Utabiri wangu juu ya Uchaguzi Mkuu na hali ya kisiasa miaka 10 ijayo

Oct 11, 2015
49
35
Kama mchambuzi wa maswala ya siasa hapa nchini nisiyekua na chama chochote, huu ndo utabiri wangu kwa siasa za nchi yetu katika miaka 10 ijayo;

CCM itashinda uchaguzi mkuu kwasababu wamesimamisha mgombea mwadilifu, mzalendo wa kweli, mchapakazi, mwajibikaji na mwajibishaji, kimsingi wamesimamisha 'masihi' wa aina yake. Ukawa itashindwa na kulalamika kua wameibiwa kura naam SIRAHA YA MUOVU YOYOTE NI UONGO. Ukawa watashindwa kwasababu wanachama wa upinzani waliochukizwa na kitendo cha ukawa kumpokea fisadi papa, wengi watampigia magufuli, naam waliokua wafuasi wa DR. SRAA na PROF. LIPUMBA wataongeza kura zao kwa Dr. Magufuli, wasomi wengi wazalendo kama mimi tuliokua tunaichukia sana ccm lakini kwa ccm kumsimamisha kiongozi mahiri na madhubuti msomi wa PhD, wengi tutaongeza kura zetu kwa TINGATINGA na kumpa ushindi.

Vyama vinavyounda ukawa yaani Chadema, cuf, nccr na nrd vitapoteza ushawishi wao kwa wananchi baada ya kushindwa vibaya katika uchuguzi mkuu. Chadema, cuf, nccr na nrd vitafifia katika ramani ya siasa nchini kama si kufutika kabisa. Hivyo wanachama wengi sana wa chadema na vyama vinavyounda ukawa watahamia ACT na CCM, hivyo CCM na ACT vitaongeza ushawishi wao kwa wananchi na kupata wafuasi lukuki kutoka ukawa. Ndipo ukawa na vyama vyake vitafutika au kufifia katika ramani ya siasa nchini huku CCM na ACT viking'aa zaidi na kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za tz. Hivyo kwa miaka kumi ijayo na zaidi tutabaki na vyama viwili tu vikubwa, CCM na ACT. Nini kitatokea nchin kipindi cha miaka kumi ijayo? Siasa ya nchi itabadilika kutoka siasa za matusi, vurugu, propaganda chafu n.k na kua siasa safi kwa maendeleo ya nchi. Kutokana na uongozi safi na bora wa kiongozi mahiri na madhubuti Dr. John Pombe Magufuli, viongozi watawajibika na kuwajibishwa, uchumi wa nchi utakua kwa kasi na kuimalika, nchi itaendelea mara kumi zaidi kuliko kipindi cha jakaya, na baada ya magufuli kumaliza muda wake nchi yetu itakua miongoni mwa nchi zenye uchumi mkubwa na imara barani afrika, na tutaingia katika nchi zenye uchumi wa kati.

Huu ndo utabili wangu kulingana na uzoefu wangu katika siasa za nchi yangu. Buriani chadema, buriani ukawa, buriani ufisadi, unafiki na siasa chafu. Karibu sana sana uadilifu, maendeleo kwa wote na uchumi imara na madhubuti nchini. Zaidi ya yote uchaguzi wa mwaka huu utavunja rekodi kwa kufanyika kwa amani, haki na usawa. Amani usiamini ujumbe huu utakua shahidi baada ya miezi kadhaa kwamba utabiri wangu ni kweli. MUNGU ibariki tz, Mungu mbariki Dr. J.P Magufuli, Mungu wabariki wapiga kura wenye moyo wa uadilifu na uzalendo kama mimi.

Waaibike, wafedheheke, wanaojali maslahi ya vyama vyao bila kujali maslahi mapana ya taifa letu tukufu la Tanzania. Amen.
 
Kumbe ni profesa wa Kutabiri, wakubwa wako walitabiri atakayegombea na
Kikwete atakufa mwisho wakafa wao wenyewe.... TUNATAKA MABADILIKO NJE
YA CCM.
 
yani ukishakuta unaikana ccm yako na kujiweka kati huku ukishindwa kuficha mahaba yako kwa chama chako chakavu kinachokanwa hata na mgombea wenu ujue wewe na lichama lako na mgombea wenu asojua hata kisw. mnaelekea motoni jiandae kuungua au una siku tatu tu za kutubu mmekwishaaaaa!!!
 
Ukweli mchungu. Haya ngoja wakwambie ukachukue buku saba yako Lumumba!
 
Hilo ni wazo lako, tanzania tuna about 45 mil kila mtu ana wazo lake. Amini hivyo nami nina wazo langu tofauti na ww.
MIMI NAAMINI KAMA CCM ITASHINDA NA AHADI WALIZOTOA ZA JUMLA YA TRILLIONI ZAIDI YA 80 AMBAZO HAZITATEKELEZEKA ZITAIFUTA KABISA CCM KATIKA RAMANI AU MEDANI YA SIASA BAADA YA MIAKA MITANO. HIVYO ZITAIPA CHADEMA NA UKAWA NGUVU KUBWA MNO. NA ACT ITAKUFA RASMI BAADA YA UCHAGUZI MAANA HAITASHINDA KITI CHOCHOTE CHA UBUNGE NA HAITAKUWA NA FEDHA YA KULIPA VIONGOZI WAKE NA TUTAISIKIA TU. HAYO MAONI YANGU LAKINI.
TUNAOMBA NA MAONI YA WENGINE
 
Join Date : 11th October 2015
Posts : 4
Rep Power : 0
Likes Received2
Likes Given2
 
Kama mchambuzi wa maswala ya siasa hapa nchini nisiyekua na chama chochote, huu ndo utabiri wangu kwa siasa za nchi yetu katika miaka 10 ijayo;

CCM itashinda uchaguzi mkuu kwasababu wamesimamisha mgombea mwadilifu, mzalendo wa kweli, mchapakazi, mwajibikaji na mwajibishaji, kimsingi wamesimamisha 'masihi' wa aina yake. Ukawa itashindwa na kulalamika kua wameibiwa kura naam SIRAHA YA MUOVU YOYOTE NI UONGO. Ukawa watashindwa kwasababu wanachama wa upinzani waliochukizwa na kitendo cha ukawa kumpokea fisadi papa, wengi watampigia magufuli, naam waliokua wafuasi wa DR. SRAA na PROF. LIPUMBA wataongeza kura zao kwa Dr. Magufuli, wasomi wengi wazalendo kama mimi tuliokua tunaichukia sana ccm lakini kwa ccm kumsimamisha kiongozi mahiri na madhubuti msomi wa PhD, wengi tutaongeza kura zetu kwa TINGATINGA na kumpa ushindi
.

Vyama vinavyounda ukawa yaani Chadema, cuf, nccr na nrd vitapoteza ushawishi wao kwa wananchi baada ya kushindwa vibaya katika uchuguzi mkuu. Chadema, cuf, nccr na nrd vitafifia katika ramani ya siasa nchini kama si kufutika kabisa. Hivyo wanachama wengi sana wa chadema na vyama vinavyounda ukawa watahamia ACT na CCM, hivyo CCM na ACT vitaongeza ushawishi wao kwa wananchi na kupata wafuasi lukuki kutoka ukawa. Ndipo ukawa na vyama vyake vitafutika au kufifia katika ramani ya siasa nchini huku CCM na ACT viking'aa zaidi na kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za tz. Hivyo kwa miaka kumi ijayo na zaidi tutabaki na vyama viwili tu vikubwa, CCM na ACT. Nini kitatokea nchin kipindi cha miaka kumi ijayo? Siasa ya nchi itabadilika kutoka siasa za matusi, vurugu, propaganda chafu n.k na kua siasa safi kwa maendeleo ya nchi. Kutokana na uongozi safi na bora wa kiongozi mahiri na madhubuti Dr. John Pombe Magufuli, viongozi watawajibika na kuwajibishwa, uchumi wa nchi utakua kwa kasi na kuimalika, nchi itaendelea mara kumi zaidi kuliko kipindi cha jakaya, na baada ya magufuli kumaliza muda wake nchi yetu itakua miongoni mwa nchi zenye uchumi mkubwa na imara barani afrika, na tutaingia katika nchi zenye uchumi wa kati.

Huu ndo utabili wangu kulingana na uzoefu wangu katika siasa za nchi yangu. Buriani chadema, buriani ukawa, buriani ufisadi, unafiki na siasa chafu. Karibu sana sana uadilifu, maendeleo kwa wote na uchumi imara na madhubuti nchini. Zaidi ya yote uchaguzi wa mwaka huu utavunja rekodi kwa kufanyika kwa amani, haki na usawa. Amani usiamini ujumbe huu utakua shahidi baada ya miezi kadhaa kwamba utabiri wangu ni kweli. MUNGU ibariki tz, Mungu mbariki Dr. J.P Magufuli, Mungu wabariki wapiga kura wenye moyo wa uadilifu na uzalendo kama mimi.

Waaibike, wafedheheke, wanaojali maslahi ya vyama vyao bila kujali maslahi mapana ya taifa letu tukufu la Tanzania. Amen. Kama wewe ni mzalendo, share na wenzako. Amen.

SIKOTAYARI KUMJIBU MPUMBAVU YOYOTE KWANI MPUMBAVU NI ZAIDI YA KICHAA, naam maarifa ya mpumbavu ni matusi naye ni rafiki wa ufisadi (FISADI PAPA), umasikini (AKILI MASIKINI), Ujinga (KUTOKUJUA MAMBO) na MARADHI

Wewe jifariji hivyo tu,mimi sipendi wanafki kama wewe eti huna chama wakati wewe ni mtoto wa kigogo fulani
 
CCM wakae pembeni angalao miaka mitano tu,alafu wamrudishe huyo Magufuli.Bora fisadi mmoja Chadema kuliko.mafisadi mia ndani ya CCM Magufuli akishinda ataingia kwenye mfumo huohuo wa CCM ambao umeshindwa kufurukuta kwa miaka 54.Atafanikiwa kupoga kelele kwa muda tu mwiso atachoka kama JK na watu kama.yeye wakichoka wanachoka vibaya
 
kama wachambuzi wenyewe ni aina yako, basi taifa lina angamia! mwandiko wenyewe kama nyumba ya buibui.we unafaa uwe mganga wa kienyeji ukachole makombe.sasa wewe nimchambuzi au mtabiri?
 
kama wachambuzi wenyewe ni aina yako, basi taifa lina angamia! mwandiko wenyewe kama nyumba ya buibui.we unafaa uwe mganga wa kienyeji ukachole makombe.sasa wewe nimchambuzi au mtabiri?
Hiyo inaitwa IT Masaki team under supervision of Kambakamba Junior.
 
Napata kichefuchefu. Msomi gani asiyejua tofauti ya silaha na siraha, utabiri na utabili? Hata jina la Slaa linalotajwa na kuandikwa kila siku hujui spelling zake? Wewe kweli ni msomi wa Dar University kama rais wako anayesema 'Southand'. Ili uwe credible lazima ujue kuandika sahihi na kuzungumza sahihi katika lugha unayoitumia. Ndiyo maana hata siipi nadharia yako umuhimu wowote, maana kama uko careless kwenye kuandika ni dhahiri uko careless katika kufikiri!
 
katika wachambuzi uchwara tena wasio jua na namna ya kuchambua maada na ww umo

yaani na uwezo wa kujua kwamba hata kama ukawa wakikosa urais basi wingi wa wabunge utakuwa fimbo kwa ccm hujui unatuambia chama ambacho hakitapata zaid ha viti vinne bungeni
 
Back
Top Bottom