Utabiri wa Siasa na Uchumi kwa mwaka 2021

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,219
Nianze kwa kusema utabiri wangu utajikita zaidi kwenye hali yakisiasa na uchumi ila ikiwa tu serikali yangu haito badili sera za uchumi kwa walizo kuw nazo ktk mwaka 2020.

Ajira niwazi kuwa kwa kipindi kimepita sera za serikali haziku stimulate uajiri ktk secta nyingine ukiacha ujenzi ndio secta imenufaika zaid. Hivyo kuna dalili idadi ya vijana wasio kuwa na ajira itazidi kuongezeka ikiwa sera za kubana matumizi itaendelea nakupeleka pesa kwenye miradi mikubwa na kuongeza miradi mpya. Hivyo watafuta ajira wenzangu kwenye hili tujipange.

Pato la mtu binafsi litashuka au kupanda ikitegemea aina ya secta uliopo

Uwezo wa kununua purchasing power utazidi kushuka ikiwa sera ya serikali yakubana na kuto ongeza mishahara itakuwa kama ya miaka ilio pita ikumbukwe wafanyakazi ndio wanunuzi wakubwa ilakutokana na sera za kubana matumizi wafanyakazi wamejikuta na wao wakibana kuweza pata fedha yakujikimu mambo mengine.

Kuwepo na tetesi za makampuni kupunguza watu niukweli usio pingika kutokana na sera za kikodi Taz Administratio act 2015 pamoja na mabadiliko madogo ya 2017 makampuni mengi yapo kwenye mtihani wa either kulipa madeni ya serikali na kushindwa jiendesha au kupunguza watu ili wawezi kujiendesha japo kwa hasara ila wapate chochote kitu. Ktk hali kama hiyo Taasisi nyingi zitakapo shindwa pata misamaha ya kodi basi tujiandae kwa option ya kupunguza. Secta binafsi kama taasisi za mawasiliano, usafirishaji na fedha zitaumia sana na kupunguza watu.

Secta ya kifedha na miamala ya fedha uwenda pia ikatikisika kutokana na sheria ngumu za kifedha zitakazo sababisha kupigwa fine kubwa na kufunga biashara.

Biashara ndogo za vitu vidogo vidogo lina athiriwa na soko la china na kodi za ndani hivyo wale wafanyabiashara tufanye biasha kwa u smart kuepuka hasara.

Secta ya kilimo ndani na nje ndio secta itafanya vizuri kwa watu watawekeza vizuri kwenye hii secta watafurahia.

Madini pia itafanya vizuri kutokana na sera zilizopo japo bado sijajuwa kwa upande wa kodi.

Siasa...

Nitaendelea..
 
Hali ya kiuchumi inaenda kuwa mbaya zaidi, pato la mtu mmoja mmoja litaathirika sana, wafanyakazi wa umma wataendelea kuwa na hali ngumu, sekta binafsi itazidi kudidimia.

Hata misaada toka nje inayosaidia bajeti yetu nayo itapungua sana kama sio kukoma kabisa na hili litasababisha wizara nyingi kushindwa kupata pesa wanazohitaji toka serikali kuu kwaajili ya matumizi yao.

Lakini pamoja na hayo yote, wapo waimba taarabu wanaoendelea kuisifia serikali kama kasuku, hawa hawajielewi wala hawaelewi chochote kuhusu maendeleo ya mtu mmoja mmoja, wanaimba mapambio kutwa wakati utakuta wanashindia mlo mmoja kama misukule, kuwa na watu wa aina hii kwenye taifa changa na masikini kama letu ni laana.

Na wengi wao wanajidanganya sisi sio masikini, hawakumbuki nusu ya bajeti yetu inategemea misaada toka kwa wafadhili ambao tumewakasirisha kwa mambo ya kishamba CCM waliyofanya kwenye uchaguzi.

Bila misaada ya wazungu tunakuwa na bajeti hewa kila siku isiyotekelezeka, wanaona raha kutaja tu zile tarakimu (trilioni & bilioni) kule bungeni wakati wa bajeti, lakini ukija kwenye uhalisia hawapeleki hata nusu ya mahitaji kwa wizara husika, matokeo yake wizara zinashindwa kujiendesha kwa ufanisi.

Ukweli wa aina hii wapo wajinga wasiotaka kabisa kuusikia, wanaona raha kuendelea kuishi ndotoni huku wakijiliwaza kwa uwepo wa Bombardier angani, wanaishi kama mazombi wa old stone age.
 
Serikali iondoe mrundikano wa posho kwa wabunge na fedha itakayookolewa iingizwe kwenye mfuko wa bima ya afya kwa watu wote!
 
Serikali iondoe mrundikano wa posho kwa wabunge na fedha itakayookolewa iingizwe kwenye mfuko wa bima ya afya kwa watu wote!

Jiwe hana akili ya uchumi, anachojua ni ujenzi wa miundombinu kwa kutoza kodi za shuruti. Kwa maneno marahisi anamkamua ng'ombe ambaye hajamlisha. Sioni ni wapi atapata shilingi 10t+ kwa ajili ya kumalizia miradi miwili ya SGR & SG. Naona uchumi ukienda kuanguka moja kwa moja. Na hakuna uwezekano wa wakezaji serious kuja baada ya wafanyabishara wa Bureau de change kuporwa hela zao.
 
Hali ya kiuchumi inaenda kuwa mbaya zaidi, pato la mtu mmoja mmoja litaathirika sana, wafanyakazi wa umma wataendelea kuwa na hali ngumu, sekta binafsi itazidi kudidimia.

Hata misaada toka nje inayosaidia bajeti yetu nayo itapungua sana kama sio kukoma kabisa na hili litasababisha wizara nyingi kushindwa kupata pesa wanazohitaji toka serikali kuu kwaajili ya matumizi yao.

Lakini pamoja na hayo yote, wapo waimba taarabu wanaoendelea kuisifia serikali kama kasuku, hawa hawajielewi wala hawaelewi chochote kuhusu maendeleo ya mtu mmoja mmoja, wanaimba mapambio kutwa wakati utakuta wanashindia mlo mmoja kama misukule, kuwa na watu wa aina hii kwenye taifa changa na masikini kama letu ni laana.

Na wengi wao wanajidanganya sisi sio masikini, hawakumbuki nusu ya bajeti yetu inategemea misaada toka kwa wafadhili, bila misaada ya wazungu tunakuwa na bajeti hewa kila siku isiyotekelezeka, wanaona raha kutaja tu zile tarakimu (trilioni & bilioni) kule bungeni wakati wa bajeti, lakini ukija kwenye uhalisia hawapeleki hata nusu ya mahitaji kwa wizara husika.

Ukweli wa aina hii wapo wajinga wasiotaka kabisa kuusikia, wanaona raha kuendelea kuishi ndotoni wakijiliwaza kwa uwepo wa Bombardier angani, wanaishi kama mazombi wa old stone age.
Uko na negativity kinoma!
 
Unataka niweke positive kwenye negative? you must be mad while i'm not, huo ndio ukweli mchungu muusome na kuuelewa.
Siwezi kuusoma upupu.

Nahighlight kwanza, ndio kama ni ujumbe mzuri ninausoma.
 
Naendeleza utabiri. Serkali yenye kupenda misifa, itapika data za ukusanyaji mapato na kudanganya kuwa mapato yanazidi kuongezeka. Lakini sisi raia wa kawaida, cha moto tutakiona.
Serikali iondoe mrundikano wa posho kwa wabunge na fedha itakayookolewa iingizwe kwenye mfuko wa bima ya afya kwa watu wote!
 
Unataka niweke positive kwenye negative? you must be mad while i'm not, huo ndio ukweli mchungu muusome na kuuelewa.
Kama ndio huo ukweli nani atausoma na kuelewa, wewe je unajitoa!

Hao walishindwa kwenye sanduku la kura sasa mnawasaidia kujifariji kwa dua mfu. WAPE POLE na waendelea kuomba dua ovu ziwarudie wenyewe
 
Kama ndio huo ukweli nani atausoma na kuelewa, wewe je unajitoa!

Hao walishindwa kwenye sanduku la kura sasa mnawasaidia kujifariji kwa dua mfu. WAPE POLE na waendelea kuomba dua ovu ziwarudie wenyewe
Walishindwa na nani kwenye sanduku la kura; Polisi? NEC, Wakurugenzi, au Kura feki?

Amka ndotoni, dunia nzima iliona lile igizo lenu la Oktoba 28.
 
Binafsi naona misaada mingi ya wahisani itapungua kutokana na kuyeyuka kwa demokrasia.

Bila ya misaada tujiandae kufunga mikanda
 
Serikali iondoe mrundikano wa posho kwa wabunge na fedha itakayookolewa iingizwe kwenye mfuko wa bima ya afya kwa watu wote!
Hii ni piont nzuri sana. Na ikiwezekana wapungizwe mshahara. Ila bunge hili nani atakae kubali hiyo proposal?
 
Back
Top Bottom