Utabiri wangu kulingana na Uhalisia: Namba mbili au namba tatu mmoja lazima apumzishwe

Uzalendo Wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
1,123
2,000
Wana JF

Nawasalimu wote

Nianze kwa kusema mimi sio Mganga wala Nabii ila ninenayo ndiyo ukweli unaotokana na uhalali wa hatimiliki kwa mujibu wa maagano.

Hizo namba tajwa hapo juu yaani 2 na 3 zina wenyewe ila bahati mbaya tu kipindi hiki kifupi wenyewe wamezikosa bila kutarajia na zinatumiwa na wengineo kwa bahati mbaya tu!

Hata hivyo kwa kuwa wenye namba zao wapo na huwa hawashindwi basi lazima substitution ifanywe ili mmojawapo hususani namba tatu akae pembeni asubiri muda muafaka arejee dimbani.

Substitution kwa nambari tatu haitokani na yeye kukosa uwezo! Hoja ni kuwa kwa sasa anacheza namba isiyo yake kulingana na desturi ya upangaji wa timu!

Wenye hatimiliki hawakujua kama haya yangalitokea hata hivyo maadamu yameshatokea basi lazima yajipange kuanzia sasa ili wamiliki wanachostahili.

Ni namba zao kwa mujibu wa maagano & mazingira halisi ya sasa!

Ni lazima iwe hivyo na ni suala la muda tu na wala usipoteze nguvu kunibeza.

Muda utaongea

Wasalaam
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,302
2,000
Uhuru wa habari umesharudi mbona unataka kuturudisha misri?
Kuna mifugo fulani ikishazoea kufungwa kamba, siku hata ukiifungulia inakuwa inabaki pale pale ikifikiri bado imefungwa kamba.

Mtu uko mtandaoni, hutumii jina lako, bado unaendekeza ramli za numerology kama mtabiri muongo anayetaka kupiga hela kwa utabiri feki bila kuwajibishwa utabiri usipotimia?
 
Kanzastone

JF-Expert Member
Jan 14, 2021
244
500
Wana JF

Nawasalimu wote

Nianze kwa kusema mimi sio Mganga wala Nabii ila ninenayo ndiyo ukweli unaotokana na uhalali wa hatimiliki kwa mujibu wa maagano

Hizo namba tajwa hapo juu yaani 2 na 3 zina wenyewe ila bahati mbaya tu kipindi hiki kifupi wenyewe wamezikosa bila kutarajia na zinatumiwa na wengineo kwa bahati mbaya tu!

Hata hivyo kwa kuwa wenye namba zao wapo na huwa hawashindwi basi lazima substitution ifanywe ili angalao mmojawapo hususani namba tatu akae pembeni

Wenye hatimiliki hawakujua kama haya yangalitokea hata hivyo maadamu yametokea basi lazima yajipange kuanzia sasa ili wamiliki wanachostahili

Ni lazima iwe hivyo na ni suala la muda tu na wala usipoteze nguvu kunibeza
Nijuavyo mimi namba;

1. Rais wa JMT

2. Makamu wa Rais wa JMT

3. Waziri Mkuu

Je nimepatia??😆😆😆
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,658
2,000
Kuna mifugo fulani ikishazoea kufungwa kamba, siku hata ukiifungulia inakuwa inabaki pale pale ikifikiri bado imefungwa kamba.

Mtu uko mtandaoni, hutumii jina lako, bado unaendekeza ramli za numerology kama mtabiri muongo anayetaka kupiga hela kwa utabiri feki bila kuwajibishwa utabiri usipotimia?
Mama alishatahadharisha kuwa hii mitandao kuna watu wengine wanaitumia vibaya kwa kutoa ramli nyingine ambazo hazina vichwa wala miguu!

Moja ya ramli hizo ni hii hapa
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
30,512
2,000
Kuna mifugo fulani ikishazoea kufungwa kamba, siku hata ukiifungulia inakuwa inabaki pale pale ikifikiri bado imefungwa kamba.

Mtu uko mtandaoni, hutumii jina lako, bado unaendekeza ramli za numerology kama mtabiri muongo anayetaka kupiga hela kwa utabiri feki bila kuwajibishwa utabiri usipotimia?
Kama hivi Mkuu?
JamiiForums-89866555.jpg
 
Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
1,354
2,000
Wana JF

Nawasalimu wote

Nianze kwa kusema mimi sio Mganga wala Nabii ila ninenayo ndiyo ukweli unaotokana na uhalali wa hatimiliki kwa mujibu wa maagano

Hizo namba tajwa hapo juu yaani 2 na 3 zina wenyewe ila bahati mbaya tu kipindi hiki kifupi wenyewe wamezikosa bila kutarajia na zinatumiwa na wengineo kwa bahati mbaya tu!

Hata hivyo kwa kuwa wenye namba zao wapo na huwa hawashindwi basi lazima substitution ifanywe ili mmojawapo hususani namba tatu akae pembeni

Wenye hatimiliki hawakujua kama haya yangalitokea hata hivyo maadamu yameshatokea basi lazima yajipange kuanzia sasa ili wamiliki wanachostahili

Ni namba zao kwa mujibu wa maagano & mazingira halisi ya sasa!

Ni lazima iwe hivyo na ni suala la muda tu na wala usipoteze nguvu kunibeza

Muda utaongea

Wasalaam
Hata wakitolewa hutateuliwa wewe.

Kenge wa njano
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,422
2,000
Hizo namba tajwa hapo juu yaani 2 na 3 zina wenyewe ila bahati mbaya tu kipindi hiki kifupi wenyewe wamezikosa bila kutarajia na zinatumiwa na wengineo kwa bahati mbaya tu!

Wenye hatimiliki hawakujua kama haya yangalitokea hata hivyo maadamu yameshatokea basi lazima yajipange kuanzia sasa ili wamiliki wanachostahili

Ni lazima iwe hivyo na ni suala la muda tu na wala usipoteze nguvu kunibeza

Muda utaongea

Wasalaam
Mimi sikubezi, kwasababu, hakuna aliyedhani No. 1 angeweza kuchomoka, hivyo everything is posible, and anyhing can happen to anyone, at anytime, hata Namba 1 , hivyo usilazimishe kusema ni lazima iwe hivyo unless kama mpangaji ni wewe, lakini kama mpangaji ni YEYE, hao wenyewe wako, wanaweza kutangulia, kabla ya hao unaotaka waondoke!.

P
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,302
2,000
Hata wakitolewa hutateuliwa wewe.

Kenge wa njano
Waziri Mkuu hawezi kutolewa bila sababu nzito, serikali ilishawahi kusema kwamba kuwa na mawaziri wakuu wastaafu wengi ni gharama kubwa.

The same goes for VP.

Hizi ramli ingefaa ziwe specific kutaja watu na tarehe watakazoondolewa ili turudi hapa kuhakiki.
 
Lakasa chika7

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
378
1,000
Mimi sikubezi, kwasababu, hakuna aliyedhani No. 1 angeweza kuchomoka, hivyo everything is posible, and anyhing can happen to anyone, at anytime, hata Namba 1 , hivyo usilazimishe kusema ni lazima iwe hivyo unless kama mpangaji ni wewe, lakini kama mpangaji ni YEYE, hao wenyewe wako, wanaweza kutangulia, kabla ya hao unaotaka waondoke!.

P
Namba 1 mwendazake kauliwa.. Korona haipo hivyo
 
Lakasa chika7

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
378
1,000
Waziri Mkuu hawezi kutolewa bila sababu nzito, serikali ilishawahi kusema kwamba kuwa na mawaziri wakuu wastaafu wengi ni gharama kubwa.

The same goes for VP.

Hizi ramli ingefaa ziwe specific kutaja watu na tarehe watakazoondolewa ili turudi hapa kuhakiki.
Mpango kumdedisha
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,391
2,000
Mimi sikubezi, kwasababu, hakuna aliyedhani No. 1 angeweza kuchomoka, hivyo everything is posible, and anyhing can happen to anyone, at anytime, hata Namba 1 , hivyo usilazimishe kusema ni lazima iwe hivyo unless kama mpangaji ni wewe, lakini kama mpangaji ni YEYE, hao wenyewe wako, wanaweza kutangulia, kabla ya hao unaotaka waondoke!.

P
Mkuu Paskali, karibu tena ulipotea sana bana, watu wakazusha eti umepitiwa na upepo wa kisulisuli - watu wabaya sana bana.

Kocha ashabalika, mbinu zimebadilika, bechi la ufundi pia lazima libadilike - ni lazima apange kikosi cha ushindi kuanzia Kepteni hadi kipa ili KAZI IENDELEE bila mikwaruzo.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,391
2,000
Waziri Mkuu hawezi kutolewa bila sababu nzito, serikali ilishawahi kusema kwamba kuwa na mawaziri wakuu wastaafu wengi ni gharama kubwa.

The same goes for VP.

Hizi ramli ingefaa ziwe specific kutaja watu na tarehe watakazoondolewa ili turudi hapa kuhakiki.
Mkuu ipi ni gharama kubwa, kuwa na mtendaji asiyetimiza majukumu yake umlinde na kazi ziendelee kulala ili mradi tu usiongeze number ya wastaafu ama !!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom