Uchaguzi 2020 Utabiri wangu 2020: Ni Dr. John Pombe Magufuli (CCM) na Wakili Msomi Tundu Antipas Lissu (Upinzani) Urais. Tuwafuatilie; tuwachambue na tuwachague!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,188
25,493
Nimefuatilia kimyakimya lakini kwa umakini mkubwa shauri la Lissu Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu Ubunge wake. Kuanzia siku alipowasilisha Maombi yake hadi leo ulipotolewa uamuzi wa kuyatupilia mbali mapingamizi ya awali ya Serikali, nimefuatilia.

Ukitazama muitikio wa watu kuhudhuria shauri la Lissu Mahakama Kuu; majopo yaliyoshiba ya Mawakili Wasomi wa pande zote za shauri na jinsi uamuzi wa leo ulivyopokelewa mahakamani na kwingineko, utakubaliana nami kuwa Lissu si tu ni maarufu ila ni mtu 'mzito' kwenye uga wa kisiasa wa Tanzania.

Bila kuzingatia kitakachotokea mwisho wa Maombi ya Msingi ya Lissu yanayoendelea kuishi Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya Uamuzi wa Jaji Matupa leo wa kutupilia mbali mapingamizi ya Serikali, shauri hilo limeshatoa picha kumhusu Lissu: si mtu wa kubezwa.

Natabiri kuwa Lissu atagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2020 kupitia chama chochote cha upinzani na atakuwa mpinzani mkuu wa mgombea wa CCM ambaye natabiri atakuwa Rais wa sasa Jemedari Dr. John Pombe Magufuli.

Kwakuwa tumeshawajua, tuwafuatulie na tuwachambue uimara na udhaifu wao kwa staha na kwenye mtazamo wa kujenga nchi yetu pendwa ya Tanzania. Muda ukifika, tumchague Rais wetu wa Tanzania kwa miaka miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2020.

Muda ukifika na utabiri wangu kutimia, nitamchagua wa kusimama naye!
 
Mimi huwa sipendi mambo ya siasa wala chochote kinacho husiana, nilijua kubadilisha system ni mpaka ma admin wakubali whatever happen mda huo ntakua singapore ntakua nakoment jf kujua nini kinaendelea kwa Tz wenzangu
 
Huu ni uchuro.
Lisu ana kesi haijaisha kusema haya ni kumchuria.maana watawala watazidi kutaka kumbana.
Watawala wenyewe wana Meno ya mamba
 
Masahihisho : Kamati kuu ya ccm kwa kauli moja imekubaliana kutopitisha jina la Magufuli , japo tunafahamu Lissu atawakilisha wapinzani lakini kwa ccm siyo uliyemtaja
Mkuu kupata vichekesho kama hivi unapiga ngapi....
 
Masahihisho : Kamati kuu ya ccm kwa kauli moja imekubaliana kutopitisha jina la Magufuli , japo tunafahamu Lissu atawakilisha wapinzani lakini kwa ccm siyo uliyemtaja
Ccm ipi hiyo mkuu? Hii ya kina Musiba?😂😂😂
 
Back
Top Bottom