Utafanya nini ukijua hela zako anatumia mwanaume mwingne?

Wala usichukue chochote....!! Mwachie Songa Mbele...!! Ushajifunza tayari
Noooo tena big noooo! ingekuwa ni mimi ningemwachia vitu vyote endapo tu alishakuwa ni mke wangu tena ambaye tushakuwa na mtoto/watoto, na si huyo wakudanda.
Nakushauri chukua vyako lakini iwe ni kwa amani kabisa, usiwashe moto kwani mlipuko wake kwako unaweza kuwa mkubwa sana na ukakuletea madhara makubwa pia.
 
Noooo tena big noooo! ingekuwa ni mimi ningemwachia vitu vyote endapo tu alishakuwa ni mke wangu tena ambaye tushakuwa na mtoto/watoto, na si huyo wakudanda.
Mkuu Mtu mpumbavu hata umwagie gunia la Pesa hamna atakachofanya.. Hilo gari Baada ya Muda litakosa Huduma na ndiyo mwanzo wa kumlaiza
 
Ushaur wowote hapo utafaa ikiwa suala LA kumuacha umelitanguliza. Hakuna haja ya kulea katoto Kama haka kanachomuona mtoto mwenzie chuo anamfaa. Mwachie na yey jeraha LA kudum akirud mtaani ajira hakuna na wew ushaoa
 
Usawa huu unahonga IST na kutoa 250k kila wiki!! Si bora utafute mke uoe tu kwanza gharama ni kidogo halafu hakuna stress kama za hawa mabinti wasomi uchwara waliojaa humu vyuoni ambao wanaishi maisha ya kuigiza.
 
Wanajamvi, wakubwa shikamoni na vijana habarini!

Nilitoa uzi juzi kati juu ya nini utafanya ukishagundua kuwa pesa unazohonga kwa mtu umpendaye kama mwanaume rijali, zinakwenda kumfaidisha mwanaume mwingine.

Ama kweli usilojua ni sawa na usiku wa giza, ile situation ni yangu na imenitokea na nilitaka kupata ushauri japo haukunitosha.

Nina demu wangu, yupo chuo mwaka wa pili, tulikubaliana kuwa nitamuoa akimaliza chuo, nimempangia nyumba nzima, nimempa usafiri(gari, IST new model), laptop nimenunulia nzuri, ana mkopo ila ada na hela ya kula namtumia 250k kila baada ya week mbili.

Nimekosa nini mimi? Nimegundua kuwa kumbe alikuwa akinitusi na kunikejeli yeye na mtu wake ambaye hata kazi wala hela hana, yaani natuma hela yeye anahonga huyo mpuuzi, gari yake anaendesha huyo mpuuzi na mengine mengi.

Wanafikia hatua ya kunicheka na kuyatusi maumbile yangu, naandika kwa uchungu mkubwa sana, nafikiria nifanye nini?

Pesa nampa kwa nini sipati mapenzi ya kweli? Nafikiria nimfanye nini yeye na huyo mpuuzi? Nina siku ya 4 sijaenda job nipo tu ndani, napitia wakati mgumu, kuhusu chuo huyo mpuuzi anasoma UDSM law.

Nishaurini nisije fanya uamuzi mbaya!
Acha kulipa kodi,chukua gari yako,sitisha msaada
 
Moja ya makosa makubwa sana tunayoyafanya wanaume kwa wanawake/wapenzi wetu.

Nakushauri tumia akili uchukue vitu vyako, mbinu ya kuchukua vitu vyako kama ashagundua kwamba umemshtukia tafuta namna yoyote ile mwambie unataka kwenda kufanyia "service" gari yako, then muombe unataka kumtembelea then take all the things of yours.

Kama unaweza kukaza achana naye, start a new page, wanawake wapo kibao kabisa tena you can take even her best friend as long as you're good in your pockets. Kama utataka mbinu za kumpata rafiki yake kama utakuwa interested kum hurt ni pm

Acha habari za kutokwenda kazini ndg, brother hutaheshimika kama utaishiwa kitu mfukoni, hata ndugu watakuona wewe ni BWEGE, Usioneshe udhaifu na punguza kupenda sana na kuwaamini watu hasa tunaokutana nao ukubwani, trust me, mtu wa kumuamini ni yule tu unayemuona kwenye kioo pindi ujiangaliapo!! Lakini bado una nafasi kubwa sana, wanawake wapo, usihangaike kutafuta unayempenda wewe bali tafuta mwanamke atakayekufariji kwani siku zote TUNAOWAPENDA HAWATUFARIJI BALI TUNAFARIJIWA NA WAPENZI TUSIOWAPENDA. This is the naked truth brother!!

You have a long way to go kwanini upoteze muda kwa mtu ambaye hata maisha bado hajayajua? A second year student automatically bado ananuka maziwa ya mama knowing nothing about life. Halafu unaonekana mshikaji wangu unapenda unazimia, acha kabisa moyo huo hadi ujiridhishe na umpendaye. Mbinu nyingine ya kuishi a happiest life in relationship ni kuwa na wa pembeni just hata kwa ku pretend but make your lover know that there's another person you're dating, sometimes make even a fake call nakuapiza utapendwa mpaka basiiiii!!! This scenario proves that love is nothing to do with your money sometimes!!

Pole sana mkuu!!
 
Wewe ulizani mapenzi ni pesa sio na toka lini mwanamke akasomeshwa!!!
Tena mwanamke ukimpatia kila kitu anakua anawaza kugongwa tu na wewe inaonesha ulijikeep busy ukashindwa kumridhisha kimapenzi
 
Hii thread Ina chai, mwanaume mwenye uwezo wa kumuhonga mwanamke gari ya IST na tshs laki 2 kila baada ya Wiki mbili hana muda wa kuja humu jF kuanzisha uzi..
 
Usawa huu unahonga IST na kutoa 250k kila wiki!! Si bora utafute mke uoe tu kwanza gharama ni kidogo halafu hakuna stress kama za hawa mabinti wasomi uchwara waliojaa humu vyuoni ambao wanaishi maisha ya kuigiza.
Na kumpangishia nyumba nzima juu,

Alaf ni demu tu hujaoa,

Soma ishara mzee, hupendwi hapo, unachunwa tu papaaa.

Tuliza akili, tafuta mfanyakazi mzuri na msomi age 25-28 wenye desperate na ndoa uoe papaaa.

Simple mbonaaa
 
Kama hii siyo Chai nakupa pole sana, chukua vitu vyako achana naye songa mbele kuna maisha baada ya kuachana.
 
Mjomba mbona hii dunia yetu ina warembo kibao.

Hiyo mizigo uliyokuwa unawekeza hapo acha tafuta mgodi mwingine tia mpunga wako acha unyonge hiyo si ridhiki jombaa😏😏
 
Huyo 'maraya' piga chini braza. Beba vitu vyako ondoka. Usirudi hata akilia kwa machozi ya damu. Hawabadiliki kamwe! Narudia hatobadilika kamwe!
 
Wanajamvi, wakubwa shikamoni na vijana habarini!

Nilitoa uzi juzi kati juu ya nini utafanya ukishagundua kuwa pesa unazohonga kwa mtu umpendaye kama mwanaume rijali, zinakwenda kumfaidisha mwanaume mwingine.

Ama kweli usilojua ni sawa na usiku wa giza, ile situation ni yangu na imenitokea na nilitaka kupata ushauri japo haukunitosha.

Nina demu wangu, yupo chuo mwaka wa pili, tulikubaliana kuwa nitamuoa akimaliza chuo, nimempangia nyumba nzima, nimempa usafiri(gari, IST new model), laptop nimenunulia nzuri, ana mkopo ila ada na hela ya kula namtumia 250k kila baada ya week mbili.

Nimekosa nini mimi? Nimegundua kuwa kumbe alikuwa akinitusi na kunikejeli yeye na mtu wake ambaye hata kazi wala hela hana, yaani natuma hela yeye anahonga huyo mpuuzi, gari yake anaendesha huyo mpuuzi na mengine mengi.

Wanafikia hatua ya kunicheka na kuyatusi maumbile yangu, naandika kwa uchungu mkubwa sana, nafikiria nifanye nini?

Pesa nampa kwa nini sipati mapenzi ya kweli? Nafikiria nimfanye nini yeye na huyo mpuuzi? Nina siku ya 4 sijaenda job nipo tu ndani, napitia wakati mgumu, kuhusu chuo huyo mpuuzi anasoma UDSM law.

Nishaurini nisije fanya uamuzi mbaya!
Kila siku watu wanazungumza hapa kuwa mchumba hasomeshwi wewe husikii?
Hapo ana Mario wake ambaye kazi yake kubwa ni kumpigisha Nondo za Skul, Kumfanyia Assignment etc....
 
umeoa!? maana dalili zinaonesha huyo dem ni mchepuko.... All in all dunia ina watu zaidi ya billioni 7 unahangaishwa na mtu mmoja!? BE A MAN MKUU
 
Back
Top Bottom