Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,233
- 8,779
Nimefuatilia kimyakimya lakini kwa umakini mkubwa shauri la Lissu Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu Ubunge wake. Kuanzia siku alipowasilisha Maombi yake hadi leo ulipotolewa uamuzi wa kuyatupilia mbali mapingamizi ya awali ya Serikali, nimefuatilia.
Ukitazama muitikio wa watu kuhudhuria shauri la Lissu Mahakama Kuu; majopo yaliyoshiba ya Mawakili Wasomi wa pande zote za shauri na jinsi uamuzi wa leo ulivyopokelewa mahakamani na kwingineko, utakubaliana nami kuwa Lissu si tu ni maarufu ila ni mtu 'mzito' kwenye uga wa kisiasa wa Tanzania.
Bila kuzingatia kitakachotokea mwisho wa Maombi ya Msingi ya Lissu yanayoendelea kuishi Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya Uamuzi wa Jaji Matupa leo wa kutupilia mbali mapingamizi ya Serikali, shauri hilo limeshatoa picha kumhusu Lissu: si mtu wa kubezwa.
Natabiri kuwa Lissu atagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2020 kupitia chama chochote cha upinzani na atakuwa mpinzani mkuu wa mgombea wa CCM ambaye natabiri atakuwa Rais wa sasa Jemedari Dr. John Pombe Magufuli.
Kwakuwa tumeshawajua, tuwafuatulie na tuwachambue uimara na udhaifu wao kwa staha na kwenye mtazamo wa kujenga nchi yetu pendwa ya Tanzania. Muda ukifika, tumchague Rais wetu wa Tanzania kwa miaka miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2020.
Muda ukifika na utabiri wangu kutimia, nitamchagua wa kusimama naye!
WATANZANIA AMKENI
CCM KATU HAIWEZI KUKUBALI DEMOKRASIA IFUATE MKONDO WAKE
KIHISTORIA-- CCM NI AFRO SHIRAZI + TANU
AFRO SHIRAZI haikukubali Demokrasia kufuata mkondo ake na ikatafuta msaada wa Tanu Tanganyika na kupindua matakwa ya wananchi
TANU - Baada ya kupata Uhuru , NYERERE alivifungia vyama vyote vya upinzani na kuanzisha mfumo wa Chama kimoja
KWA HALI HII CCM NI CHAMA KISICHOKUBALIANA NA MAAMUZI YA WANANCHI NA TOKEA MFUMO WA UCHAGUZI KUANZA WANAENDELEZA UHARAMIA WAO