75%????
 
C

chabusalu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Messages
6,746
Likes
4,072
Points
280
C

chabusalu

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2016
6,746 4,072 280
Hahah kwenye nchi ambayo 14% tu ya wakazi wake wana Umeme, na zaidi ya 68% wanaishi chini ya Dola 1 kwa siku, halafu zaidi ya 90% ya hao Wananchi wanataka waangalie TV live??????!!!!!!
Kweli sisi Waafrika kulikuwa na kila sababu ya kupigwa viboko ni wajinga kama Giza!
Kwanini unafanya mambo yako yako kinyume nyume, maana yake unapinga taarifa za serikali zinazoonyesha kuwa kasi yake ya kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na umeme ni KUBWA SANA! Hata hivyo, nini wewe binafsi unapendelea katika hili kwa kuzingatia hizo takwimu "uchwara" ulizotuwekea: Je, tusiangalie Bunge mubashara au tuangalie?
 
LUS0MYA

LUS0MYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2011
Messages
243
Likes
105
Points
60
LUS0MYA

LUS0MYA

JF-Expert Member
Joined Aug 4, 2011
243 105 60
Serikali iruhusu haya matangazo ya moja kwa moja kwani itasaidia kuumbua wale wabunge na vyama vilivyokuwa mstari wa mbele kupiga vita wizi,ufisadi,utumishi mbovu,rushwa,mikataba mibovu,nk ambao wamegeuka na kuwa wasemaji wa wahalifu....Wale waliokuwa wakilalamikia gharama kubwa za ziara za raisi,viongozi,wabunge ambazo hazina tija..leo wanakejeli zuio la kusafiri nje ya nchi bila ruhusa....wale waliokuwa wakilalamika viongozi wezi wabovu na watuhumiwa wa rushwa na ufisadi kuhamishwa vituo vya kazi au kuchelewa kuchukuliwa hatua na sasa wanapiga kelele kuhusu haki ya mtumishi kusikilizwa na kuachwa hadi mahakama ithibitishe...Wale waliokuwa wakipiga kelele kuhusu dili zinazofanywa na maafisa wakubwa wa serikali kuweka fedha katika mabenki(deposits) na fixed deposit na baadaye serikali kukopa fedha zake kwa riba za juu kutokana na fedha zake..kwamba serikali iache hela zake huko ili kulinda mabenki...nk watu watapata kutambua haya mambo kama watayaona live bila kuhadithiwa...
 
Gangongine

Gangongine

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2015
Messages
3,861
Likes
1,754
Points
280
Age
49
Gangongine

Gangongine

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2015
3,861 1,754 280
Hao labda wa JF. Mwananchi wa kawaida hicho siyo kipaumbele. Watu wanataka maji, barabara, huduma za Afya, umeme , masoko ya mazao na bidhaa, Elimu nk. Kuuza sura wapi na wapi????
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,028
Likes
5,491
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,028 5,491 280
Hakuna haj ya Serikal kuficha mazungumzo wanayozungumza Bungeni. Kwanini Serikali inaficha? Kuna kitu wanacho tuficha serikali sisi Wananchi tusipate kukiona nacho Udhaifu wa Kiutendaji kazi wa Serikali iliyopo madarakani. Hakuna kabisa haja au umuhimu wa kuficha Mazungumzo yanayozungumzwa katika Bunge, hii ni dalili inayo onyesha udhaifu wa Serikali iliyo madarakani kiutendaji wake wa kazi.
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,028
Likes
5,491
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,028 5,491 280
Hao labda wa JF. Mwananchi wa kawaida hicho siyo kipaumbele. Watu wanataka maji, barabara, huduma za Afya, umeme , masoko ya mazao na bidhaa, Elimu nk. Kuuza sura wapi na wapi????
Pasipo kuwaona Wabunge wenu au Viongozi wenu wanavyojadiliana katika kuendeleza uchumi wa nchi na maendeleo mutajuaje kinacho endelea kwenye Serikali yetu siku za mbele? kuwaona na kusikia majadiliano bungeni ni bora kuliko kusikia kwenye maredioni tu. Ndio maendeleo ya nchi lazima kuwe na ushindani ndani ya bunge kati ya Wabunge wa upinzani na Serikali ndipo kutakuwepo na maendeleo ya nchi pasipo na kuwaona wanavyo shindana bungeni utajuwa kitu gani kinacho endelea Serikalini?Na Wakati wa uchaguzi utakuwa wewe Mpiga kura kazi yako unamchaguwa mtu ambae hafai kukuongoza kwa kuwa hujamuona anavyofanya kazi zake. Amka Mkuu kuona bunge live jinsi linavyofanyika ni bora kuliko kusikia Ma- redioni tunakwenda na wakati mkuu.
 
C

Chagga King

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2011
Messages
1,768
Likes
680
Points
280
C

Chagga King

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2011
1,768 680 280
Huo utafiti ni wa uwongo, ukweli ni kwamba wananchi asilimia 100, wanataka bunge lioneshwe mubashara.
 
Forum statistics

Threads 1,275,064
Members 490,894
Posts 30,531,911