Utafiti 1990: Watanzania ni wavivu

MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,064
2,000
Unataka wabadili mfumo wa elimu Ili ccm Ife? Kwani wao wajinga?
Sasa hutuambii kwa namna gani elimu ya sasa inaisaidia CCM kuwa madarakani, na ni mabadiliko gani ktk elimu yatakayo saidia kutoka tulipo. nijuavyo mimi ukiondoka URAIS/CIVICS masomo mengine yote ni standard ya ki dunia, principals na formula ni zile zile. Labda mfumo wa ufundishaji vyuoni. course work 40% huku 60% ikiwa ni final exams. wenzetu km KOREA, USA na nk, course work ni 60%-80% final exam 20%-30%.
 
MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,064
2,000
Hata CDM hawako exceptional. Wakati mmoja CDM waliaminishwa ZZK ni msaliti, wanachama wengi wakajaa. Kisa ni waraka wa akina Mwigamba na Prof. Kitila uliokuwa unajenga mkakati wa kumuandaa ZZK ili awe mkiti wa CDM.
2020 ZZK akaketi meza moja wakubwa CDM kusaini MoU kupinga matokeo ya uchaguzi. Kama wangekuwa wanafikiri vya kutosha, kumuita mtu msaliti kwa kujiandaa kimkakati kugombea uongozi na wanachama wakajaa, hapo kuna shida pahala.
Ni CDM hao hao kwa miaka mingi walimwita EL fisada, 2015 wakamsafisha kwa hisopo huku TL akigeuka na hoja nyepesi as if sio yeye ambae kwa miaka ya kutosha alimuimba EL kama mtu asie msafi.

Iko haja Watanzania tukaja na mijadala fikirishi yenye kufungua fahamu zetu kila mahali kwa ajili ya kesho njema kwetu, wanetu na wajukuu zetu.
Ukilaza hauna chama, hata CDM wameshindwa kutumia science kuiondoa CCM madarakani.
 
mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
5,493
2,000
Ukilaza hauna chama, hata CDM wameshindwa kutumia science kuiondoa CCM madarakani.
Mbona hata wewe umeshindwa kuiondoa,
Huyo mtafiti huwa anahudimia familia za watanzania Hadi aseme wavivu?
 
Bepari2020

JF-Expert Member
Nov 7, 2020
522
1,000
Uvivu uliletwa na Nyerere na Ujamaa wake. Mashirika ya umma watu walilipwa hata kama hawafanyi kazi kwa bidii. Kwa sababu hayo mashirika yanabebwa na serikali hata kama yanafanya kazi kwa hasara.
 
MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,064
2,000
Uvivu uliletwa na Nyerere na Ujamaa wake. Mashirika ya umma watu walilipwa hata kama hawafanyi kazi kwa bidii. Kwa sababu hayo mashirika yanabebwa na serikali hata kama yanafanya kazi kwa hasara.
wajamaa asilia china na korea mbona ni wachaoa kazi?
 
Bepari2020

JF-Expert Member
Nov 7, 2020
522
1,000
wajamaa asilia china na korea mbona ni wachaoa kazi?
Wachina waliacha ujamaa siku nyingi kwa sababu ulifeli kule pia. Cultural revolution ya Mao Zedong iliacha China masikini sana na mamilioni walikufa. Korea kaskazini watu wanakufa njaa hawana uchapa kazi wa aina yoyote.
 
Kalunya

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
3,771
2,000
Sasa hutuambii kwa namna gani elimu ya sasa inaisaidia CCM kuwa madarakani, na ni mabadiliko gani ktk elimu yatakayo saidia kutoka tulipo. nijuavyo mimi ukiondoka URAIS/CIVICS masomo mengine yote ni standard ya ki dunia, principals na formula ni zile zile. Labda mfumo wa ufundishaji vyuoni. course work 40% huku 60% ikiwa ni final exams. wenzetu km KOREA, USA na nk, course work ni 60%-80% final exam 20%-30%.
Mfumo wetu wa elimu hauna tija kwa muhitimu unamfanya tu asiruke stage ya ukuaji,haumsaidii mwanafunzi kuwa critical thinking kumudu kutatua changamoto zinazomzunguka,zaidi ya kumfanya awe mkariri mzuri,thus ukiwa na uwezo mzuri wa kukariri ni rahisi kupata A kwenye masomo..
Kiufupi ni mfumo unaomfanya mwanafunzi kuendelea kuwa mjinga thus sio ajabu kukuta mhitimu anaacha raslimali tele zilizojaa kijijini kwake anakimbilia mjini kuuza machinga au kuendesha bodaboda,hali wenzetu weupe sababu ya elimu bora anarudi kulekule kijijini penye raslimali zilizokimbiwa na mhitimu wetu anazigeuza fursa anapata pesa anakuwa tajiri nchini yake inakuwa tajiri pia.
Sasa ccm inatoa elimu duni haitaki kubadili mitalaa ya critical thinking Ili vijana wajinasue waone fursa maana wanaamini huwezi mtawala mwenye shibe.Pia utumia kodi kama njia ya kuwafanya watz wasiinuku wazidi kuwa masikini kwa kuwezesha wachache ndio wamudu kununua bidhaa muhimu mfano magari,ujenzi,nk.
Watz ni masikini sio kwa sababu hawana pesa au mitaji bali wamenyimwa elimu,maana ya umasikini ni upeo Mdogo wa kuona fursa zinazowazunguka.Mfano sekta ya madini na kilimo hizi mbili tu zinaweza ajili vijana wote nchini plus na wengine toka nchi jirani na still zikapelea.Shida ni elimu,asiye na maarifa ni mjinga ni rahisi kumtawala.Thus wajinga wanayo nguvu ya kuiweka ccm madarakani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom