Utafanyaje ukijua mtoto uliyenaye, unayempenda na kujivunia, Sio mtoto wako?

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Kuna ndugu amekutwa na mkasa huu nikaona embu ni shee na wewe mwana JF (Home of Great Thinkers).

Umelea ujauzito kwa mapenzi kubwa, umemkuza mtoto vizuri mno, umemsomesha vema, vyote kwa upendo wa dhati. Na bahati mbaya uliyenaye ni huyohuyo kwakua badae mke hakufanikiwa kushika ujauzito.

Halafu unakuja kujua kumbe huyo mtoto si wako!
Utafanye?
 
Ukielewa kuwa duniani tunapita tu, jambo hilo siyo la kuumiza kichwa, tena unaweza kwenda kusaidia na wengine kama una uwezo
 
Hakuna cha kufanya, ni kutulia, kujifanya hujui na kumpenda kama mwanao.

Kuna mzee mmoja hapa yeye mweupe, mama mweupe, watoto weupe lakini alizaliwa mmojawapo mweusi akahisi si wake. Huyo mzee(jina kapuni) akamnyanyapaa sana na kuwapenda wale wengine kwa kuwasomesha shule nzuri yule mwingine kayumba. Mwisho wa siku dogo alifaulu na ana maisha safi, ndo anaisaidia familia kwa sasa. Wale wengine walifeli na wanasaidiwa na huyo dogo japo nao walimnyanyapaa.
 
Tatizo kubwa ni wewe kuanza kutaka kujua mtoto ni wa nani. Kama mama hajawahi kukuambia kuwa mtoto ni wa nani unatafuta nini zaidi? Kama wewe ndio mwenye tatizo ulishindwa kumzalisha mkeo, ya nini kutafuta babake? Kama mtoto umekaa naye zaidi ya miaka 10 wala hujawahi kuona mtu amekuja kusema anatafuta mimba yake iliyoibwa kimazingira sasa umetoa wapi maneno machafu kuwa huyu sio wako??
Kaa kimya, hadi aje huyo soro mwenye akili fupi ya kuokota mtoto mtu mzima. Na huyo mtoto akienda na aende tu wala hakufai. Nawachukia sana wazazi wanaokwenda kupima DNA. Je ukikuta ni wako huyo mtoto uliyemdhalilisha mamake hivyo hivi kweli naye atakupenda? Acheni hizo
 
Wanaume bora tuishi kwa kujikubali tu kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa sisi ni social fathers kwa wanetu (i.e. not necessarily biological fathers). Kitanda hakizai haramu.
 
kama umejua unasubiri nini.chagua kifurushi gani kwa nyumbani kumenoga au mitandao mengine
 
Hii imeshawahi kunikuta ila nilishituka punde tu baada ya mtoto kuzaliwa,

Nilimwambia ukweli mama yake japo alijifanya kusikitika, na kunilaani

Nilitoa jibu moja tu najinukuu "kama umeichoka hii dunia ya kina diamond, hamissa mobeto na trump endelea kuning'ang'ania"

Tuliachana pale pale hospital, namshukuru Mungu baada ya kuondoka pale ndio nikamjua baba halali wa yule mtoto

ok turudi kwenye mada, huyo jamaa kama amethibitisha pasipo shaka, hatakiwi kumng'ang'ania huyo mtoto pia hatakiwi kubaki na mama wa huyo mtoto.
 
Mpende Tu mtoto hakuna shida. Dhambi zako zote unazofanya hakuna anaezihesabu, hivyo kama mwanamke kakudanganyia mtoto wewe mlee mtoto kwa mapenzi yote, hiyo dhambi atailipia yeye mwenyewe tena hapa hapa duniani
 
Endelea kumpenda hivo hivo kwani upendo ndio silaha pekee ambayo itakufanya usione kama sio mwanao

Kisa cha kweli jamaa mmoja alikuwa kwenye deathbed alikuwa Na jamaa mwingine amelazwa pembeni jamaa wakati anakata roho alitamka maneno yafuatayo "hakuwa mwanangu lakini nilimpemda kweli"

Issue ilikuwa hivi mwanamke alimbambikia mtoto mwanaume na yule mwanaume alijua kila kitu lakini hakuwahi mwambie mkewe

Upendo wake kwa mwanae haukuwahi pungua alimpenda kweli kweli lakini alijua wazi sio mtoto wake

Aliweza useme huu ukwel wakati anakata roho mke wake alipopewa habari alilia sana lakini jamaa alikuwa Na upendo wa kwel, upendo ni Dawa ya magonjwa yote
 
Ila tukiongea ukweli guys,inauma sana aisee..

Kwa Mimi sitaweza vumilia kuishi na huyo mama na mtoto wake kabisa..
 
Kuna ndugu amekutwa na mkasa huu nikaona embu ni shee na wewe mwana JF (Home of Great Thinkers).

Umelea ujauzito kwa mapenzi kubwa, umemkuza mtoto vizuri mno, umemsomesha vema, vyote kwa upendo wa dhati. Na bahati mbaya uliyenaye ni huyohuyo kwakua badae mke hakufanikiwa kushika ujauzito.

Halafu unakuja kujua kumbe huyo mtoto si wako!
Utafanye?
Kama hata huyo mtoto anakuheshim mpende tuu usioneshe tofauti
 
Now days, washikaji kibao wanalea watoto ambao sio damu yao, daah wanawake pepo mtaiona kwa mbali sana
 
Kitendo cha kulea ujauzito, kumpenda mtoto, kumsomesha na kumvesha na kumlisha tayari huyo ni Mtoto wangu, sintakuwa na tatizo naye na nitaendelea kumlea bila kinyongo chochote kwake..

Ila ili niendelee kuishi naye Kwa amani, mamake itabidi afe..
 
Baba mtoto akija kumchukua kwa kwa kufuata sheria za mahakama.
Utafanya nn
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom