Utafanya nini endapo utagundua mkeo hajui kupanga bajeti?

lewis acid

Member
Mar 21, 2017
57
120
Habari zenu wadau
Naandika kwa kifupi sana ila naomba kupata mawazo yenu.
Assume unaishi na mke katika zama hizi za maisha kua ghali lakini kuna jambo linakukwaza kwamba mkeo hawezi kupanga bajeti na kuisimamia kwa fedha unazompa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Fedha unaitoa kwa ajili ya matumizi madogo madogo, ikiwa na mantiki kwamba vitu vyote vya kutumia kama chakula,mboga,mafuta,sukari etc vipo ndani, na umeamua kutoa fedha kiasi kwa ajili ya emergencies ndogo ndogo lakini unakuja kugundua kwamba fedha hiyo inafujwa (inatumika tofauti na kusudi lake).

Kwa mara kadhaa unajaribu kukaa na mwenzi wako kumuelekeza lakini kila awamu anarudia yaleyale
Naomba mawazo yenu nini kinafaa kufanya katika situation kama hii

Kwa Picha ya harakaharaka kuna watu wananikejeli na kunitolea lugha za kunitusi kana kwamba wao hawana changamoto katika familia zao, huu uzi wangu unabeba changamoto za familia nyingi na hii ni sauti ya wanaume wengi nimewasaidia kusema,

naona bado tuna tatizo baadhi wa wake zetu bado hawana dream wala hamu ya kusonga mbele kiuchumi ndio maana kila senti inayopatikana wao hutaka itumike iishe ilimradi waishi vizuri Leo, suala la maisha ya kesho wanawake wanaliona kama sio muhimu
 
Si useme tu ukweli umemchoka mkeo unamtafutia sababu,kupanga matumizi kitu gani. Si umfundishe na mkae pamoja kama familia mpange hayo matumizi,ikishindikana uanze kwenda kununua hivyo vitu mwenyewe hakuna kumkabidhi pesa itaondoa malalamiko na utajua bei za bidhaa husika
 
Sababu umeandika story ya kufikirika kuonyesha mkeo hana akili au mpenda pesa sana. Ingekua anagongwa na wauza genge kisa pesa hapo sawa ungekua na haki ya kulalamika ila suala la matumizi mzigo wako mwenyewe

Hatujui kipind mnatongozana ulimzoesha pesa ndefu au lala. ulimuonyesha una hela sana sasa ya nn awe mbahili wakati kuna hela za kumwaga
Nimekujib ivo kwa sababu umekuja na conclusion
Sasa wewe ulijuaje kwamba nimemchoka?
 
sasa ndg yng hilo kosa ndo l kuacha mke? msaidie mpangie t bajet kama vp nenda mwnyw sokoni kanunue kumbuka hakuna binadam mkamilifu mapunguf yp t
 
Back
Top Bottom